NA LUCAS RAPHAEL NZEGA
MWENYEKITI wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa katiba haina dini,rangi
wala ukabila kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya wananchi ya kila siku.
Akiwahutubia wananchi
wa Nzega mjini katika viwanja vya parking jana alisema kuwa wananchi wanapaswa
kutoa maoni yao dhidi ya rasim ya katiba kabla ya Agust 30 mwaka huu.
Alisema chama hicho
kinapiga kampeni ya kuhamasisha waTanzania kuangalia mambo ya msingi katika
katiba hiyo ambayo yataleta tija kwa wananchi ilikatiba ijayo iwena masirahi
kwa wananchi wote.
Alisema kuwa endapo
wananchi wakipuuzia ushauri huo utawagharim kwa miaka kadhaa na kusababisha
hali mbaya ya maisha dhidi ya katiba itakayo pita.
Alisema kuwa mchakato
huo wa kukusanya maoni ya katiba hauna itikadi ya kisiasa,Dini,rangi wala
kabila bali ni masirahi ya wananchi wote hapa nchini ambapo wanapaswa kutoa
ushirikiano wa kutosha ilikuweza kupata katiba itakayo wasaidia katika maisha
yao.
Alisema kuwa
watanzania waliobahatika kutoa maoni ya katiba katika duru ya kwanza ni
wachache kuliko idadi iliyopo na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa watoe maoni
yao katika kupata katiba waitayo yenye masirahi ya msingi kwa kila mtanzaia.
Mwenyekiti huyo
aliipongeza Tume ya mabadiliko ya katiba inayongozwa na mwenyekiti wake Jaji
sinde warioba kuwa imetoa rasimu ya msingi yenye maoni ya watanzania na
kuongeza kuwa baadhi ya vyama vya siasa vinafanya utaratibu wa kuipinga rasim
hiyo baadhi ya vipengele.
Kwa upande wake
mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM
kinampango wa kupinga baadhi ya vipengele ikiwepo na mfumo wa serikali tatu.
Alisema kuwa maoni ya
wananchi yaheshimiwe kimsingi kutokana na rasimu hiyo ya katiba hivyo wananchi wanapaswa
kuendelea kutoa maoni yao dhidi ya rasimu hiyo ya katiba.
Lisu alisema kuwa
katika Bunge la katiba lijalilo litakuwa halitoshi kutokana na kuhakikisha haki
za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kutosha ili kila maoni ya msingi yawqeze
kupita.
Alisema kuwa
watahakikisha vipengele vyote vinasimamiwa kikamilifu kwa kuzingatia sheria na
utaratibu na kuongeza kuwa wananchi wazingatie mambo yao ya msingi waliyoyataka
katika maoni.
Shuguli za uzalishaji
mali nzega mjini ikiwepo kufungwa kwa maduka,soko zilisimama zaidi ya masaa
sita kutokana na wananchi kukusanyika kwa wingi kusubili msafara huo wa
mwenyekiti wa chama hicho pamoja na mnazimu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment