Na
Lucas Raphael,Tabora
Mahakama
ya rufaa nchini imetengua maamuzi ya mahakama kuu na kumrudishia ubunge wake
Dkt Peter Dalali Kafumu – CCM wa jimbo la Igunga baada ya kuridhika ha hoja za
upande wa mrufani kuwa jaji aliyesikiliza shauri hilo hakuzingatia matakwa ya
kisheria.
Akisoma uamunzi huo mwenyekiti wa jopo la majaji wa mahakama hiyo jaji
Nathalia Kimaro akisaidiana na jaji William Mandia na jaji Semistrocles Kaijage
amesema kuwa mlalamikiwa hakulipa ada ya mahakama kama sheria ya uchaguzi
inavyoelekeza.
Aliongeza kuwa awali wakati shauri hilo namba 10/2011 linafunguliwa
mahakama kuu jaji aliyelisikiliza hakusikiliza pingamizi la mrufani kwamba
hakukuwa na ada iliyolipwa hivyo hakupaswa kuendelea na usikilzwaji wake.
“ kutolipwa ada ama kutokuwepo kwa kumbukumbu yoyote katika jalada la mahakama
inayoonyesha kitu kiwekwa kama kinga ilikuwa ni sababu tosha ya kutosikiliza
shauri hilo” walisema majaji hao katika maamuzi yao.
Katika hoja zake wakili wa serikali Gabriel Malata za kutaka
yatenguliwe maamuzi ya mahakama kuu aliwaambia majaji wa mahakama ya
rufaa kuwa jaji aliyesikiliza kesi hiyo alikosea kuanza kuisikiliza kwani
mlalamikaji hakutimiza matakwa ya kisheria.
Malata alidai kuwa mlalamikaji hakulipa ada ya mahakama kiasi cha shilingi
milioni moja alizotakiwa kutoa au hati ya nyumba kabla kesi hiyo haijaanza
kusikilizwa kama sheria ya uchaguzi kifungu na 111 inavyoelekeza.
Wakili Malata aliongeza kuwa kwa vile mjibu Rufaa Joseph Kashindye na
wenzake hakutekeleza sharti hilo usikilizwaji wa shauri hilo pamoja na
mwenendo mzima yakiwemo maamuzi vyote vilikuwa ni batili.
Aliongeza kuwa malalamiko yaliyopelekwa mahakama ni ya kutengeneza kwani hayajawahi
kuwasilishwa katika kamati ya maadili ya uchaguzi kama walivyofanya juu ya
suala la mbunge wa Tabora mjini Ismali Aden Rage ambaye alitozwa faini ya
shilingi laki moja kwa kutembea na
silaha kwenye mkutano.
Hoja hizo na nyingine zilipingwa na wakili wa mjibu rufaa profesa Abdalah
Safari ambaye aliitaka mahakama ya rufaa kuzitupilia mbali na kwamba Mahakama
iliyosikiliza kesi hiyo iliridhika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati
wa zoezi zima la uchaguzi wa jimbo la Igunga ndipo katengua matokea.
Kukatwa rufaa hiyo kunafuatia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotengua
matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani hapa baada ya kubainika
kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho
dhidi ya wapiga kura.
Jaji Mary Nsimbo Shangali wa mahakama kuu Agasti 21 mwaka jana alitangaza
kutengua matokeo hayo baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba
zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji kati ya hoja 19
zilizowasilishwa katika mahakama hiyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) Joseph kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili
Maarufu nchini Profesa Abdallah Safari ambapo alipinga matokeo ya
uchaguzi huo akilalamikia kukiukwa kwa sheria ya uchaguzi mkuu.
Upande wa Utetezi uliwakilishwa na mawakili Mohamed Salum Malik na
Gabriel Malata kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali,Msimamizi wa
Uchaguzi jimbo la Igunga, na mawakili Antony Kanyama na Kamaliza Kayaga
waliokuwa wakimtetea mbunge wa Igunga Dkt Peter Dalali Kafumu.
Akisoma hukumu jaji Shangali alizitaja baadhi ya kasoro zilizopelekea
kutengeliwa kwa uchaguzi huo ni pamoja na Ahadi iliyotolewa na
Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu ujenzi wa daraja la
Mbutu ambalo alidai kwamba kama wananchi hawataichagua CCM daraja hilo
halitajengwa, wakati ambapo katika kipindi hicho kulikuwa na shida kubwa ya
usafiri katika eneo hilo.
Alisema Kitendo pia kilichofanywa na mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage,
hakikuwa cha uungwana kwani alitumia lugha ya uongo kwa lengo la kupotosha
wapiga kura ambapo alidai mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (
Chadema) amejitoa katika uchaguzi huo.
akizungumza na gazeti hili mara baada ya maamuzi hayo nje ya mahakama aliyekuwa
mjibu rufaa Joseph Kashndye amekubali na kuridhika na maamuzi
hayo huku akiwalalamikia mawakili wake kwamba hawakumwelekeza kufanya
hivyo.
“ Sikujua, sikuelezwa hili ni tatizo la kiufundi hivyo silaumu”
alisema Kashindye.
Umati wa wananchama wa chadema ambao ulijaa ndani ya chumba cha mahakama
kwakweli uliondoka kwa uzuni eneo hilo la mahakama wakikibali matokeo huku
wengine wakisema tukajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao
Hata
hivyo Dkt kafumu akuwepo mahakamani alipotafutwa kwa njia ya simu alisema
kwamba hukumu iliyotewa na mahakama ya Rufaa ndio haki kamili kwani mwanzo
alikuwa na wasiswasi na jaji yule lakini alionekana anaongopa kuangushwa .
Alisema
kwamba amerejeshwa ubunge wake kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Igunga bila
kujali Itikadi ya chama chochiote cha siasa kwani waliompa kura na kumyima kura
wote ni wananchi wa Igunga.
