Katibu wa Imetosha Salome Gregory akifuatiwa na Balozi Mdimu na Issaya Mwakilasa(wakuvwang) wakiteremka toka ndegeni leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Mwanza. |
|
Ujumbe
wa taasisi ya Imetosha inayojishughulisha na utoaji elimu juu ya
kumaliza unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini
uliwasili jijini Mwanza leo hii saa 2 asubuhi kwa ziara ya siku 3 ambapo
kati siku hizo tatu ujumbe huo utakutana na viongozi wa ki serikali na
usalama wa baadhi ya mikoa na wilaya za kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na
Shinyanga. Lengo la mikutano hiyo ni kamati kujitambulisha kwa viongozi
hao na kuwaeleza nini Imetosha inatarajia kufanya katika kanda hii mwezi
ujao ambako pamekuwa na matukio mengi ya ukatili na mauaji kwa watu
wenye ualbino nchini Tanzania.
Vile vile kamati itakuwa na siku moja ambapo itatembelea vyombo ya habari vya jijini hapa kabla ya kurejea Dar es Salaam.
Habari na picha na Mkala Fundikira wa Mkalamatukio/keronyingi blog
No comments:
Post a Comment