Wednesday, May 8, 2013

CCM YA TUPILIA MBALI ZIARA ZA MADIWAN ZA MILL,82.3





 NA LUCAS RAPHAEL NZEGA



 

CHAMA cha mapinduzi ccm wilayani nzega mkoani Tabora kimetupilia mbali ziara iliyopangwa kufanywa na Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya, iliyokadiliwa kutumia kias cha Mill,82.3 katika mikoa ya Arusha,Singida,Dodoma pamoja Moshi kwa muda wa siku kumi na nne(14) kwa malengo ya kujifunza mambo malimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mwenyekiti wa chama hicho wilaya Amosi Majire kanuda alisema kuwa kamati ya siasa wilaya ilikutana na kutoa uamzi huo kutokana na kuona wilaya inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

Alisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Resolute ulilipa halmashauri hiyo kias cha shilingi Bill 2.4 kama malipo ya ushuru wa huduma wa madeni nyuma,fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya amana hadi April 15 zilipo toa faida ya shilingi Mill 82.3

Alisema kwa kiwango hicho kilichotengwa kufanyia ziara kwa madiwani hao kimebadilishwa badala yake fedha hizo zielekezwe katika mambo ya maendeleo mengine yenye tija kwa wananchi.

Alisema Baraza hilo lilipanga kufungua Benki ya kijamii itakayo weza kukopesha wananchi lengo likiwa ni kuinua uchumi na kukuza wajasilia mali,kamati hiyo imetengua uanzishwaji wa benk hiyo badala yake fedha hizo kila kata itapatiwa kias cha shilingi Mill,50 hadi 61 iliwananchi waweze kufanya mambo ya maendeleo.

Kanuda alifafanua sababu za kuzuia benk hiyo ni kutokana na kuwepo kwa Taasisi mbalimbali za kibenk wilaya hapa hivyo wananchi wanafursa ya kukopo na kujiendeleza kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla.

‘’madiwani wanapaswa kuiangalia jamii kwanza inataka nini sio kujiangalia wao kwani ziara hiyo inatija lakini wananchi kwanza kunakero mbalimbali zipo hapa tumeamua fedha hizo wazigawe kwa kila kata na wananchi watasema wanataka nini kwani fedha hizo ni zawananchi’’alisema mwenyekiti huyo.

Alisema chama cha mapinduzi kina madiwani wengi kimeshauri mambo hayo ya msingi kwa kujali masirahi ya wananchi na kuongeza kuwa ziara za madiwani ni kwa mujibu wa kisheria hivyo ziara zao watakwenda ilikuweza kuleta maendeleo.

Alisema kabla ya kuanza ziara hiyo madiwani hao watapaswa kuwaeleza wananchi madhumuni ya ziara yao na kuwahakikishia mafanikio ya zaira hizo ili kuweza kushirikisha wananchi katika maamuzi thabiti tofauti na hili lilivyo kuwa limejitokeza pamoja na matumizi makubwa ya fedha huku wananchi wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kero.

Aliwataka wabunge na madiwani wote kwa ujumla kuwa Baraza la madiwani la halimashauri hiyo lijalo kubadilisha Bajeti ndogo ya fedha za ushuru wa Huduma shilingi Bill 2.4 zielekezwe kwenye mipango ya maendeleo itakayo gusa wananchi.

Hata hivyo mwenyekiti  huyo wa chama cha mapinduzi wilaya ya nzega alivitaka vyama vya upinzani kutowaposha wananchi juu ya fesha hizo bali kuwaeleza kweli wananchi hao matumizi sahihi juu ya fedha hizo kwani fedha hizo zilitowalewakwa ajili ya matumizi ya wananchi wa wilaya ya nzega.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi alipoulizwa suala hilo alisema kuwa serikali imechukua hatua za awari za kusimamisha ziara hiyo hadi pale uchunguzi na matumizi thabiti yatakapo patikana ya fedha hizo.

Alisema kuwa wilaya ya Nzega inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa na uhaba wa madawa,madawati pamoja na zaidi ya nyumba 354 za wananchi kudondoka kutokana na mafuriko yaliyotokea mwezi March na April.

 Baraza la madiwani la halmashauri hiyo lililofanyika kati ya April 24 na 25 mwaka huu lilipitisha mchanganuo wa bajeti ndogo ya fedha za ushuru wa huduma zilizo lipwa na mgodi wa dhahabu wa resolute Bill,2.4 huku ziara ya madiwani na wabunge wawili kutumia Mill,82.3, Mill,300.7 kulipa madeni ya halmashauri pamoja na Bill,2 uanzishwaji wa Benk ya kijamii,aidha Fedha hizo zitaendelea kuwekwa kwenye akaunti ya amana hadi mchakato utakapo kamilika.

Mwisho.
 


No comments:

Post a Comment