Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Hamisi Mdee akielezea malengo ya mkutano huo wa wadau ambapo pamoja na mambo mengine alihimiza wadau kujitokeza kufungua maduka ya dawa muhimu vijijini ambayo yatasajiliwa NHIF na yatakuwa yakitoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii. |
Katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua akizungumza katika mkutano huo |
Meneja wa NHIF kanda magharibi Bw.Emmanuel Adina akitoa maelezo mafupi kuhusu mfuko huo kwa kanda ya magharibi. |
Baadhi ya viongozi na wadau wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati wa mkutano wa Wadau ambao unalengo la kujadili Changamoto mbalimbali zinazoukabili Mfuko huo. |
SERIKALI
mkoani Tabora imewaagiza viongozi na watendaji wote huduma za mfuko wa taifa wa
bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kuwa ajnda za vikao vyote
vya maamuzi.
Agizo
hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa kwenye mkutano wa siku
ya wadau wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) uliofanyika ukumbi wa mtemi
Mwanakiyungi.
Akisoma
taarifa kwa niaba ya mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu
alisema mkoa wa Tabora unaonyesha takwimu hadi kufikia mwezi machi 30 mwaka huu
ni kaya 39,969 sawa na asilimia 11 zimejiunga na CHF kati ya kaya 379,268
zilizopo mkoani Tabora.
Kingu
aliongeza takwimu hizo zinaonyesha kuwa viongozi mkoani hapa bado hawajatimiza
wajibu kuwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko.
Aidha
alisema kwa upande mwingine watoa huduma wamekuwa chanzo cha wananchi kukata
tama kujiunga na CHF huku wananchi wengine wakisita kujiunga na mfuko kutokana
nap engine kuwepo na huduma hafifu.
‘Ipo
haja ya kuangalia kwa umakini ni kwani kunakuwepo na kuzorota kwa utaratibu hu
ambao baadhi ya halmashauri hapa nchini umeimarika.’ alisema.
Mkuu
huyo wa mkoa pia aliwaasa watoa huduma kufanya kazi zao kwa weledi na bila
ubaguzi wowote kwa wananchi kwani mojawapo ya malalamiko ya wananchi ni
kukithiri kwa hali ya ubaguzi.
Aidha
aliwaomba wanachama wa NHIF na CHF kutumia kadi za matibabu kwa kuzingatia
taratibu zilizopo na kuacha tabia ya kuhamishana kadi au kufanya biashara ya
kadi hizo.
Mwassa
aliwaomba watumia wa NHIF kutimiza wajibu wao bila woga wakati wowote pale
wanapohitajika na kuwataka kushirikiana na serikali kutatua changamoto za mfuko
kwa pamoja.
Mwisho-
No comments:
Post a Comment