TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 05/05/2014.
Ndugu
waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora ifuatayo ni taarifa ya
tukio moja la kifo na taarifa ya Operesheni
inayoendelea katika wilaya zote za mkoa wa Tabora. Ambapo kufuatia operesheni
hizo tulifanikiwa kukamata watuhumiwa wa makosa mbali mbali kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 04.05.2014
majira ya saa 10:00hrs huko eneo la Utwigu wilaya ya Nzega FRANCE S/O AMBROSE
HUSSEIN 11yrs, Mnyamwezi mwanafunzi wa darasa la Tano katika shule ya Msingi
Mwanhala alifariki dunia baada ya kutumbukia katika bwawa la maji ambapo
alikuwa ameenda kwa ajili ya kuogelea.
Tarehe 01.05.2014 huko
wilaya ya Nzega alikamatwa FROLA D/O SHIJA, 28yrs, mnyamwezi, mkulima na mkazi
wa kujiji cha Igalula akiwa na bunduki aina ya Gobore ambayo anamiliki kinyume
na sheria. Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani.
Aidha tarehe 02.05.2014 huko
katika eneo la Utwigu kata ya Nyasa wilaya ya Nzega walikamatwa SHIJA S/O
KAPONA, 39yrs, Mnyamwezi, Mkulima na BAHATI S/O SHIJA, 28yrs, wote wakazi wa
Utwigu wakiwa na vipodozi aina ya Lemon Vate Cream 02, Beater Soap 02, Deproson
chupa 15, Demason 01, na Banistar 01, vipodozi
hivyo vilibainika kuwa havifai kwa matumizi ya binadamu na mtaalam kutoka TFDA.
Watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.
Katika
opereheni hii pia wamekamatwa PILI D/O BUNDALA 65yrs, Mnyamwezi, MACHIBYA S/O
MGETE 40 yrs, Mnyamwezi, KULWA S/O MASANJA, 35yrs, Msukuma, DAUDI S/O KABOGA
28yrs, Msukuma, MWAJUMA D/O RAJABU, 30yrs, Mnyamwezi, na MWASITI D/O MUHOJA
37yrs, wote wakazi wa kata ya Nyasa – Nzega wakiwa na Pombe ya moshi lita 15,
pia watuhumiwa wote hawa ni watumiaji na wauzaji wa pombe hiyo haramu. Wote
wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Jeshi
la Polisi linazidi wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao ili
kukomesha na kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua wahalifu, aidha
wazazi napenda kuwakumbusha wazazi kuwaangalia watoto na kuwafuatilia katika
michezo yao ya kila siku, pia napenda kuwaasa wananchi kufuata sheria za nchi
na pia kwa wale wote ambao wanamiliki magobore kinyume na sheria wasalimishe
magobore hayo kwa kuwa operessheni hii ni endelevu.
Imetolewa
na :-
SUZAN KAGANDA – ACP
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.
No comments:
Post a Comment