IMEELEZWA kuwa,vifo vya kina mama wanaojifungua katika ukanda
wa ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma vimepungua
kutokana na uboreshaji wa huduma ya upasuaji wa dharura katika kituo cha afya
cha Buhingu,ambacho awali kilikuwa kiwanda cha vifo hivyo.
Akifafanua hilo mbele ya wandishi wa habari kigoma Ujiji Mtaalamu Magonjwa ya kinamama Dr.Calist
Nzambuhakwa alisema awali wanawake wajawazito walikuwa wakihofu kubeba mimba,
kutokana na kuzorota kwa huduma hiyo ambapo kati ya wajawazito 578 kati ya vizazi hai 100,000
walikuwa wakipoteza maisha wakati wa kujifungua 2009-2013.
“kumsafirisha mama mjamzito kwenye boti la mbao la abiria ni
hatari, na kutoka kituo cha buhingu hadi hospitali ya rufaa Maweni kigoma mjini masaa 18 ,kifo kwa
wenye uzazi pingamizi , wanaovuja damu na kifafa cha uzazi hali ilikuwa tete,ndo mana
kituo kile kiliitwa kiwanda cha kifo kwa wajawazito” alibainisha
Dr.Nzimbahukwa.
Alisema Mradi wa Afya ya Uzazi wa shirika la World Lung Foundation
wamekidhi kuondoa idadi ya vifo kwa wahanga hao, kutoka vifo 12 kwa mwaka 2012
hadi vifo 2 kwa mwaka 2013 kati ya vizazi hai 1000 .
Kwa upande wa
wawakilishi wa Mradi wa World Lung Foundation Victoria Marijani na Dr.Ngukie
Mwakatundu kwa nyakati tofauti walisema mradi wao umelenga wilaya ya Kigoma ,Kasulu,Kakonko kwa kutoa vifaa tiba na mafunzo elekezi kwa
wahudumu katika vituo mtambukwa tisa
kikiwemo kituo cha Buhingu.
Walisema huduma yao
imeokoa vifo vya uzazi pingamizi 171 kwa
wanawake waliojifungua kwa njia ya kisu mkoani hapa na kuahidi kutumia
tathimini zao kujenga majengo bora ya
mapumziko ya kinamama wajamzito kutoka
vijiji vilivyopo mbali na vituo vya afya,kwa lengo la kuokoa maisha ya mama na
mtoto Huku wakiitaka serikali ichangie
katika hilo.
Naye Mganga Mkuu huo alisema 80% ya damu salama inatumika kwa
wakina mama na watoto,ambapo changamoto kubwa ya vifo hivyo ni kuvuja damu kwa
mlengwa wakati wa kujifungua ambapo vifo
68 katika vizazi hai 100,000 na kudai kuwa, hali hiyo itakwisha endapo jamii
itaendelea na hulka ya kutoa damu kwa hiari .
Alisema lengo la serikali na wadau wa afya ni kuboresha
huduma za wahanga hao,ambao ni chachu ya maendeleo ya nchi ,Huku akiwaonya
wahudumu wanaouza damu kwa wahanga hao na wananchi kwa ujumla,ambapo kisheria
ni kosa kuuza damu.
Aidha aliwataka wandishi wa habari wajikite kutoa elimu ya
umuhimu wa kutoa damu kwa hiari ,ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau hao
wanajenga kituo cha kukusanyia damu salama mkoani hapo, kutokana na mwitikio wa
umma husika kuchangia asilimia 114 ya damu salama .
No comments:
Post a Comment