"KUKATAA KUWEPO TEN PERCENT KWENYE MIRADI KWANIPONZA"
Na Hastin Liumba,Uyui
SAKATA
la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, kumvua cheo cha ukuu wa
idara ya maji, injinia Nestory Nicodemus, kwa tuhuma kadhaa, limechukua
sura mpya baada ya injinia huyo kudai anawasiliana na wanasheria wake
ili haki itendeke.
Akizungumza na waandishi wa habari, injini Nestory Nicodemus, alisema kuwa suala lake limeendeshwa kimajungu na uonevu na kwamba ametolewa kafara kwa chuki za baadhi ya watu.
Nicodemus
alisema awali aliundiwa tume ya uchunguzi ambayo haikuzingatia kuwepo
kwa changamoto kadhaa katika kile kinachoelezwa kuwa anatuhumiwa kwa
uzembe, katika upotevu wa vifaa vya gari, kutokamilika kwa mradi wa maji
na ujenzi wa vyoo 6 katika kata ya Kizengi.
“Tume
niliyoundwa iliegemea upande mmoja na kwamba katika uchunguzi wao
hawakuzingatia changamoto zilizoko kwenye miradi ninayotuhumiwa
kutoikamilisha kwa wakati…..hii ni uonevu kwangu ikiwa ni kwa maslahi ya
wachache wanaopenda ten percent.” Alisema
Akifafanua
juu ya tuhuma hizo, injinia huyo alisema kuwa kuhusiana na mradi wa
Water Sector Development Project-WSDP ulipatiwa kiasi cha sh milioni 20
ili kutekeleza ujenzi wa vyoo 6 lakini baadhi ya vifaa vilitumika
kujenga nyumba kadhaa za walimu wa kata ya Kizengi.
Alisema
licha ya mradi huo kutokamilika kwa wakati, tayari vyoo vitatu
vilishakamilika, huku choo kimoja kikijengwa na wananchi, hali hiyo ya
ujenzi wa nyumba za walimu na kutumika vifaa kadhaa kwenye ujenzi wa
nyumba za walimu ndizo sababu zilizopelekea kutokamilika mradi huo kwa
wakati na taarifa zake zipo.
Kuhusu
tuhuma za kushindwa kukamilika kwa mradi wa maji makao makuu ya wilaya
ya Uyui, Isikizya, alisema zipo sababu za msingi kwa mkandarasi
aliyepewa kazi hiyo, PET Company Ltd, alipewa miezi mitano katika kazi
yake ya uchimbaji wa mtaro lakini kutokana na mtaro huo kupita eneo la
mashamba ya tumbaku wananchi waliomba hadi mavuno yao yaishe na mradi
huo haukuwa na fedha za fidia.
Aliongeza
kuwa suala hilo ofisi ya mkurugenzi ilikuwa na taarifa ikiwemo taarifa
za mkandarasi kuomba siku 90 zaidi ili kukamilisha mradi huo, huku mradi
huo pia ukichelewa kutokana na eneo hilo pia kuwa na mwamba na hivyo
kazi hiyo kuwa ngumu na ya muda mrefu.
Kuhusu
tuhuma za kutakiwa kurejesha kiasi cha sh milioni 4,420,640 ndani ya
siku saba, ambazo zingejenga vyoo sita vya kata ya Msimba na Kizenge,
inamshangaza kwani fedha hizo zipo kwenye akaunti benki kwani kama fedha
hazikutumika ina maana zipo na hakuna wizi.
Alisema
tuhuma nyingine ni kuhusiana na ununuzi wa mashine ya maji ya Diesel
badala ya umeme, injinia Nicodemus alisema alifanya hivyo kutokana na
agizo la aliyekuwa waziri wa maji Profesa Mark Mwandosya, kipindi cha
mwaka 2010 alipofanya ziara kwani hakuwa na jinsi kutengua agizo la
waziri hasa kutokana na kipindi hicho makao makuu ya wilaya hayakuwa na
umeme.
Alisema
maamuzi ya ununuzi wa mashine hiyo pia yalipitia kwenye vikao vya
zabuni na taarifa zake zipo, huku suala la upotevu wa vifaa katika stoo
ya maji kama mkuu wa idara liliripotiwa kituo cha polisi na uchunguzi
unaendelea huku kampuni ya ulinzi ikijulishwa suala la mtumishi wao
kuhusika na upotevu wa vifaa hivyo.
Aliongeza kuwa alichukua hatua kama mkuu wa idara ambaye anamwakilisha mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi.
Alimalizia
kuwa kutokana na maamuzi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui
kuketi kwenye kikao cha baraza maalumu na kumvua madaraka, amewasiliana
na wanasheria wake kuangalia hatua za kuchukua ili haki zake kama
mwajiriwa zipatikane.
Mnamo
mwezi desemba 19 mwaka 2012 baraza la madiwani maalumu liliketi na
kuazimia kumvua madaraka injini Nestory Nicodemus kwa uzembe wa tuhuma
ainishwa.
No comments:
Post a Comment