Askari
Polisi wa kikosi cha FFU Tabora mjini wakijaribu kumdhibiti kijana mmoja
aliyefahamika kwa jina la Jonas Oscar(25)ambaye inadaiwa kuwa alitoroka
Gereza la mahabusu Tabora maarufu kwa Zuberi wakati akiwa anatumikia
kifungo cha mwaka mmoja.
Awali
Jonas Oscar imedaiwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja
akiwa ni mfungwa No.02,2013 katika Gereza la mahabusu Tabora mjini baada
ya kupatikana na hatia ya kutishia kumuua baba yake mdogo huko katika
wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Na mwandishi wetu maalumu
Mwananchi mmoja kwa kushirikiana
na askari wa kikosi cha kuzuia ghasia FFU mjini Tabora wamefanikiwa
kumkamata mfungwa mmoja wa gereza la mahabusu Tabora wakati akifanya
jaribio la kutoroka akiwa amevua nguo na kubakia uchi wa mnyama.
Mfungwa huyo ambaye anafahamika
kwa jina la Jonas Oscar(25)imedaiwa kuwa mnamo majira ya mchana siku ya
tarehe 14 januari 2013 alifanya jaribio hilo wakati akiwa kwenye kazi za
bustanini na wafungwa wenzake.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo lililokuwa kama mchezo wa kuigiza mfungwa huyo alilazimika kuvua
nguo zote(sare za kifungwa) ili isiwe rahisi kumkamata na kuanza
kutokomea mitaani.
Hata hivyo wakati akiwa ameanza
safari hiyo ya kukwepa kifungo cha mwaka mmoja ambacho ameanza
kukitumikia mapema mwaka huu,mfungwa huyo Jonas aliibukia katika kambi
ya Jeshi la Polisi iliyoko jirani na gereza hilo la mahabusu hatua
ambayo ilisababisha kuonwa mapema kwakuwa alionekana kuwa ni mtu wa
ajabu kwa kukimbia akiwa uchi wa mnyama.
"Nilipomuona niliamua kumkimbiza
na kutaka kujua anatatizo gani,nilimkamata na kuwaomba msaada FFU
waliokuwepo hapo jirani na Kituo chao"alisema mwananchi huyo ambaye
alijifahamisha kwa jina la Mapinduzi
Aidha katika hatua nyingine
mfungwa huyo amefikishwa mahakama ya wilaya ya Tabora,mbele ya hakimu
Mheshimiwa Magori na kukabiliwa kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi
halali kinyume cha sheria namba 16 kifungu cha 116 ya mwaka 2002,ambapo
alihukumiwa kutumikia adhabu kwenda jela kwa kifungo cha miezi 16,adhabu
ambayo ameanza kuitumikia mara moja.
No comments:
Post a Comment