Tuesday, August 6, 2013

MAKADA WA CHADEMA WAFUTIWA KESI YA UGAIDI

Na Lucas Raphael,Tabora

 

MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Tabora jana  imefuta shitaka la ugaidi lilokuwa likiwakabili makada wa Chama cha demokrasia na mandeleo CHADEMA nakubakiza kesi moja ya kummwagia mtu tindi kali.

Akitoa uwamuzi huo Jaji mfawidhi wa Mahakama hiyo Simon Lukelerwa amesema kuwa ametoa maamuzi hayo kutokana na kutokidhi sababu za kisheria zilizotolewa na upande wa mashitaka.

Jaji huyo aliieleza mahakama hiyo kwamba kulingana na  kifungu (che) cha sheria ya mwenendo wa mashitaka ya mwaka 1985 kesi hiyo anaamuru ahamishiwe katika mahakama ya wilaya ya Igunga.

Aidha alisema kuwa sheria namba 245 kifungu kidogo  (1) kinasema nilazima washiatakiwa wanatakiwa katika mahakama ya sehemu ambayo wanadaiwa kutenda kosa husika.

Jaji Lukelerwa ameamuru washitakiwa wote wapelekwe wilayani Igunga kwa ajili ya kusikilizwa upya shauri lao na kwamba dhamana ipo wazi kwa washitakiwa iwapo watakuwa wamekidhi matakwa ya mahakama ya wilaya hiyo ya Igunga.

Hali ya ulinzi wa askari Polisi wakiwa na silaha nzito ilikuwa imeimarishwa mahakamani hapo wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa katika mahakama kuu kanda ya magharibi.

Kesi hiyo ya ugaidi ilifunguliwa mahakamani hapo mwezi juni 24 mwaka huu,baada ya washitakiwa hao kuachiwa awali wilayani Igunga,katika kesi ya madai ya kummwagia tindikali kada wa Chama cha mapinduzi CCM, Musa Tesha.

Watuhumiwa hao ni Evodius Justunian, (30) mkazi wa Bukoba,Osca Kaijage mkazi wa mkoa wa Shinyanga,Seif Magesa mkazi Nyasaka Mwanza,Rajabu Daniel mkazi wa Dodoma na Henry Kilewo.

Mapema mwezi julai 8 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Tabora,hakimu wa mahakama hiyo Issa Ibrahim Magori alisema hana mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo na kuihilisha kwa muda.

Wakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo Peter Kibatala amewambia waandishi wa habari kwamba,mahakama kuu imetenda haki na anaimani kubwa na mahakama hiyo.

Aidha alisema kwakuwa washitakiwa hao walikamatwa katika sehemu tofauti hivyo kesi zao zilipaswa kusikilizwa maeneo waliyokamatiwa.

Mwisho

No comments:

Post a Comment