Na Lucas Raphael,Nzega
ZAIDI ya Tembo 100 wilayani Nzega mkoani Tabora wamevamia kata ya
Mwakashanhala na kufanya uhalibifu mkubwa wa mazao mbalimbali ya vyakula vya
wananchi.
Hayo yalisemwa na Diwani wa Kata hiyo Julius Mshandete kuwa Tembo
hao zaidi ya 100 walivamia kata hiyo Julay 30 mwaka huu.
Alisema kuwa Tembo hao 100 wakitembea kwa makundi katika vijiji
mbalimbali vya kata hiyo hukuwakifanya uhalibifu mkubwa wa mazao ya wananchi
ikiwa na kubomoa nyumba zao kwa lengo la kutafuta chakula ambacho kimehifadhiwa
ndani.
Julius Mshandete alisema kuwa mazao wanayokula Tembo hao kuwa ni pamoja
na mahindi,Mihogo na Viazi vitamu ambavyo vimekaushwa.
Alisema licha ya kuharibu mazao na makazi ya wananchi Tembo hao
wamekuwa tishio kubwa kwa Raia hali ambayo maisha ya wananchi yapo hatarini kwa
muda wowote endapo Tembo hao wakicharuka.
Alisema Tembo hao imekuwa ni kawaida kila mwaka kufika katika kata
hiyo na kuhalibu mazao ya wananchi pamoja na nyumba ikiwa na kufanya mauaji kwa
muda wowote hali itakayo tokea.
Alisema kuwa serikali ichukue jukum la kudhibiti maliasili hao
ilikuweza kutoingilia makazi ya wananchi ikiwa na kuepusha uhalibifu huo pamoja
na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Diwani huyo aliiomba Idara ya maliasili wilayani hapa kuchukua
hatua za dharula kuwafukuza tembo hao iliwaweze kurejea katika hifadhi yao
husika ikiwa na kupisha shuguli za maendeleo za wananchi zikiendelea.
Aliwataka wananchi kuwa waangalifu na watulivu katika kipindi hiki
kigumu pamoja na kutolala ndani ya nyumba za kuhifadhia mazao ya vyakula.
Kwaupande wake Ofisa mali alisili wilaya Juma madata alisema kuwa
tayari kishaagiza kikosi kazi cha kuwafukuza Tembo hao ilikuepusha madhara
yanayo wezakujitokeza kwa nyakati kama hizi Tembo hao wapo katika eneo hilo.
Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu watatu mwaka jana waliuawa
na Tembo wilayani Nzega kutokana na Tembo hao kuvamia makazi ya wnanchi pamoja
na kuhalibu mazao.
No comments:
Post a Comment