NA LUCAS RAPHAEL,TABORA.
Shehkh wa mkoa wa Tabora Salum Shaban Salum
na waumini wenzake wa dini ya kiislam watano wamefikishwa mahakama ya
hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wakikabiliwa na shitaka la kutishia kufanya fujo.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wa Tabora Issa Magoli ilidaiwa na wakili
wa serikali Juliana Changalawe kuwa watuhumiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo
tarehe 14/06/2014 katika msikiti mkuu wa mkoa uliopo eneo la Gongoni mjini
hapa.
Wakili huyo aliiambia mahakama kuwa siku hiyo majira ya mchana watuhumiwa
Shaban Salum, Mgude Ahmed, Said Maganga, Kassim Shomary, Abubbakar Ludenga na
Kassim Rajab walimtoa sehemu ya ibada
Shehkh Ibrahim Mavumbi.
Watuhumiwa ambao wanawakilishwa na wakili msomi Mussa Kwikima wa miji hapa mara
baada ya kusomewa shitaka hilo waote walikana na kesi hiyo imeahirishwa hadi
tarehe 30/06 kwa ajili ya kuanza
kusikilizwa kwani upelelezi umeisha kamilika na wote walipata dhamana.
Kukamatwa hadi kufikishwa mahakamani kwa shehkh huyo na wenzake kunafuatia
mgogolo ambao umekuwa ukiendelea na
kupelekea Mufti wa Tanzaniia Shaban
Simba kutangaza kumuengua shehkh wa mkoa wa Tabora
Shaban Salum kitendo ambacho kinapingwa na baadhi ya waislamu.
Katika mgogolo huo baadhi ya waislamu wanapinga uhamzi huo ambapo Mufti
alimtangaza shehkh Mavumbi Ally kuwa kaimu shehk wa mkoa wakati kwenye uchaguzi
alishindwa .
Hata hivyo habari kutoka ndani ya waumini wa dini ya kiislam mkoani hapa
wanadai kuwa mgogolo huo unachochewa na viongozi wa serikali ambao
wanalazimisha shehk mavumbi ndiye awe kiongozi wa mkoa wa dini hiyo.
Shehkh wa mkoa wa Tabora Salum Shaban Salum na waumini wenzake wa dini ya kiislam watano wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wakikabiliwa na shitaka la kutishia kufanya fujo.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wa Tabora Issa Magoli ilidaiwa na wakili wa serikali Juliana Changalawe kuwa watuhumiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo tarehe 14/06/2014 katika msikiti mkuu wa mkoa uliopo eneo la Gongoni mjini hapa.
Wakili huyo aliiambia mahakama kuwa siku hiyo majira ya mchana watuhumiwa Shaban Salum, Mgude Ahmed, Said Maganga, Kassim Shomary, Abubbakar Ludenga na Kassim Rajab walimtoa sehemu ya ibada Shehkh Ibrahim Mavumbi.
Watuhumiwa ambao wanawakilishwa na wakili msomi Mussa Kwikima wa miji hapa mara baada ya kusomewa shitaka hilo waote walikana na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30/06 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwani upelelezi umeisha kamilika na wote walipata dhamana.
Kukamatwa hadi kufikishwa mahakamani kwa shehkh huyo na wenzake kunafuatia mgogolo ambao umekuwa ukiendelea na kupelekea Mufti wa Tanzaniia Shaban Simba kutangaza kumuengua shehkh wa mkoa wa Tabora
Shaban Salum kitendo ambacho kinapingwa na baadhi ya waislamu.
Katika mgogolo huo baadhi ya waislamu wanapinga uhamzi huo ambapo Mufti alimtangaza shehkh Mavumbi Ally kuwa kaimu shehk wa mkoa wakati kwenye uchaguzi alishindwa .
Hata hivyo habari kutoka ndani ya waumini wa dini ya kiislam mkoani hapa wanadai kuwa mgogolo huo unachochewa na viongozi wa serikali ambao wanalazimisha shehk mavumbi ndiye awe kiongozi wa mkoa wa dini hiyo.
Sheikh Shaaban Salum akiwa na baadhi ya waumini waliounganishwa naye katika kesi moja mahakama ya hakimu mkazi Tabora mjini. |
No comments:
Post a Comment