Mwenyekiti
wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza
katika kikao cha kwanza cha kamati tendaji ya Chama hicho kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano Frankman Hotel mjini Tabora.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha
kamati tendaji wakitoa hoja na maoni mbalimbali katika kikao hicho
kilichofanyika Frankman Hotel.
Mwandishi maalum,Tabora
Wajumbe wa kikao cha kamati
tendaji ya Chama cha mpira wa miguu mkoani Tabora Tarefa leo wamejikuta
katika wakati mgumu na kulazimika kuendesha mkutano wao pasipo kuwa na
vifaa na nyaraka mbalimbali za chama hicho kufuatia viongozi waliomaliza
muda wao kutokabidhi vifaa hivyo tangu waachie madaraka mwishoni mwa
mwaka jana.
Mwenyekiti wa Tarefa Yusuph
Kitumbo pamoja na kuzungumzia mambo kadhaa kama hatua ya kwanza kwa
uongozi mpya tangu uchaguliwe,wakiwa katika kikao hicho cha kamati
tendaji alilazimika kupiga simu kwa aliyekuwa katibu wa Chama hicho
Albert Sitta kumtaka arejee barua aliyoandikiwa kukabidhi vifaa vya
ofisi, hatua ambayo itawezesha uongozi mpya kupata fursa ya kuanza
kutumikia Chama hicho kikamilifu.
Katika mahojiano ya simu Yusuph
Kitumbo walikubaliana na Katibu huyo wa zamani Albert Sitta kuwa
anataraji kukabidhi vifaa hivyo mnamo siku ya jumatatu tarehe 14 Januari
2013 saa nne na nusu asubuhi ingawa haijajulikana ni wapi makabidhiano
hayo yatafanyika.
Hata hivyo kikao hicho cha kamati
tendaji kiliendelea pasipokuwa na nyaraka mbalimbali za kumbukumbu za
Chama hicho na hivyo kufanya utaratibu wa kikao kuwa mgumu.
Pamoja na maadhimio kadhaa
yaliyofikiwa na Tarefa lakini Chama hicho kimeendelea kuwa na wakati
mgumu kwa madai kwamba uongozi uliopita umepoteza mvuto kwa baadhi ya
wadau wa soka pamoja na kutoaminiwa na Viongozi wa Serikali ya mkoa wa
Tabora.
Kitumbo aliwaeleza wajumbe wa
kamati hiyo kuwa bado kuna kazi mgumu ya kujaribu kurejesha heshima ya
uamini kwa Chama hicho ili kiweze kupata misaada kutoka kwa wadau wa
soka wa ndani na nje ya mkoa waliokuwa wamekisusia kwa muda mrefu.
"Jamani uongozi uliopita tayari
umekiathiri sana Chama chetu,na hii imetokana zaidi na migogoro ya mara
kwa mara ya viongozi jambo ambalo hata kwa sisi viongozi wapya
limetufikisha kupoteza mvuto kabisa kwa Serikali ya mkoa wetu"alisema
Kitumbo huku akiwatahadharisha wajumbe kuwa makini ikiwa ni pamoja na
kuepukana na tabia ya kuzungumzia mambo ya chama hicho nje ya vikao
visivyo rasmi.
Aidha uongozi mpya wa Tarefa
uliingia madarakani mnamo Desemba 22 mwaka jana baada ya kufanyika
uchaguzi mkuu wa Chama hicho.
No comments:
Post a Comment