NA LUCAS RAPHAEL
AFISA MAHUSIANO WA KAMPUNI YA ALLIENCES ONE HAMIS LIANA AKIONGEA NA WALIMU NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA MADAHA WILAYA YA UYUI WAKATI AKIKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 75 |
Kampuni
ya ununuzi wa tumbaku ya Allience One imetoa msaada wa madawati 75 yenye
thamani ya shilingi milioni 4,875,000/= katika shule ya msingi Madaha iliyopo
katika kijiji cha Mpenge kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora.
Akikabidhi
msaada huo Afisa mahusiano wa kampuni hiyo Hamis Liana amesema msaada huo wa
madawati utasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Alisema
msaada huo wa madawati uwe chachu kwa walimu kuongeza juhudi za kufundisha na
wazazi kujikita zaidi katika shughuli za kilimo kwa kuwa wamepunguziwa mzigo wa
kuchangia ununuzi wa madawati katika shule hiyo.
Liana
alibainisha kuwa kampuni ya Allience one imejiwekea mkakati wa kuchangia katika
shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu kwa kutoa
madawati na vitabu.
Afisa
huyo mahusiano alisema kampuni yake imekuwa ikichangia katika miradi hiyo
katika maeneo ambayo wananunua tumbaku kupitia vyama vya msingi vya ushirika
ambavyo vinaiuzia tumbaku kampuni hiyo.
“Wakulima
kupitia vyama vya msingi wamekuwa wakionesha jitihada za kuwauzia tumbaku,
hivyo nasi tunalazimika kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao”.
Alisema Liana.
Akipokea
msaada huo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Catherine Mmbando alisema anashukuru kwa
kupata msaada huo wa madawati kwani umeondoa tatizo la upungufu wa madawati
katika shule hiyo.
Alisema
kuwa shule hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 71 lakini kampuni hiyo
imefanikiwa kuwapatia madawati 75 ikiwa ni zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji ya
shule.
Mwalimu
huyo alisema shule yake yenye jumla ya wanafunzi 391 na walimu 13 kwa pamoja
watahakikisha wanatumia madawati hayo kwa uangalifu ili yaendelee kuleta tija
kitaaluma shuleni hapo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment