Thursday, January 3, 2013

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA RASMI CHANJO YA MTOTO 2013

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akihutubia kwenye uzinduzi wa Chanzo

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akimwekea chanjo mmoja ya kati ya watoto walioshiriki kwenye Uzindu wa Chanjo kwa Mtoto 13 Mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akishiriki kwenye buradani ya msanii mchelemchele muda mfupi baada ya Kuzindua Chanjo kwa Mtoto 2013 Mkoani Mwanza Leo
---
Zoezi la Chanjo limefanyika kimkoa katika Wilaya ya Sengerema kwenye Tarafa ya Sengerema  kijiji cha Sima na Kata ya Sima Mkoani Mwanza.
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo amesema zoezi hilo kimkoa ni lazima lifanikiwe kwa mujibu wa malengo walio jiwekea ya 95% kwa kila wilaya kinyume chake wale wote watakaoshindwa kufikia lengo itabidi wajieleze na sababu zilizofanya washindwe kuvuka malengo katika Mkoa wake.

Ndikilo amesema yeye kama mtendaji Mkuu katika Mkoa wa wa Mwanza hayupo tayari kuona Mkoa huo unakuwa wa mwisho katika zoezi hilo.
Amewahimiza wazazi kujitokeza kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo hiyo kwani kuacha kuwachanja watoto, si hatari kwa mototo tu, bali pia watoto wenzake wanao mzunguka hivyo ni vema kila mzazi akaona umuhimu wakumpeleka watoto katika chanjo.

Mkuu huyo wa Mkoa amewahakikishia wananchi wa Sengerema na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla wake kuwa, chanjo hiyo ni salama kwakuwa imefanyiwa utafiti wakutosha na wataalam wa afya wa Ulimwenguni na  Wizara ya afya hapa nchini.

Akihututubia mamia ya wananchi wa kijiji hicho cha Sima,  Amesema watoto wa chini ya miaka 5 wanachangamoto nyingi, hasa kwenye nchi zetu hizi zinazo endelea , kwani kwingineko kwa nchi zilizo endelea watoto wanao zaliwa hukua kwa takriba ni 99% tofauti na hapa kwetu.

Amesema ugonjwa wa kichomi huua watoto kwa 14% ukitanguliwa na Malaria ambao huuwa kwa asilimia 15% huku ugonjwa wa kuharisha ukishika nafasi ya tatu kwa kuuwa watoto wengi kwa asilimia 12% kwani nchini Tanzania kila mwaka watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wapatao takriba ni 198,443 huugua ugonjwa wa kuharisha na kati yao 13,397 hufariki dunia.

Ujumbe mahususi wa siku hiyo ni Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye afya, ameongeza kuwa Chanjo hiyo ni sehemu ya Ilani, hivyo kufika 2015 jamii ya kitanzania iwe ni jamii iliyo na ustawi.

Magonjwa ambayo hadi hivi sasa yana chanjo ni donda koo, kichomi, kuharisha, pepopunda, kifua kikuu, surua, homa ya uti wa mgongo, kifaduro, homa ya ini, na polio, haya ndio magonjwa yaliopo katika mpango wa Taifa wa chanjo alisema na kuongweza.

Amehiza  viongozi wa kila  ngazi kuzindua kampeni hiyo, na watoto walengwa ambao ni kuanzia wiki 6 hadi wiki 32 wapatiwe chanjo hiyo bila kukosa.

Jumla ya watoto 149,000 wanategemewa kupatiwa chanjo hiyo na amesema zoezi hilo ni endelevu hadi tarehe 31. DEC. 2013.

Kaulimbiu ya katika maadhimisho hayo ni kuwa “Mtoto asiye chanjwa ni hatari kwake na kwawenzake, mpeleke mototo wako akachanjwe”

No comments:

Post a Comment