Wednesday, March 5, 2014

CCM YAZIDI KUTESA KALENGA,MWENYEKITI CHADEMA AITABIRIA CCM USHINDI WA KISHINDO


 Mgombea ubunge Jimbo la Kalemnga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (kushoto) akijiunga kucheza ngoma ya asili ya kabila la wahehe iliyokuwa ikiongozwa na msanii maarufu wa filamu na muziki, Dokii wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kalenga leo katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini .Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema wa Kijiji hicho aliitabiria CCM ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
 Wafuasi wa CCM katika Kijiji cha Lupembelwasenga wakishangilia kwa furaha walipokuwa wakimlaki Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa kwenye mkutano wa kampeni leo.
 Msanii wa filamu na muziki, Dokii akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni hizo katika Kijiji cha Lupembelwasenga.
 Ofisa wa CCM Makao Makuu ya Umoja wa Vijana, Mwampamba ambaye alijitoa Chadema, akielezea kisa cha kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga na CCM.
 Mwenyekiti wa Chadema katika Kijiji cha Lupembelwasenga, Ezekiel Kibiki 9kushoto), akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo na kuamua kujiunga na CCM leo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Kalenga. Kibiki aliitabiria CCM ushindi katika uchaguzi huo. Pia amesema kuwa tayari amewashawishi wanachama wengine wa Chademe kujiunga na CCM.
 Wanakijiji cha Lupembelwasenga wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea uchaguzi wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo mchana.
 Mgimwa akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kikombwe leo.
 Dokii akiungana na wananchi kucheza ngoma ya asili ya kabila la wahehe katika Kijiji cha Kikombwe
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo, akichuchumaa ikiwa ni heshima ya kumuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akielezea mikakati ya chama hicho  kukigalagaza chama Chadema katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga leo mchana katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini.
IMG_1329
Godfrey Mgimwa akijinadi katika mkutano wa  kampeni leo katika Kijiji cha Kikombwe. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO).

AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI MHE. RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO


D92A2847 D92A2857 D92A2868 D92A2877Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua madaraja ya kijeshi yakiwemo yale ya kuelea juu ya maji wakati alipokagua zana za kijeshi jana, Jumatatu, Machi 2, mwaka huu, 2014. (Picha na Freddy Maro wa Ikulu).

RAIS DR.JAKAYA KIKWETE AKAGUA MADARAJA YA KIJESHI


 

·        ARIDHISHWA NA UTIMAMU WA VIKOSI HIVYO KIMAFUNZO NA ZANA

·        AAHIDI TATIZO LA MAJI KUPATIWA UFUMBUZI NDANI YA MWAKA 2014
·        KIKOSI CHA UHANDISI WA MEDANI CHAAHIDIWA VIFAA ZAIDI ILI KUPAMBANA NA MAJANGA NCHINI
·        AAGIZA JWTZ KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOKANA NA MAKAZI YA MUDA
Ziara hiyo ya siku moja ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
(Na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT)
1Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando 2Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro. 3Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake. 5Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha. 6Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake. 7Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani). 8Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa. 9Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa. 10Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi. 11Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya  mitambo mipya inaotumiwa na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa maji safi na salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani. 12Akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani. 13Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.

