Salma
Abas ambaye ni mpishi na muuzaji wa vitumbua Stendi mpya ya mabasi
Tabora mjini,wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wetu kuhusu
ufahamu wake juu ya RASIMU YA KATIBA MPYA ambapo alisema yeye pamoja na
washirika wenzake wanaofanya biashara ndogo ndogo hawajui chochote
wamekuwa wakisikia tu kwenye vyombo vya habari na tena wanaona mambo
hayo ya Rasimu yanawahusu zaidi viongozi na si kwa wao......."Mara
tusikie wapo Bungeni huko Dodoma wanataka waongezewe pesa eti laki tatu
kwa siku haiwatoshi kwa kujadili hiyo Rasimu kwani ndio kitu gani?...na
sisi Wauza vitumbua itatusaidia nini?Baadhi ya Wauza vitumbua hapa
Stendi mpya ya mabasi ndivyo walivyo na uelewa huo juu ya Rasimu ya
Katiba mpya......SWALI LA MSINGI :-Itakapofikia hatua ya kupigia kura
Katiba hiyo nini watafanya watu kama hawa? |
No comments:
Post a Comment