Na Lucas Raphael,Tabora
TAASISI ya kuzuia na
kupambana na rushwa,(TAKUKURU),mkoani Tabora imemkamata na kumfikisha
mahakamani hakimu mkazi wa mahakama ya
wilaya ya Urambo,Oscar Bulugu kwa tuhuma tatu za kuomba na kupokea rushwa
ya shilingi milioni tano.
Mbele ya hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya mkoa Issa Magoli ilidaiwa na mwanasheria wa Takukuru
Simon Mashingia kuwa mtuhumia alitenda makosa hayo kati ya tarehe 15 marchi na
22 mwaka huu huko wilayani Urambo.
Upande wa mashitaka
ulidai kuwa march 15 mwaka huu mtuhumia akiwa ni hakimu wa mahakama ya wilaya
ya Urambo alimshawishi Lucas Raymond Changala ampe fedha hizo ili aweze kumpa
dhamana ndugu yake aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya wizi wa fedha za benki ya
NMB.
Mashingia alidai katika
shitaka la pili kuwa tarehe 18/03/2013 hakimu huyo ambaye ni mtuhumiwa alipokea
shilingi milioni moja toka kwa Changala
kama malipo ya awali ili aweze kumpa dhamana Phillipo Raymond aliyekuwa mtumishi
wa benki ya nmb anayetuhumiwa kuiba zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Mwanasheria huyo wa
Takukuru alidai katika shitaka la tatu kuwa tarehe 21/03/2013 mtuhumiwa
huyo alipokea tena shilingi milioni moja ikiwa ni endelezo la malipo aliyoomba
aweze kumpa dhamana mtumishi huyo wa nmb.
Hakimu huyo baada ya
kusomewa mashitaka hayo matatu yote alikana na yuko nje kwa dhamana na kesi
hiyo imepangwa kutajwa tena 14/05/2013.
Cha kushangaza mahakama
ilimwamuru mtuhumiwa huyo kujidhamini mwenyewe kitendo ambacho kiliwashangaza
watu waliokuwepo mahakamani hapo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment