NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora Sheikh Shaaban Salum akizungumza katika hadhara hiyo. |
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika hafla ya Futari hiyo. |
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya TABORA mjini, Moshi Abdulrahman-Nkonkota
amekemea vitendo vya ubaguzi wa dini, ukabila na rangi katika jamii kwani
vinahatarisha amani ya nchi.
Amesema
suala la ubaguzi wa dini, ukabila na rangi halifai na halitakiwa katika jamii
kwa lengo la kuimaisha usalama na amani ya wanajamii.
Moshi
alikuwa akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya TABORA mjini, Emmanuel Mwakasaka katika ukumbi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma, tawi la TABORA.
Kwa
upande wake, Sheikh wa mkoa wa TABORA, Sheikh Shaban Salum amempongeza ,Mwakasaka
kwa ushirikiano wake na kuwa karibu na jamii ya kiislamu.
Amesema
kitendo chake cha kuwaandalia futari waislamu, kinaoneyesha jinsi alivyo na
ushirikiano wa karibu na mshikamano na jamii ya waislamu.
Naye
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya TABORA mjini, Emmanuel Mwakasaka
amesema uamuzi wake wa kufuturisha waislamu unatokana na jinsi
anavyothamini jamii hiyo bila kujali tofauti za dini wala rangi.
No comments:
Post a Comment