Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI
ya Simon Group Limited imesisitiza dhamira yake ya kuboresha sekta ya
usafiri katika Jiji la Dar es Salaam licha ya kampeni zinazoendelea
kutoka kwa washindani binafsi ikiwa na lengo la kuvuruga mpango
unaoendelea wa uwezekezaji katika Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA)
ili waweze kuitawala biashara ya usafiri.
Kwa
mujibu wa taarifa ya UDA, mpango unaendelea wa kuifanya Dar es Salaam
liwe jiji lenye urahisi katika usafiri kwa kufanya kazi kwa karibu na
Serikali na Jiji.
“Tumeona
taarifa ambazo zimekuwa zikichapishwa katika vyombo mbalimbali vya
habari ikiwamo mitandao ya kijamii kutoka katika kundi linalojiita
Consortium of Concerned Tanzanians International wakijaribu kuwafanya
watu waamini kila uwekezaji unaofanywa katika kuboresha mfumo wa usafiri
jijini Dar es Salaam kupitia UDA hauna maana.
“Hili
ni hatua inayosikitisha sana, tunajaribu kuuboresha mfumo wa usafiri
Dar es Salaam kutoka katika msongamano ili kuwa katika hali
inayoridhisha kwa kuongeza idadi ya magari na kuboresha huduma za
usafirishaji lakini watu wengine wanatumia muda mwingi kufanya kampeni
zenye lengo la kuhakikisha malengo hayo hayatimii,’’ ilisema taarifa
hiyo kutoka kwa mwenyekiti ambaye pia ndiye Ofisa Mtendaji Mkuu, Robert
Kisena.
Aliitaja
kampeni hiyo iliyopewa jina la “Kampeni ya Kurudisha Shirika la Usafiri
Dar es Salaam (UDA) Mikononi mwa wananchi” inajaribu kuligeuza mtaji
suala la kujivunia umiliki wa kampuni hiyo kwa umma bila ya kuangalia ni
vipi kampuni inaweza kusimamiwa kwa namna bora na kufanikiwa kutimiza
malengo ya kurahisisha usafiri Dar es Salaam.
Alisema
kwamba kampuni yake iliamua kuwekeza UDA baada ya kutangazwa
kubinafsishwa kwake kwa sababu kampuni ya Simon Group Limited ilitaka
kuleta mabadiliko yenye maana katika mfumo wa usafiri katika Jiji la
Biashara la Dar es Salaam hasa katika mabasi ya abiria na usafirishaji
kwa ujumla.
“Mpango
wa kuboresha usafiri umeelezwa vizuri katika mipango yetu ya muda mfupi
na muda mrefu inayoonyesha ni jinsi gani tuna mpango wa kusimamia
mabadiliko haya hatua kwa hatua. Katika mpango wetu pia tumebainisha ni
vipi tunajipanga kuihusisha Serikali na Jiji katika mpango mzima wa
usafiri Dar es Salaam. Naamini hii ndio maana hasa ya uzalendo, kufanya
kazi na serikali yako ili kutoa huduma bora kwa wananchi wake,’’
alieleza Kisena katika taarifa hiyo.
Katika
taarifa hiyo ofisa huyo mtendaji mkuu alibainisha kwamba mpango
walioudhamiria wa kampuni hiyo kuboresha huduma ya usafiri Dar es Salaam
uko pale pale ukihusisha mradi wa kuwa na mabasi zaidi ya 3,000 pamoja
na mabasi mengine ya kifahari 50 yenye viyoyozi na huduma ya internet.
Alisema
kwamba sambamba na mpango huo, kampuni itasimamia sera ya kuwaajiri
wataalamu wazawa badala ya kuwapa wataalamu wa kigeni kazi ambazo
Watanzania wanazimudu.
“Kampuni
ya Simon Group Limited inamilikiwa na Watanzania, katika hilo nitakuwa
mtu wa mwisho kumkubali mtaalamu wa kigeni kuajiriwa katika nafasi
ambayo inaweza kushikwa na Watanzania wenzangu. Kama hatutopata mtaalamu
Mtanzania, tutaleta wataalamu wa kuwapa mafunzo Watanzania ili baadaye
wazichukue nafasi hizo. Kampuni yetu inalifanya hilo kama njia mojawapo
ya kuwawezesha wazawa kiuchumi na kuwapa utaalamu.
Alisema
kwamba tathmini inaonyesha kuwa ili kuwezesha mabasi yapatayo 3000
kufanya kazi hapo baadaye wataalamu wapatao 7800 watahitaji kupewa
mafunzo na kuajiriwa.
Aliongeza
kwamba mara baada ya mpango huo kukamilika, unyanyapaa miongoni mwa
wanajamii kuhusu utumiaji wa mabasi ya uma hautokuwepo tena na watu
wataacha kupaki magari yao katikati ya jiji, watanunua tiketi za UDA kwa
njia ya mtandao jambo ambalo litapunguza msongamano Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment