NA LUCAS RAPHAEL,NZEGA
VIONGOZI WA Dini mbalimbali hapa nchini
wametakiwa kujiendeleza kiEleimu wasilizike na Elimu waliyo
nayo kutokana na mabadiliko ya kisayansi na Teknolojia nayo jitokeza hivi sasa
katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwa na kiu Tamaduni.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Eangelistic
Assemblis of God Tanzania(EAGT) Stephano Nzowa wakati wa sherehe za
Kuwatunuku Udakitari wa Falisafa PHD Askofu Emmanuel Shani na mkwe Hosena Chales katika
Viwanja vya kanisa hilo wilayani Nzega Mkoani Tabora.
Amepata PHD hiyo katika Chuo Kikuu cha Africas
Graduate University kutoka Nchini Senegal na
Bregedia General Dk,Timothy Kasembe mbele ya waumini wa kanisa
hilo.
Dk,Nzowa alisema kuwa Elimu ni Bahari pana ambayo
inapaswa kila mtu kuogerea humo kwani bila Elimu hakuna maisha hivyo kila
nyakati yapaswa kupata nafasi ya kujifunza kwa bidiii.
Askofu Nzowa alisema viongozi wa makini hususani wachungaji na
maafisko wanapaswa kusomea Elimu mbalimbali ikiwemo ya kidini ili waweze
kukabiliana na mabadiliko ya kisanyans na Teknolojia katika jamii
mbalimbali.
Alisema kuwa Viongozi wa Dini wakisoma wataweza kubadilisha Jamii
inayo wazunguka kupitia Elimu hiyo na kuongeza kuwa jamii imebadilika kwa kias
kikubwa tofauti na hapo zamani.
Alisema kuwa suala la Elimu limeelezwa katika vitabu vya mungu kwa
nyamba mbalimbali hivyo Viongozi wa kidini wanapaswa kuyatenda hayo iliwaweze
kufikia malengo kwa Nyanja mbalimbali kadri uwe zavyo.
Dk,Askofu Mkuu wa kanisa hilo Stephan Nzowa aliwataka Vijana
kuiishika Elimu kama walishikavyo neon la Mungu iliwaweze kufikia malengo yao
ya kimaisha ikiwa na kufanya mambo mema kwa jamii inayo wazunguka.
Alisema kuwa jamii ya watu waliosoma hufanya matendo mema kwa
wananchi ikiwa na kuendeleza mema na kupinga mabaya kama maandiko yanavyo sema
dhidi ya suala hilo la Elimu.
Mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha udakitari wa Falisafa PHD Dk,Askofu
Emmanueli Shani aliwataka wazazi na walezi kufanya juhudi kupeleka watoto shule
ikiwa na kusimamia maendeleo ya wanafunzi iliwaweze kufikia malengo.
Akizungumzia mchakato wa kupata Elimu Dk,Emmanueli Shani
alisema kuwa suala la Elimu lina changamoto nyingi katika kufikia malengo na
kuwataka wazazi na walezi kuvumilia changamoto hizo iliwaweze kufikia malengo
husika.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walisema kuwa Elimu nikitu muhimu
katika maisha ya mwanadam hivyo wananchi na jamii kwa ujumla inapaswa kujikita
katika kuendana na mazingira husika ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa.
Alisema kuwa Elimu ya sasa ni ile ya chuo kikuu na vyuo mbalimbali
ikiwa na kusomea fani furani ambayo itaweza kukutoa sehem moja hadi kukufikisha
sehemu nyingine ya kimaisha ikiwa na kuisaidia jamii husika.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment