Tuesday, August 20, 2013
CHINA YATAKA KUWEKEZA KWENYE TUMBAKU YA TABORA,MAKAMPUNI YA WAZUNGU YAPATA HOFU KUBWA
![]() |
| Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing akiwa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa wakati alipotembelea Ghala la Tumbaku lililopo eneo la Cheyo manispaa ya Tabora. |
![]() |
| Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Youqing akizungumza na baadhi ya wataalam katika kikao kifupi ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora wakati alipofanya ziara yake mkoani Tabora. |
![]() |
| Mkuu wa mkoa Bi Fatma Mwassa akiwa na ugeni huo walipokuwa wakiangalia tumbaku iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kupelekwa katika viwanda vya Sigara. |

CHINA KUJENGA MJI WA KISASA TABORA,NEEMA YANUKIA,WAWEKEZAJI WENGI WAJA KUWEKEZA.
![]() |
| Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing akiwa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Tabora wakati wakipata maelezo ya eneo la kujenga Bandari ya nchi kavu huko Inala nje kidogo ya mji wa Tabora. |
Sunday, August 11, 2013
UAPISHO WA RAIS WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA, TPSC-TABORA
TANZANIA PUBLIC SERVICE COLLEGE {TPSC} KIMENDESHA ZOEZI ZIMA LA
KUUAPISHA UONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI AMBAPO MKURUGENZI WA CHUO
ALIWAAPISHA RAIS NA MAKAMU WAKE NA RAIS KULIAPISHA BARAZA LAKE
LITAKALOFANYA KAZI KWA MUHULA WA MWAKA 2013/14.
ZOEZI HILO LILIAMBATANISHWA NA UKARIBISHWAJI WA WANACHUO WAPYA KWA MWAKA
HUU WALIOANZA MASOMO YAO HIVI PUNDE KWA MICHEZO MBALIMBALI IKIWEMO
MPIRA WA KIKAPU, MPIRA WA MIGUU, VOLLEYBALL NA NETBALL.
RAIS AKISAINI KIAPO
MKURUGENZI WA CHUO AKISAINI KIAPO HICHO BAADA YA KUMUAPISHA RAIS.
MAKAMU WA RAIS AKIAPISHWA NA MKURUGENZI WA CHUO
MAKAMU AKISAINI KIAPO CHAKE CHA KUITUMIKIA SERIKALI YA CHUO HICHO KWA MWAKA 2013/14
RAIS AKILIAPISHA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI
PICHA YA PAMOJA YA UONGOZI WA CHUO NA MARAIS
RAIS NA MAKAMU WAKE
MKURUGENZI AKIWAHOTUBIA WANACHUO
RAIS WA CHUO AKIWAHOTUBIA WANACHUO PAMOJA NA KUTOA SHUKRANI ZAKE
BARAZA LA MAWAZIRI
PICHA YA PAMOJA KATI YA BARAZA LA MAWAZIRI NA UONGOZI WA CHUO
RAIS NA BARAZA LAKE
WANACHUO
WANACHUO WAKITEGA MASIKIO YAO KWA UMAKINI
WAKIJONGEA ENEO LA TUKIO KWA KIAPO
MWANAUME AFIA GESTI AKIFANYA MAPENZI NA MPENZI WAKE JIJINI DAR
MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi.
Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.
Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana.
Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.
JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA TUKIO LA KUPIGWA RISASI SHEIKH PONDA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani
ya Simu “
MKUUPOLISI” &
nbsp; Ofisi ya Inspekta Jenerali wa
Polisi,
Simu
: (022)
2110734 Makao
Makuu ya Polisi,
Fax
Na. (022)
2135556 S.L.P.
9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DAR ES SALAAM AGOSTI 10, 2013.
1. MNAMO
TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA
MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA
BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO.
DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA
ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.
2.
KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU
WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA
AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA
JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA
SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA
UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA
UVUNJIVU WA AMANI.
3.
BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO
KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA
RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.
4.
KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI
SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA
MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA
ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.
5.
KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI
JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU
IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.
6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
KATIBU WA JUMUIYA YA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA SHEIKH ISSA PONDA NI KWELI HAPO JANA ALIPIGWA
RISASI NA KWASASA YUPO HOSPITALI YA
RUFAA YA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI NA SI KWELI KAMA YUPO CHINI YA
ULINZI WA POLISI KAMA SMS MBALIMBALI
KUPITIA SIMU ZA VIGANJANI ZINAVYOSAMBAZWA.
PIA JUMUIYA NA TAASISI YA KIISLAMU
TANZANIA LEO IMETOA TAARIFA ZA TUKIO HILO NA HUKU IKILAANI VIKALI
KUPIGWA RISASI SHEIKH PONDA NA KWAMBA KAMA ALIKUWA NA HATIA KITENDO CHA
KUMPIGA RISASI SIO SULUHISHO BALI NI KUONGEZA CHUKI MIONGONI MWA
JAMII.(picha na S Magambo)
Subscribe to:
Posts (Atom)

















