Jenereta iliyotolewa msaada kwa Shule hiyo. |
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Tabora mjini Mwalimu Lucas Masanja akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo. |
NA LUCAS RAPHAEL TABORA
WANAFUZI wa shule ya
sekondari ya wasichana, (Tabora Girls), wameiomba Serikali ijenge uzio katika
shule hiyo ili kukomesha matukio
ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kila mara shuleni hapo.
Kilio hicho walikitoa jana muda mfupi baada ya kupokea msaada wa
vifaa vya masomo, vilivyotolewa na mdau wa elimu Emmanuel Mwakasaka, katika
hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Tabora.
Vifaa hivyo ni kompyuta tatu, Projekta moja na Jenereta moja,
vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8.4.
Katika Risara yao iliyosomwa na Edina Marisa, wanafunzi hao
walisema kuwa wanaiomba serikali na wadau hao wa elimu wenye mapenzi mema kwa
shule hiyo kujiokeza kutoa michango ya fedha ili ziweze kutumika kujenga uzio
huo kwa ajili ya usalama wa wananfunzi pamoja na mali za shule.
“Ndugu mgeni Rasmi shule yetu inakabiliwa na tatizo la kutokuwa na
uzio kwa muda mrefu sasa, hivyo tunakuomba wewe pamoja na wenzako mtusaidie
kujenga uzio, maana hapa tumekuwa tukivamiwa kila mara na wezi” ilisema sehemu
ya risara hiyo.
Wameeleza kwamba kutokana na kutokuwepo kwa uzio huo, imekuwa ni
rahisi kwa wezi na vibaka kuingia katika eneo la shule kufanya uhalifu na hivyo
kupelekea wanafuzi kuishi kwa hofu kubwa ya kuvamiwa na vibaka hao ambao
wamekuwa wakivamia shuleni hapo kila mara na kuwapora vitu kadhaa na kuwafanyia
vitendo vya udharirishaji wa kijinsia.
Mbali na hayo pia wamesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mabweni ya kulala, ukosefu wa vifaa
vya kujifunzia, uchakavu wa madarasa na kuwepo mazingira hatarishi.
Kwa upende wake Mwalasaka ambaye pia mjumbe Halamshauri kuu ya CCM
mkoani tabora, alisema
kuwa ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na hali haluisi ya changamoto
zinazoikabili shule hiyo yenye historia kubwa hapa nchini pamoja na wanafuzi
wake.
“Kutoa nimoyo siyo utajili mimi nimeamua kusaidia hivi vitu kwa
mapenzi yangu mwenyewe, sikuombwa na mtu wala kushawishiwa” alisema Mwakasaka.
Mwakasaka ametoa wito kwa wadau wengine wa elimu kujitokeza kutoa
misaada mbalimbali kwenye shule hiyo, huku Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora
mjini Moshi Nkonkota akiwataka viongozi waliosoma katika shule hiyo nao
wachangie fedha ili ziweze kutatua changamoto hizo.
Aliwataka mawaziri, mabalozi, makatibu wakuu wa wizara, na wabunge
waliosoma shuleni hapo kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa shule
inatatua matatizo yake.
Nkonkota alisema kuwa niabu kubwa kuona shule hiyo yenye historia
ya kusoma viongozi wa serikali nchini, kukosa uzio wakati wao wangari wapo na
wanauwezo mkubwa wa kunya hivyo.
Shule ya maalum ya sekondari ya wasichana Tabora (Tabora Girls)
ilianzishwa mnamo mwaka 1928.
Mwisho
No comments:
Post a Comment