Saturday, January 12, 2013

RAIS JK - "KUNA HAJA YA KUUNDWA HALMASHAURI MBILI WILAYA YA UYUI"

 Rais Kikwete akifungua jiwe la msingi ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Tabora hadi Nyahua.
 Mkuu wa wilaya ya Uyui Bi.Lucy Mayenga akiwa jukwaani kwa lengo la kuwasalimia wananchi na kumkaribisha Rais Kikwete katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara.
 Baadhi ya Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui nao walitoa mpya baada ya kukosa viti vya kukalia katika mkutano wa hadhara wakaamua kukaa chini wakiwa na shauku ya kumsikiliza Rais Kikwete kwenye viwanja vya Chipukizi Tabora mjini.

Na Lucas Raphael,Tabora.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika  ziara yake ya kikazi mkoani Tabora amesema kuwa kuna haja ya kuundwa Halmashauri mbili katika wilaya ya Uyui ili kusogeza karibu huduma za maendeleo kwa wananchi.

Akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Uyui katika kata ya Ilolangulu alisema serikali yake itatekeleza ombi lao la kuwa na halmashauri mbili katika wilaya moja, huku akiahidi kuiagiza wizara ya ardhi na maendele ya makazi kupima ardhi ya vijiji hivyo ili waweze kupata hati ya kumiliki ardhi ili waweze kukopesheka katika taasisi za fedha.

Alisema hipo haja ya kuwa na halmashauri hizo mbili ilikuwaze kusongeza mahitaji muhimu kwa wananchi hasa ukizigatia hoja yaumbali mrefu kutioa ilolagulu hadi Isikizya .

Dkt kikwete alisema kwamba licha ya umbali huo lakini hipo haja kwa wananchi kuwa karibu na utawala wao ili kusuma maendeleo kwa wananchi na wapiga kura wa wilaya ya uyui na jimbo la Tabora Kaskazini.

Akizungumzi swala la ardhi Rais kikwete alisema kwamba hatamwangiza wazri husika kufika katika kijiji hicho ili kiweze kupimwa na hatimaye wananchi wa kata hiyo waweze kupata hati na kupata mikopo katika taasisi za fedha .


Awali Rais Kikwete alimtaka mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ilolangulu wilayani Uyui kueleza kero zinazowakabili wananchi wake ambapo mwenyekiti wa serikali ya kijiji, Ali Magowa, alimweleza kuwa wananchi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafiri umbali mrefu kufwata huduma za kiutawala, kuwa na ardhi ambayo haija piwa na kukosekana kwa maji safi na salama.

Hata hivyo alisema kwamba mradi wa milenia mbola bado unahitaji kuendelezwa na serikali ili kuwasaidia wananchi wa vijiji 16 mabvyo vipo chini ya maradi huo.

Alisema mradi wa viojiji vya milenia ni muhimu sana kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania kwani umesaidia kupunguza umaskini kwa idadi kubwa ya wajkazi wa vijiji hivyo .

Alisema kwamba haba baada ya mradi huo kulimza muda wake serikali itaendelea kuendeleza ili kuwa wasaidia wananchi kuendelea kupata mafanikio ya tanfa lao.

Akizungumzia huduma duni za maji waziri wa maji nchini Prof, Jumanne Maghembe, amesema vijiji hivyo vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika kipindi kifupi kijacho.

Alisema utafiti wa upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo ulifanywa na jaica ulisitishwa baada ya nchi ya Japan kukumbwa na tetemeko la tsunami ambapo kwa sasa serikali ya Japan ipo teari kuendelea na utekelezaji wa mradi huo.

Wilaya hii ya  uyui mkoani Tabora ambayo wananchi wake wanahitaji kusogezewa huduma za kijamii, kiutawala inatarafa 3, ambazo ni Ilolangulu, Igalula na Uyui, ina kata 24 na vijiji 120  ikikadiriwa kuwa na watu wapatao 372,761 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 .

No comments:

Post a Comment