Thursday, January 3, 2013

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAHUDHURIA MSIBA WA MAREHEMU SAJUKI NYUMBANI KWAO TABATA BIMA LEO



Picha Kwa Hisani Ya Michuzi Blog

WIZARA YA HABARI, VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO TANZANIA YATUMA SALAAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA SAJUKI


 
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.


“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.

Dkt. Mukangara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja  na Revenge  ya Kampuni ya RJ 

Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers  kwa kushirikiana na Shija  Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk    
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
 
Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na  furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli  huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.

Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen

Imetolewa na:
Mkurugenzi
Idara ya Habari(MAELEZO).
Dar es Salaam.
2 Januari 2013

Wednesday, January 2, 2013

TAJIRI AMPIGA RISASI MLALAHOI BAADA YA KUDAIWA 15000 NZEGA



Levis Ndugu akiwa amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguu wa kushoto kufuatia alikwenda kudai pesa yake  shilingi 15000 baada ya kufanyakazi ya ujenzi kwa mkurugenzi wa kampuni ya Lekuni ya wilayani Nzega matokeo yake badala ya kupata haki yake hiyo aliyokuwa akidai kama ujira kwa kazi aliyoifanya imedaiwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Silvesta Msele alimfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mguu huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora ACP Anthony Rutha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mnamo tarehe 16 Desemba 2012 majira ya saa 12:45 jioni huko maeneo ya Kitongo wilayani Nzega.


Hata hivyo tukio hilo limeendelea kuzua malalamiko kwa baadhi ya wakazi wa wilayani Nzega huku wakitafsiri unyama wa aina hiyo umefanyika kutokana na kibri cha uwezo wa kifedha kwakuwa anayedaiwa kufanya unyama huo yupo mitaani akiendelea na shughuli zake huku majeruhi kijana Levis akiendelea kusota kwa kutibu majeraha aliyonayo ambayo yamesababisha kushindwa kuendelea na shughuli za utafutaji wa riziki yake ya kila siku.  


MR & MRS KAMNA WAPATIKANA USIKU WA MWAKA MPYA TABORA

 Katika ni mshindi wa kwanza wa shindano la Miss Kamna,Mariam Wilfred akifuatiwa na mshindi wa pili kulia ni Mwasiti Thabit,kushoto ni mshindi wa tatu  Sabrina Michael.
 Baadhi ya washabiki waliofurika katika ukumbi wa Theophilo Kisanji wakiwa wanashuhudia mashindano ya kuwasaka Mr. na Mrs Kamna usiku wa mwaka mpya.
 Washindi wa tano bora wakiwa Jukwaani mara baada ya kutangazwa wakisubiri kuulizwa maswali ili kujiongezea idadi ya point katika mashindano hayo yaliyokuwa na mvuto mkubwa.
 Majaji walikuwa na kazi ngumu ya kuhesabu na kutoa point kwa washindi katika mashindano hayo
 Huyu ndiye Mr.Kamna 2013 Daniel Kisanga muda mfupia mara baada ya kutangazwa mshindi katika mashindano hayo.
 Washindi wa tano bora kuwania Mr.Kamna 2013 wakiwa jukwaani wakisubiri maswali ya kizushi ambayo kwakweli yalikuwa ni mtihani mkubwa kwao.
 Washabiki
 Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kmchaya akicheza muziki wakati wa mashindano hayo akiwa na Naibu Meya manispaa ya Tabora Waziri Mrenda kulia,na kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora Moshi Nkonkota,ilikuwa ni mara baada ya kutimu saa sita kamili usiku hii ilikuwa ni ishara ya kuupokea mwaka mpya wa 2013. 
Hawa ni baadhi ya wadau wa TABORALEOHABARI.COM wakiwa katika moja ya pozz la picha ya pamoja wakati wa mashindano hayo.

Tuesday, January 1, 2013

WATANZANIA SASA WAFIKIA IDADI YA MIL.44.9 KUTOKA MIL.34.4


Rais Jakaya Kikwete ametangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi, Watanzania waongezeka kutoka watu milioni 34.4 hadi kufikia watu milioni 44.9.

TUWASA WASHEREHEKEA MWAKA MPYA KWA KUKAMATA WEZI WA MAJI


 Baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Tabora Tuwasa wakiwa katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaodaiwa kuiba maji ambapo walimkamata mkazi mmoja wa Kata ya Ipuli mtaa wa Nyerere anayefahamika kwa jina la Faston Byaba ambaye alikutwa amejiunganishia huduma ya maji kinyume cha sheria.

Mmoja kati ya mafundi wa Tuwasa akiwa amemkabidhi kifaa cha kuunganishia maji  mama aliyekutwa amejiunganishia huduma hiyo ya maji. 

