Tuesday, January 22, 2013

TAREFA YAHITAJI MSAADA WA WADAU WA SOKA TABORA


Na Lucas Raphael,Tabora

CHAMA cha soka mkoa wa Tabora,(TAREFA),kimewataka wadau na wapenzi wa
mchezo huo,kuweka uzalendo mbele na kuunga mkono jitihada
zinaazofanyika kuhakikisha timu ziliopo daraja kwanza zinafanikiwa
kuingia ligi kuu.

Mwenyekiti wa chama hicho,Yusuph Kitumbo alisema hayo wakati akiongea
na waandishi wa habari akibainisha mikakati iliyopo chini ya uongozi
wake ikiwemo mikakati ya kurejesha Tabora inarejesha hadhi ya mchezo
wa soka kama kipindi cha timu ya Mirambo.

Kitumbo alifafanua kuwa hivi sasa kwa kushirikiana na viongozi
wenzake,wanaweka mipango mizuri ili kupandisha timu moja ambayo
itawakilisha mkoa kwenye ligi kuu na kurejesha makali ya kipindi cha
miaka ya 1994.

Aidha mwenyekiti huyo aliingeza kuwa hivi sasa kuna timu mbili za
Rhino Rangers,na Polisi,na kwamba wanaweka mikakati mikubwa
kuhakikisha timu hizo zinzcheza ligi kuu mwakani.

“Nawaomba wapenzi na wadau wa mchezo wa soka mkoani Tabora,yakiwemo
mashirika na taasisi za fedha kuungana katika kufaniukisha malengo ya
uongozi wa TAREFA ili hapo baadaye mkoa wetu unakuwa na timu zaidi ya
moja ligi kuu.”alisema.

Alisema haya yote hayatafanikiwa endapo kutakuwa hakuna uzalendo
kuanzia ngazi ya uongozi wa soka wenyewe,wapenzi na wadau katika
kuinua soka mkoani Tabora.

Kitumbo aliongeza kuwa chini ya uongozi wake wamejipanga vyema ikiwemo
kualika timu kadhaa kuja Tabora kucheza na timu za Polisi na Rhino
Rangers ili kujenga uwezo wa timu hizo.

Kuhusiana na mikakati ya kiuongozi mwenyekiti huyo alisema
watahakikisha wanawaunganisha wana Tabora katika michezo kadhaa
ikiwemo soka ya wanawake na kuweza kuweka timu ya wanawake inayocheza
soka la kisasa.

Kwa upande wake mwakilishi wa soka upande wa wanawake mkoa wa
Tabora,mwalimu Janeth Kabeho, alisema amejipanga vyema kuhakikisha
anawawakilisha vyema wanawake kwenye mchezo huo.

Mwalimu Kabeho alioingeza kuwa hivi sasa anajipanga kujenga timu imara
ya wanawake kila wilaya na baada ya hapo ni kutafuta timu ya mkoa
ambayo itawakilisha Tabora kwenye mashindano mbalimbali.

Aliongeza kuwa hivi sasa amepata mipira 10 ambayo itatumika kwa timu
za wilaya na kwamba baada ya hapo anatarajia kutafuta vifaa vya mchezo
huo kwa wafadhili baada ya timu za wilaya zitakapopatikana.

No comments:

Post a Comment