Naibu
Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa ameambatana
na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda
(kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Prof. Isaya Jairo
kabla ya kuzindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi
hiyo katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na
Mbeya.
Naibu
Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizindua Baraza la
Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo mjini
Bagamoyo.
Wajumbe
wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)
wakiimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya kuanza kwa mkutano wao leo
mjini Bagamoyo.
Wajumbe
na viongozi wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza
hilo leo mjini Bagamoyo. Picha na Aron Msigwa/MAELEZO.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
SERIKALI
imeyata Mabaraza ya wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu kote nchini
kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi, kanuni na sheria
zinazosimamia mabaraza hayo ili yawe chachu katika kuleta maendeleo ya
Elimu na mabadiliko ya kiuchumi ya taasisi hizo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba
wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi
hiyo katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na
Mbeya.
Mhe.
Mwigulu amesema kuwa iwapo mabaraza hayo yatazingatia weledi katika
kusimamia masuala mbalimbali ya taasisi hizo nchini yataleta mabadiliko
ya kiutendaji katika usimamizi wa mapato na matumizi na kutoa ushauri
utakaoisaidia Serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
Mhe.
Mwigulu ameeleza kuwa endapo mabaraza hayo yataacha kufanya kazi kwa
mazoea na kujikita katika kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa,
taasisi hizo zitaongeza uzalishaji, zitakuza mapato na kutatua kero
mbalimbali za wafanyakazi mahali pa kazi.
“
Napenda niweke wazi kuwa mabaraza haya ni muhimu sana kwa wafanyakazi,
hayana tofauti na bunge ,kazi yake kubwa ni kusimamia mapato na
matumizi, kushauri taasisi na Serikali juu ya utekelezaji wa mipango
mbalimbali ikiwemo ajira kwa watumishi wapya” Amesisitiza.
Akizungumzia
changamato ya uhaba wa walimu na watumishi wa kada mbalimbali katika
taasisi hiyo na taasisi nyingine za Umma za Elimu ya juu amesema
Serikali inaendelea kutenga fedha katika bajeti ya kila mwaka ili
kuondoa tatizo hilo.
Aidha,
amesema Serikali inaendelea kulishughulikia suala la usimamizi wa ziada
ya mapato yanayozalishwa na taasisi za umma ili yaweze kupelekwa
katika maeneo mengine yenye uhitaji.
“Serikali
tunaendelea kuangalia utaratibu wa kutumia ziada ya mapato
inayozalishwa na taasisi mbalimbali za umma ili iweze kupelekwa katika
maeneo mengine yenye uhitaji maana fedha hizi ni za umma,taasisi moja ya
Serikali haiwezi kung’ania ziada ya mapato iliyozalisha, hizo ni fedha
za umma lazima zikafanye kazi maeneo mengine yenye uhitaji hasa kwenye
kugharamia mahitaji ya wodi za akina mama kote nchini”
Pia
amesisitiza mkakati wa Serikali wa kuzifanya taasisi hizo za elimu ya
juu kuwa na mamlaka yake katika kuajili watumishi wake na kjitegemea.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ndiye Mkuu wa Taasisi ya
Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda akizungumza na wajumbe wa baraza
hilo amesema kuwa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka 5 imepata
mafanikio makubwa ya kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi
Bilioni 6 za mwaka 2010 hadi kufikia shilingi Bilioni 18 mwaka
2014/2015.
Amesema
Taasisi hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
uhaba wa miundombinu, ufinyu wa bajeti , uhaba wa walimu wenye shahada
za uzamivu (PhD) na watumishi kimeendelea kupata idadi kubwa ya
wanafunzi wanaodahiliwa kutoka 7635 waliodahiliwa mwaka 2011/2012 hadi
kufikia 14974 mwaka 2014/2015.
“Licha
ya kuendelea kufanya vizuri taasisi yetu inakabiliwa na tatizo la
waalimu katika matawi yetu yaliyo mikoani ,jambo hili hutufanya tutumie
gharama kubwa kuwasafirisha kutoka makao makuu kwenda kufundisha
wanafunzi wetu wanaochukua michepuo ya Biashara, Uhasibu, Rasilimali
Watu, Ununuzi na Ugavi,Uhasibu katika Sekta ya Umma na Masoko na
Mahusiano kwenye matawi yetu” Amesisitiza.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya wizara ya Fedha wa Taasisi hiyo Prof.
Isaya Jairo akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano huo amesema
kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)katika kukuza na kuongeza mapato
ya ndani na kupunguza utegemezi kutoka serikalini itaendelea kufanya
shughuli kibiashara ,kufanya utafiti, kutoa ushauri katika Nyanja za
uhasibu, ununuzi na ugavi kote nchini.