Taarifa hii ni kwa hisani ya Gospel Kitaa...
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Jim ambaye ni Mkristo Mkatoliki pamoja na mkewe, amesema licha ya filamu
hiyo kuuza zaidi ya nakala milioni 400 lakini mambo si shwari kwake
kwakuwa hapewi tena nafasi ya kuigiza lakini amesema alishapewa onyo na
muongozaji wa filamu hiyo Mel Gibson ambaye alimwambia uamuzi wake wa
kutaka kuigiza nafasi ya Yesu katika filamu hiyo utamfanya kutoigiza
tena katika Hollywood na kufikia tamati ya uigizaji wake,muigizaji huyo
alimjibu akisema kila mmoja atabeba msalaba wake, kwasababu anakiamini
kile anachotaka kukifanya hivyo kila mmoja abebe msalaba wake lasivyo
uzito wake utatudondokea wenyewe tusipoibeba kwahiyo achana na hayo
twende tufanye kazi.
Aidha mwigizaji huyo amekiri kuwa alijua fika kwamba kuigiza nafasi ya
Yesu katika filamu hiyo ilikuwa ni kuiweka uigizaji wake matatani lakini
hakujali hilo na kuamua kuigiza huku muongozaji wake bwana Gibson
amewahi kushutumiwa na watu mbalimbali kuhusu mwenendo wake ikiwemo
suala la ulevi jambo ambalo Jim amesema watu waache kuhukumu kama
wameona Gibson ni mtenda dhambi jambo wanalotakiwa kufanya ni kumuombea
ili aache nasio kumuhukumu. Ameongeza kwamba imani yake ndio muongozo
wake binafsi na katika utaalamu wake katika uigizaji.
Jim akipata maelezo kutoka kwa Mel Gibson wakati wakirekodi filamu hiyo. |
KWA TAARIFA YAKO tangu kutoka kwa filamu hiyo mwaka 2004 hadi leo
hii mwigizaji huyo ameigiza katika tamthilia na filamu nyingine ambazo
hata hivyo kwa mtazamo wmingine ni kwamba labda angepata kazi nyingi
zaidi. Lakini hata hivyo mwigizaji huyo ametoa kazi yake mwenyewe ya
sauti hivi karibuni aliyoipa jina "Words of Promise" Ikiwa ni biblia
waliyoweka kwa njia ya sauti akiwashirikisha waigizaji wenzake. Hata
hivyo licha ya mambo ya uigizaji Hollywood kutokuwa kama alivyotegemea
lakini kwasasa anaonekana kukaza msuli zaidi katika utumishi wa kidini
kwakuzungumza kwenye makongamano na mambo mengineyo... Kwahiyo
hakijaharibika kitu
No comments:
Post a Comment