Barabara ya Tabora - Itigi kwa kiwango cha Lami ambapo balozi Lu alitembelea.
NIONAVYO MIMI
Ama
kwa hakika Mungu si Athumani,amini usiamini kuna kila dalili kwa mkoa
wa Tabora kuwa sehemu inayovutia kwa utafutaji wa maisha.
Pamoja
na kuwa tulizoea kusema kuwa Tabora hakuna kitu,Tabora pakavu
sana,Tabora hakuna lolote,Tabora majungu tu,Tabora wachawi,Tabora mauaji
ya kupindukia na mambo kadha wa kadha ...Lakini hayo yote hivi
karibuni katika kipindi kifupi kijacho huenda yakabaki kuwa historia tu
ikiringanishwa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya mkoa wa Tabora
katika kutafuta wawekezaji.
Si
vibaya hata kuliona hilo kubwa lililofanywa na Rais Kikwete la kuweka
barabara za kiwango cha Lami ikiwa ni mkakati wa kuufungua mkoa wa
Tabora ambapo kwa wengine wamekuwa wakibeza jitihada hizo na kuletea
maneno mengi yasiyo na mashiko kila upande,Lakini hili sasa wenzetu wa
Serikali ya mkoa wa Tabora wakalitazama tofauti kidogo kwa maana ya
kuona mbali zaidi.
Wakafumbua
macho yao na kuona baada ya barabara za lami nini maandalizi yetu kama
mkoa,...bila kufanya ajizi wakaanza mpango mkubwa wa kutafuta wawekezaji
kila kona ili mradi tu kuona kama kweli mabadiliko yatakuwepo au la
kama walivyozoea wenyeji ambao wengi wao hawataki mabadiliko na kubaki
na msemo "eti Tabora ilishalaaniwa na waarabu haiwezi kupata
maendeleo"jambo ambalo ni fikra mfu kwa ulimwengu wa sasa wa Sayansi na
Teknolojia.
Hapa
nakubaliana na vichwa vilivyokaa na kutafakari namna ya kuwaondoa
wakazi wa Tabora pale walipo na kujaribu kuwafikisha eneo ambalo nao
wataona kuwa ni nafasi yao kipekee katika kuyaona maisha katika mwanga
bora,kumbe MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA INAWEZEKANA.
Hongereni sana Jamani kwa kuumiza vichwa hili lilikuwa gumu sana kulifikia hapa Tabora.
Wawekezaji
kutoka china imeelezwa kuwa tayari wamethibitisha wapo tayari kuwekeza
kwa kununua tumbaku ambayo katika kipindi hiki chote wakulima wamekuwa
wakinyonywa na makampuni ya wazungu ambayo yamekuwa yakinunua zao hilo
kwa kadri wanavyotaka wao tena naweza kusema kuwa kwa dhuruma kubwa
wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi ambao nao kwa
sehemu kubwa huchangia kuzidisha umasikini kwa wakulima wenzao.
Tukiachana
na zao la tumbaku ambalo ndilo zao kuu la biashara na linaloingiza pato
kubwa lisilo mnufaisha mkulima,fursa nyingi zilizotangazwa ambazo
zitaleta mabadiliko makubwa Tabora,Uwekezaji katika maeneo mbalimbali
ikiwemo ujenzi wa bandari ya nchi kavu,mji wa kisasa wa china,ujenzi wa
Stand mpya ya kisasa utakaotokana na kukamilika kwa barabara hizi za
kiwango cha Lami na ukizingatia Tabora kama vile ipo katikati
hivi!!...Kwa maana kila itakuwa vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa
kuendesha shughuli zao pasipo kuifikiria Tabora ambayo sasa itakuwa
kiunganishi kikubwa hata na nchi za Rwanda,Burundi,Uganda na pengine
hata Kongo pia.
Sasa
naomba nitoe tahadhari kwa wananchi wenzangu wa Tabora,...Jamani
msibweteke maana ninaloliona kwenu kwasasa ni kubaki walalamikaji pale
wenzetu kutoka mikoa jirani watakapo kuja na kuchangamkia fursa
mbalimbali hizi zinazoanza kunukia.....Jamani msije ,mkawalaumu viongozi
wa serikali kwani hata mbeleko waliyojaribu kutubebea hadi sasa
itakatika na matokeo yake tutadondoka chini na kuumia,...Lamsingi
tuchangamkie fursa hizi zinakuja.
Balozi
wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing ametembelea mkoa wetu wa Tabora
hii ina maanisha ni jitihada za Serikali ya mkoa ndio zimefikia hatua
hiyo na niwazi kwamba Balozi pia amefuatana na Jopo la viongozi wa Asasi
za Wawekezaji huko China ambapo wameonesha kuridhishwa na fursa
zilizopo Tabora na kukubali kuwekeza katika nyanja mbalimbali.
|
No comments:
Post a Comment