NA LUCAS RAPHAEL,URAMBO
Wakazi wa wilaya za Urambo na Kaliua watakumbwa na baa la njaa iwapo
serikali na wananchi wenyewe hawata siamamia ipasavyo utunzaji wa
chakula walichovuna kutokana na mvua kuharibu vibaya asilima 35 za
hekta ya zao la mahindi yaliyolimwa msimu huu.
Akijibu hoja za madiwani kuhusu hali ya chakula katika wilaya hizo
afisa kilimo Erasto Konga alisema kuwa uzalishaji wa mazao ya
chakula msimu huu hasa mahindi siyo mzuri kutokana na kuharibiwa na
ukame kutokana na kutonyesha mvua wakati wa mwezi wa pili na
watatu.
Konga amebainisha kuwa makadirio ya chakula kwa wakazi 564,895 wa
wilaya hizo mbili ni tani 195,776 hivyo akatoa wito kwa madiwani
hao kuwaelekeza wananchi kununua chakula hasa mahindi kutoka
maeneo mengine hapa nchini.
Aliongeza kuwa zaidi ya tani 90,000 za chakula kinachozalishwa na
wakulima wa wilaya hizo ni cha wanga huku wananchi wakipendelea
kutumia kwa wingi mahindi kama chakula japo wananalima mpunga
ambao ufanywa kama zao la biashara.
Afisa kilimo huyo ameliambia gazeti hili kuwa kiashiria moja wapo
ambacho kinaonyesha kuwepo kwa tatizo la njaa ni kutokana na
kutoshuka kwa bei ya mahindi hadi sasa kwani debe la mahindi
kung’ang’ania shilingi 9000/= badala ya thsh 3500/= au 4000/= wakati
wa msimu wa mavuno hali ambayo inaonyesha kwamba mahindi hayapo.
Konga ameongeza kwamba bado wimbi la walanguzi linatishia hali ya
chakula katika wilaya hizi mbili kwani pamoja na serikali kuwahimiza
wananchi wasiuze chakula lakini wengi wao ulazimika kufanya hivyo kwa
ajili ya kujipatia mahitaji.
Amesema kuwa uzalishaji wa zao la muogo pia utapungua msimu huu
kutokana na zao hilo kukumbwa na ugonjwa wa BATO BATO KALI hivyo
kuongeza .
Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2012 / 2013 zilipangwa kulimwa hekta
135, 704 za mazao ya chakula ambazo zilitarajia kuzalisha tani 325,465
ambapo hekta za mazao ya chakula zilizolimwa ni 131, 785 sawa na asilimia
97 ya lengo.
Naye mkuu wa wilaya hiyo Anna Magowa aliwataka watendaji kutafuta ni
jinsi gani watakabiliana na tatizo hilo la upungufu wa chakula hasa mahindi
ambao umekuwa ukiikumba wilaya hiyo mara kwa mara.
Aliongeza kuwa watafute uwezekano wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji
hasa utumiaji wa matone kwani ndio hatumii maji mengi kwenye mazao ya
mahindi kutokana na tatizo la upungufu wa mvua.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment