NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
WANANCHI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI MKOANI TABORA WAKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MSIMAMISI WA BANDA LA PSI KWENYE VIWANJA VYA NANENANE MKOANI HAPA JUU YA UZAZI WA MPANGO |
HATA WANAFUNZI HAWAKUWA MBALI KWA AJILI YA KUJIFUNZA MASWALA YA UZAZI WA MPANGO NA MAMBO MENGINE KWA AJILI YA MASOMA YA SANYASI |
Shirika la Psi mkoa wa Tabora limetoa hamasa kwa wananchi juu
ya umuhimu wa uzazi wa mpangona huduma hiyo utolewa bure kwa kina mama
wanaotaka huduma hiyo
Huduma hiyo imekuwa ikitolewa kwa kushirikiana na wizara ya
afya na ustawi wa jamii mkoani hapa katika zahanati zilizopo katika kata zaote
za mahispaa ya Tabora
Akizungumza na watu waliofika katika banda hilo la PSI afisa mhamasishaji
maswala ya uzazi wa mpango wa shirika mkoani
Tabora. Haika Msuya alisema kuwa shirika
hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na Idara ya afya mkoa katika kutoa huduma
hiyo kimkoa yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya nanenane mkoani hapa.
Alisema kwamba Katika kutoa huduma hiyo wanatembelea vituo vya
afya mbalimbali kwenye kata zote za mkoa
wa Tabora na kutoa huduma hiyo bure kwa
akina mama wanao taka kupanga uzazi.
Afisa huyo aliwashauri pia akina baba waliotembelea banda hilo
kwenye maonesho ya nanenane kukaa na wake zao na kupanga nao juu maswala ya
uzazi wa mpango maana itawasaidia katika kupanga mambo ya kimaendeleo.
Pamoja na mambo mengine katika maonesho hayo banda la shirika
hilo lilikuwa likitoa elimu ya ukimwi juu ya matumizi sahihi ya kondomu pamoja
na kutoa elimu juu ya maswala ya uzazi wa mpango.
Katika wiki hiyo ya maonesho ya nanenane shirika hilo la Psi
lilikuwa likitoa huduma hiyo bure ya kufunga uzazi kwa muda mrefu kwa njia ya
vitanzi na vipandikizi katika zahanati ya Isevya mkoani Tabora.
mwisho
No comments:
Post a Comment