Na Lucas Raphael ,Siginda
SERIKALI imewataka viongozi wa kada mbalimbali
pamoja na wananchi kuwa na nidhamu na uwajibikaji mahali pakazi ili iwesehemu
kubwa ya mabadiliko ya kimaendeleo ya kiuchumi na sayansi na Teknolojia hapa
nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu Ubinafisishaji na uwekezaji Dkt,Merry Nagu wakati akifunga mkutano wa
kuhamasisha matumizi ya sayansi na Tekinolojia kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi
kanda ya kati singida.
Alisema Serikali imelenga kukuza uchumi kwa
wafanya Biashara wakubwa na wadogo kupitia sayansi na Tekinolojia ikiwa na
kuzingatia nidhamu na uwajibikaji mahali pakazi.
Alisema kuwa baadhi ya viongozi hawatambui wajibu
wao kwa kukosa ni dhamu na uwajibikaji mahali pakzi badala yake husababisha
miradi mingi ya kimaendeleo kudorola.
Alesema viongozi wanapaswa kujitambua na kujua
uwepo wao katika nafasi husika ili waweze kutekeleza kero za wananchi ikiwa na
kuleta maendeleo dhabiti kwa maeneo husika.
Alisema kuwa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC)
linahakikisha mikutano hiyo inaendelea kupitia makundi mbalimbali ikiwepo na
ngazi za mikoa,wilaya na kata lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi watumie
sayansi na tekinolojia katika kukuza uchumi wa ndani nje.
Waziri Nagu alisema kuwa yote hayo yanatokana na
nidhamu kwa viongozi,wadau pamoja na uwajibikaji mahali pakazi ilikuweza
kufikia malengo hayo.
Alisema Baraza la Biashara Tanzani TNBC limeweka
malengo kuwa ifikapo mwaka 2025 litafikia malengo hayo ya kukuza uchumi kwa
watanzania hususani wajasilia mali wa dogo na wa kubwa na kuondokana na
umasikini.
Alisema Baraza hilo limeweka vipaumbele vitavyo
changia kukuza uchumi huku vikiendelea kufanyiwa malekesho ilikufikia malengo
hayo ni pamoja na upatikanaji wa maji safi,Kilimo na mifugo,miundombinu ambayo
ni Barabara,Reli na Bandari lengo likiwa ni kuimalisha miundombinu hiyo.
Vipaumbele vingine ni pamoja na kuimalisha
nisharti na madini ilikuweza kukuza uzalishaji,ukusanyaji madhubuti wa mapato
ya ndani na je pamoja na kutoa elimu mbadala kwa wananchi dhidi ya miradi
husika.
Kwaupande wake kamishina msaidizi,mwandamizi
wa polis makao makuu Dar es salaam Lucas Kusima akiwasilisha maada ya umuhimu
wa usalama wa watu na mali zao katika mageuzi ya kiuchumi ya sayansi na
tekinolojia kwa jamii.
Alisema kuwa jeshi hilo limejipanga kukabiliana na
majambazi yanayotumia Tekinolojia hiyo ikiwepo na huduma ya kibenki A T
M,Simu za kiganjani,mitandao ya kijamii pamoja na mitandao mingne.
Kusima amewataka wananchi kutoa ushirikia wa
kutosha kwa wahalifu hao kupitia Teknolojia za mawasiliano ilikuweza kukuza
uchumi huo na kuimalisha ulinzi na usalama kwa mali za wananchi ikiwa na
wananchi kwa ujumla.
Mkutano huo wa kuhamasisha matumizi ya sayansi na
tekinolojia kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi umeyakutanisha makundi mbalimbali
wakiwepo wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na mikoa pamoja
na wakuu wa mikoa kwa mikoa mitatu ikiwa ni Singida,Tabora na Dodoma.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment