MRATIBU WA WAJASILIAMALI NA HAKI ZA KAZI KWA WALEMAVU WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA HUSSEIN GEYA AKISOMA RISALA MBELE YA NKUU WA WILAYA YA UYUI LUCY MAYENGA |
MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALEMAVU MANISPAA YA TABORA JOHN KUKA AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA UYUI KWA AKIJI YA KUFUNGUA MAFUNZO |
MKUU WA WIALAYA UYUI LUCY MAYENGA AKIFUNGUA MAFUNZO YA UJASILIAMALI NA HAKI YA KAZI KWA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA UKUMBI WA KITUO CHA WANAFUNZI MJINI HAPA LEO |
NA LUCAS RAPHAEL TABORA
Halmashauri ya wilaya uyui mkoani Tabora kwa mwaka huu
imetenga kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya kuwakopesha vijana na wanawake ili kuweza kujiongezea
kipato na kujiunga katika vikundi .
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Uyui Lucy mayenga
wakati akifungua mafunzi ujasiliamali na haki za kazi kwa walemavu iliyofanyika
katika ukumbi wa kituo cha wananafunzi mjini hapa .
Alisema kwamba fedha hizo zitolewa katika makundi hayo ambapo
vijana wametengewa kiasi cha shilingi milioni 20 na wanawake wametengewa kiasi
kama hicho.
Alisema kwamba fedha hizo ukopeshwa kwa riba nafuu ili
kuwawezesha vijana na kinamama kufanya
marejesho bila maumivu .
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka walemavu hao kujiunga katika
vikundi ambavyo vimesajiliwa na kuandaa andiko sanjari na kuwa na wathamini.
Awali mratibu wa mafunzo hayo Hussein Geya alisema kwamba
mafunzo hayo yanalengo la kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu kupitia
vikundi vya wajasiliamali vya watu wenye ulemavu kutoka katika wilaya hiyo ya
uyui vilivyowezeshwa kikamilifu na kutambulika kisheria.
Alisema kwamba katika kipindi cha utekelezaji mradi huo
shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kutoa elimu kwa ajia ya redio na televishini
,kuendesha mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali kwa watu wenye ulemavu .
Mafunzo hayo
yameandaliwa na chama cha walemavu wilaya ya uyui mkoani Tabora na kufadhiliwa
na shirika la Akiba Uhaki Foundation la nchini kenya
No comments:
Post a Comment