Dkt
Kafumu alisema kwamba yale ambayo alikuwa hameyaanzisha ndio anataka kuendeleza
kwa nguvu zake zote kwa ajili ya maendeleo ya Igunga na wananchi wake kwa
ujumla.
“mimi
nijembe kama nilivyokuwa nasema wakati wa kampeni zangu kwamba mimi ni kwa
ajili ya wananchi wa Igunga hasa vijana na wale wa vyama Rafiki na ccm “alisema
Dkt Kafumu.
Aidha
mwenyekiti wa ccm wilaya ya Igunga Costa Olomi alisema kwa ushindi wa kafumu ni
wananchi wote wa Igunga sio wa chama bali ni kwajii ya maendeleo ya Igunga na
mkoa wa Tabora .
Alisema
kwamba baaada ya kurejeshwa umbunge wake chama cha mapinduzi kimepanga mapokezi
makubwa ya kupokea mbunge huyo hapa mei 12 mwaka huu kwa ajili ya sherehe ya
kupongeza .
MWISHO.
Akisoma uamunzi huo mwenyekiti wa jopo la majaji wa mahakama hiyo jaji Nathalia Kimaro akisaidiana na jaji William Mandia na jaji Semistrocles Kaijage amesema kuwa mlalamikiwa hakulipa ada ya mahakama kama sheria ya uchaguzi inavyoelekeza.
Aliongeza kuwa awali wakati shauri hilo namba 10/2011 linafunguliwa mahakama kuu jaji aliyelisikiliza hakusikiliza pingamizi la mrufani kwamba hakukuwa na ada iliyolipwa hivyo hakupaswa kuendelea na usikilzwaji wake.
“ kutolipwa ada ama kutokuwepo kwa kumbukumbu yoyote katika jalada la mahakama inayoonyesha kitu kiwekwa kama kinga ilikuwa ni sababu tosha ya kutosikiliza shauri hilo” walisema majaji hao katika maamuzi yao.
Katika hoja zake wakili wa serikali Gabriel Malata za kutaka yatenguliwe maamuzi ya mahakama kuu aliwaambia majaji wa mahakama ya rufaa kuwa jaji aliyesikiliza kesi hiyo alikosea kuanza kuisikiliza kwani mlalamikaji hakutimiza matakwa ya kisheria.
Malata alidai kuwa mlalamikaji hakulipa ada ya mahakama kiasi cha shilingi milioni moja alizotakiwa kutoa au hati ya nyumba kabla kesi hiyo haijaanza kusikilizwa kama sheria ya uchaguzi kifungu na 111 inavyoelekeza.
Wakili Malata aliongeza kuwa kwa vile mjibu Rufaa Joseph Kashindye na wenzake hakutekeleza sharti hilo usikilizwaji wa shauri hilo pamoja na mwenendo mzima yakiwemo maamuzi vyote vilikuwa ni batili.
Aliongeza kuwa malalamiko yaliyopelekwa mahakama ni ya kutengeneza kwani hayajawahi kuwasilishwa katika kamati ya maadili ya uchaguzi kama walivyofanya juu ya suala la mbunge wa Tabora mjini Ismali Aden Rage ambaye alitozwa faini ya shilingi laki moja kwa kutembea na
silaha kwenye mkutano.
Hoja hizo na nyingine zilipingwa na wakili wa mjibu rufaa profesa Abdalah Safari ambaye aliitaka mahakama ya rufaa kuzitupilia mbali na kwamba Mahakama iliyosikiliza kesi hiyo iliridhika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa jimbo la Igunga ndipo katengua matokea.
Kukatwa rufaa hiyo kunafuatia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani hapa baada ya kubainika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura.
Jaji Mary Nsimbo Shangali wa mahakama kuu Agasti 21 mwaka jana alitangaza kutengua matokeo hayo baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji kati ya hoja 19 zilizowasilishwa katika mahakama hiyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joseph kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili Maarufu nchini Profesa Abdallah Safari ambapo alipinga matokeo ya uchaguzi huo akilalamikia kukiukwa kwa sheria ya uchaguzi mkuu.
Upande wa Utetezi uliwakilishwa na mawakili Mohamed Salum Malik na Gabriel Malata kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali,Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga, na mawakili Antony Kanyama na Kamaliza Kayaga waliokuwa wakimtetea mbunge wa Igunga Dkt Peter Dalali Kafumu.
Akisoma hukumu jaji Shangali alizitaja baadhi ya kasoro zilizopelekea kutengeliwa kwa uchaguzi huo ni pamoja na Ahadi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo alidai kwamba kama wananchi hawataichagua CCM daraja hilo halitajengwa, wakati ambapo katika kipindi hicho kulikuwa na shida kubwa ya usafiri katika eneo hilo.
Alisema Kitendo pia kilichofanywa na mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage, hakikuwa cha uungwana kwani alitumia lugha ya uongo kwa lengo la kupotosha wapiga kura ambapo alidai mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) amejitoa katika uchaguzi huo.
akizungumza na gazeti hili mara baada ya maamuzi hayo nje ya mahakama aliyekuwa mjibu rufaa Joseph Kashndye amekubali na kuridhika na maamuzi hayo huku akiwalalamikia mawakili wake kwamba hawakumwelekeza kufanya hivyo.
“ Sikujua, sikuelezwa hili ni tatizo la kiufundi hivyo silaumu” alisema Kashindye.
Umati wa wananchama wa chadema ambao ulijaa ndani ya chumba cha mahakama kwakweli uliondoka kwa uzuni eneo hilo la mahakama wakikibali matokeo huku wengine wakisema tukajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao
MWISHO.
No comments:
Post a Comment