MTOTO WA MIAKA MITANO ABAKWA NA BABA YAKE MZAZI,MAMA ACHOMWA MOTO KIFUANI-TABORA


Mwasiti Juma(21) akiwa na familia yake yenye watoto watatu hivi sasa amepata hifadhi katika Kambi ya kulelea watu wasiojiweza ya kijiji cha Amani manispaa ya Tabora baada ya kukumbwa na mkasa wa kufanyiwa ukatili wa kuchomwa moto kifuani na Mumewe anayefahamika kwa jina la Hamisi Kajuguja tukio ambalo lilitokana na mwanamke huyo kumkea mumewe wakati alipomkuta akimbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano ambaye pichani amevaa t.shirt nyeupe pembeni ya mama yake.
Mwasiti  ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nzubuka manispaa ya Tabora ameuambia mtandao huu kuwa mumewe amekuwa akimfanyia matukio mbalimbali ya ukatili kwa muda mrefu sasa na amekuwa akijaribu kuachana naye mara kadhaa lakini inashindikana,Matukio ya vitisho vya kuuawa yanayokwenda sambamba na vipigo imekuwa ni hali ya kawaida lakini jambo baya zaidi linaloendelea kumhuzunisha ni pamoja na hilo la kumbaka mtoto huyo ambalo limedumu kwa muda wa miaka miwili sasa.
Mtoto huyu  mwenye umri wa miaka mitano ndiye amekuwa akibakwa na baba yake kwa muda wote huo.Akielezea kwa undani zaidi kuhusu tukio hilo la ubakaji mama wa mtoto huyu Bi.Mwasiti Juma alisema mumewe kila siku ifikapo majira ya saa kumi na mbili asubuhi alikuwa akimuamsha na kumuaru kwenda kuchota maji kisimani huku yeye mwanaume huyo Hamisi Kajuguja akibakia na watoto nyumbani ambapo hupata fursa ya kufanya mchezo huo mchafu jambo ambalo pia linathibitishwa na mtoto mwingine huyo mwenye t.shirt   nyekundu kwenye picha ya juu kabisa....Hata hivyo Mwasiti baada ya kuchoshwa na matukio hayo ya mumewe aliamua kukimbia na watoto wake hao watatu hadi Tabora mjini mahali ambako alipata msaada wa kisheria ikiwa ni pamoja na kufika kituo kikubwa cha Polisi Tabora kuripoti adha hiyo hatimaye zoezi la kukamatwa kwa mumewe lilifanikiwa huku yeye Mwasiti pamoja na familia yake akipatiwa hifadhi ya muda kijiji cha kulelea watu wasiojiweza cha Amani.


"RASIMU YA KATIBA NDIO NINI?"-WAUZA VITUMBUA


Salma Abas  ambaye ni mpishi na muuzaji wa vitumbua Stendi mpya ya mabasi Tabora mjini,wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wetu kuhusu ufahamu wake juu ya RASIMU  YA KATIBA MPYA ambapo alisema yeye pamoja na washirika wenzake wanaofanya biashara ndogo ndogo hawajui chochote wamekuwa wakisikia tu kwenye vyombo vya habari na tena wanaona mambo hayo ya Rasimu yanawahusu zaidi viongozi na si kwa wao......."Mara tusikie wapo Bungeni huko Dodoma wanataka waongezewe pesa eti laki tatu kwa siku haiwatoshi kwa kujadili hiyo Rasimu kwani ndio kitu gani?...na sisi Wauza vitumbua itatusaidia nini?Baadhi ya Wauza vitumbua hapa Stendi mpya ya mabasi ndivyo walivyo na uelewa huo juu ya Rasimu ya Katiba mpya......SWALI LA MSINGI :-Itakapofikia hatua ya kupigia kura Katiba hiyo nini watafanya watu kama hawa?   

"BABA ANATAKA NIOLEWE ILI APATE NG'OMBE WAKATI MIMI NI MLEMAVU NA NINA UMRI MDOGO SANA"