"KUKATAA KUWEPO TEN PERCENT KWENYE MIRADI KWANIPONZA"

"KUKATAA KUWEPO TEN PERCENT KWENYE MIRADI KWANIPONZA"



Na Hastin Liumba,Uyui
 
SAKATA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, kumvua cheo cha ukuu wa idara ya maji, injinia Nestory Nicodemus, kwa tuhuma kadhaa, limechukua sura mpya baada ya injinia huyo kudai anawasiliana na wanasheria wake ili haki itendeke.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, injini Nestory Nicodemus, alisema kuwa suala lake limeendeshwa kimajungu na  uonevu na kwamba ametolewa kafara kwa chuki za baadhi ya watu.
 
Nicodemus alisema awali aliundiwa tume ya uchunguzi ambayo haikuzingatia kuwepo kwa changamoto kadhaa katika kile kinachoelezwa kuwa anatuhumiwa kwa uzembe, katika upotevu wa vifaa vya gari, kutokamilika kwa mradi wa maji na ujenzi wa vyoo 6 katika kata ya Kizengi.
 
“Tume niliyoundwa iliegemea upande mmoja na kwamba katika uchunguzi wao hawakuzingatia changamoto zilizoko kwenye miradi ninayotuhumiwa kutoikamilisha kwa wakati…..hii ni uonevu kwangu ikiwa ni kwa maslahi ya wachache wanaopenda ten percent.” Alisema
 
Akifafanua juu ya tuhuma hizo, injinia huyo alisema kuwa kuhusiana na mradi wa Water Sector Development Project-WSDP ulipatiwa kiasi cha sh milioni 20 ili kutekeleza ujenzi wa vyoo 6 lakini baadhi ya vifaa vilitumika kujenga nyumba kadhaa za walimu wa kata ya Kizengi.
 
Alisema licha ya mradi huo kutokamilika kwa wakati, tayari vyoo vitatu vilishakamilika, huku choo kimoja kikijengwa na wananchi, hali hiyo ya ujenzi wa nyumba za walimu na kutumika vifaa kadhaa kwenye ujenzi wa nyumba za walimu ndizo sababu zilizopelekea kutokamilika mradi huo kwa wakati na taarifa zake zipo.
 
Kuhusu tuhuma za kushindwa kukamilika kwa mradi wa maji makao makuu ya wilaya ya Uyui, Isikizya, alisema zipo sababu za msingi kwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo, PET Company Ltd, alipewa miezi mitano katika kazi yake ya uchimbaji wa mtaro lakini kutokana na mtaro huo kupita eneo la mashamba ya tumbaku wananchi waliomba hadi mavuno yao yaishe na mradi huo haukuwa na fedha za fidia.
 
Aliongeza kuwa suala hilo ofisi ya mkurugenzi ilikuwa na taarifa ikiwemo taarifa za mkandarasi kuomba siku 90 zaidi ili kukamilisha mradi huo, huku mradi huo pia ukichelewa kutokana na eneo hilo pia kuwa na mwamba na hivyo kazi hiyo kuwa ngumu na ya muda mrefu.
 
Kuhusu tuhuma za kutakiwa kurejesha kiasi cha sh milioni 4,420,640 ndani ya siku saba, ambazo zingejenga vyoo sita vya kata ya Msimba na Kizenge, inamshangaza kwani fedha hizo zipo kwenye akaunti benki kwani kama fedha hazikutumika ina maana zipo na hakuna wizi.
 
Alisema tuhuma nyingine ni kuhusiana na ununuzi wa mashine ya maji ya Diesel badala ya umeme, injinia Nicodemus alisema alifanya hivyo kutokana na agizo la aliyekuwa waziri wa maji Profesa Mark Mwandosya, kipindi cha mwaka 2010 alipofanya ziara kwani hakuwa na jinsi kutengua agizo la waziri hasa kutokana na kipindi hicho makao makuu ya wilaya hayakuwa na umeme.
 
Alisema maamuzi ya ununuzi wa mashine hiyo pia yalipitia kwenye vikao vya zabuni na taarifa zake zipo, huku suala la upotevu wa vifaa katika stoo ya maji kama mkuu wa idara liliripotiwa kituo cha polisi na uchunguzi unaendelea huku kampuni ya ulinzi ikijulishwa suala la mtumishi wao kuhusika na upotevu wa vifaa hivyo.
 
Aliongeza kuwa alichukua hatua kama mkuu wa idara ambaye anamwakilisha mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi.
 
Alimalizia kuwa kutokana na maamuzi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui kuketi kwenye kikao cha baraza maalumu na kumvua madaraka, amewasiliana na wanasheria wake kuangalia hatua za kuchukua ili haki zake kama mwajiriwa zipatikane.
 
Mnamo mwezi desemba 19 mwaka 2012 baraza la madiwani maalumu liliketi na kuazimia kumvua madaraka injini Nestory Nicodemus kwa uzembe wa tuhuma ainishwa.