Issaya Mngulu – CP
Mkurugenzi wa
upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI)
|
JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI
TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE
11/06/2014
IGP ATEUWA TIMU YA WAPELELEZI KUCHUNGUZA
TUHUMA ZA WIZI KATIKA VYAMA VYA MSINGI MKOANI TABORA.
Ndugu
waandishi wa habari, Jeshi la Polisi Tanzania kutokana na maagizo ya Rais wa
Jamuhuri ya muungano na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama
mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliyoyatoa tarehe 07/06/2014 ya kuagiza timu
ya upelelezi kutoka makao makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya kuchunguza
wizi unaofanywa na vyama vya msingi kwa wakulima wa Tumbaku, timu hiyo
imeshawasili mkoani Tabora.
Timu
hii inaongozwa na Kamishna wa Polisi – Issaya Mngulu Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai Tanzania.
Kama
alivyoagiza Rais, timu hii maalum imekuja mahususi kwa ajili ya kuchunguza wizi
wanaofanyiwa wakulima wa tumbaku kupitia vyama vya msingi mkoani Tabora. Hivyo
timu hii inaanza kazi mara moja kwa kuchunguza chama kimoja hadi kingine ili
kuweza kubaini wizi na hujuma zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika ambazo
ni kero kwa wakulima wa tumbaku katika mkoa wa Tabora.
Natoa
rai kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kutoa ushirikiano kwa timu hii mara
wanapohitajika ili kuweza kukamilisha kazi yake.
Imetolewa na:-
Issaya Mngulu – CP
Mkurugenzi wa
upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI)
No comments:
Post a Comment