Moshi Hussein ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi nyumbani kwa baba yake mzazi huko katika kijiji cha Magiri wilaya ya Uyui mkoani Tabora,binti huyu anaumri wa miaka 13 hajawahi kupelekwa Shule kwa maana ya kupata haki kama wapatavyo watoto wengine,Moshi amekuwa akililia hilo kwa baba yake mzazi bila mafanikio.Jambo baya zaidi kwa mujibu wa maelezo ya Moshi baba yake anahitaji aolewe ili aweze kupata Ng'ombe  licha ya kuwa ana umri mdogo na hawezi kukabiliana na Changamoto za ndoa kulingana na ulemavu alionao.   
Moshi kwakuwa hana uwezo wa kutembea umbali hata wa hatua kumi anawaomba wasamalia wema kumsaidia mambo makubwa matatu,kwanza ikibidi kumuondoa nyumbani kwao ili aepukane na ndoa ya lazima,Pili apelekwe shuleni kwakuwa anaona kukaa kwa baba yake ni wazi kwamba atakuwa anatafuta umasikini mwingine wa ziada ukiachana huo wa ulemavu wa viungo ambao umekuwa kikwazo kikubwa hata cha kujihudumia masuala mengine ya kiutu wa mwanamke.Kwa mujibu wa maelezo yake Moshi ana mshangaa baba yake kwa uamuzi wa kutaka aolewe kwakuwa hata ndoa yenyewe haoni kama itakuwa na maana kutokana na ulemavu alionao na pia haoni sababu ya kuwa mzigo kwa mtu mwingine katika maisha yake. 
Moshi amekuwa akijikatia tamaa kulingana na ulemavu alionao,"Kama ningekuwa na mama labda hata ningeweza kupelekwa shule na mimi ningekuwa msomi kama wengine,lakini kwa hali hii ni bora hata ningekufa nimfuate mama yangu huko aliko" 


"CHAMA KIPYA CHA ACT CHASHUSHA BENDERA ZA CHADEMA KIGOMA"

 

Na Magreth Magosso, Kigoma.
CHAMA cha Alliance For Change and Transparency Mkoa wa Kigoma,kimeshusha Bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la Ujiji  stendi ya zamani na kupandisha bendera ya (ACT) wakati wa uzinduzi rasmi wa matawi sita katika manispaa ya kigoma ujiji.

 

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la kushusha bendera hiyo ni hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu wengine kwa kukosa haki ya kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho na
hivyo  kuanzisha  ACT kama chama cha  wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja.

 

Kabogo aliwataka wanachama wahitaji, wachukue kadi za ACT ili chama kipate usajili kamili kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu husika pamoja na kutoa michango endelevu ,ikiwa ni jitihada za makusudi kuhakikisha chama kinasonga mbele
kwa maslahi ya Taifa.

 

“Wananchi nyie ni chachu ya chama kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kukiamini  na kukipatia ridhaa kiweze kuleta
mabadiliko ya kimaendeleo” alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF kigoma.

 

Kwa upande wa Katibu ACT Kanda Magharibi Wiston Moga alisema, lengo la chama ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa siasa,ambapo wao wamedhamiria kutetea maslahi  ya umma kwa lengo la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambayo ni chachu ya vyama vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
 

Katika ziara hiyo ya uzinduzi wa matawi ya chama husika,ACT kimefanikiwa kufungua matawi kwenye kata sita kati ya kata 19 zilizopo katika manispaa ya kigoma ujiji,huku baadhi ya viongozi kutoka UPD,CHADEMA na CUF wakijiunga na chama hicho
kwa kudai wanahitaji chama chenye uchungu na kukabiliana na changamoto za wanyonge.

 

Hata hivyo  wanachama 3500 wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema katika tawi la Ujiji mkoani Kigoma wamehamia chama kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT).

"JAMAA ABADILIKA NA KUWA ALBINO BAADA YA KUTUMIA DAWA ZA MALARIA"-TABORA

 
Bw.Hafidh Masokola Damson ambaye alibadilika na kuwa Albino kutokana na matumizi ya dawa za Malaria baada ya kuzitumia mnamo mwaka 2010,Kwa maelezo yake mara baada ya kunywa dawa aina ya Metakelfin alianza kubabuka ngozi ya mwili wake huku magamba yakitoka mithiri ya nyoka. 
Hafidhi ambaye kwasasa anaishi Tabora mjini eneo la National Housing amebadilika maeneo yote ya viungo vya mwili wake isipokuwa meno pekee na kuwa albino hata kufikia hatua ya kujiunga na chama cha Maalbino Tanzania tawi la Tabora,kwa uthibitisho wa habari hii waweza kumpigia kwa simu ya kiganjani 0767 298 348 au 0658 298 348.
Hafidh Masokola kabla ya kubadilika kuwa mlemavu wa ngozi Albino.