Baadhi ya wanawake watatu katika soko la mkulima Tabora mjini wamejikuta wakipeana kipigo kikali mchana kweupe wakati walipokuwa wakifanya biashara za mbogamboga hatua ambao ilisababisha kuharibu sehemu ya bidhaa wanazouza ambapo muda mfupi baadae waliamuliwa ugomvi huo na askari polisi Fakih Abdul aliyekuwa akipita sokoni hapo,hata hivyo chanzo cha ugomvi huo kimetokana na mmoja wa wanawake hao kuwa mbabe kwa wenzake na hivyo kushindwa kumvumilia kutokana na vituko vyake.
Friday, July 25, 2014
WANAWAKE WATWANGANA SOKONI HUKU WAKIWA NA SWAUMU-TABORA
Baadhi ya wanawake watatu katika soko la mkulima Tabora mjini wamejikuta wakipeana kipigo kikali mchana kweupe wakati walipokuwa wakifanya biashara za mbogamboga hatua ambao ilisababisha kuharibu sehemu ya bidhaa wanazouza ambapo muda mfupi baadae waliamuliwa ugomvi huo na askari polisi Fakih Abdul aliyekuwa akipita sokoni hapo,hata hivyo chanzo cha ugomvi huo kimetokana na mmoja wa wanawake hao kuwa mbabe kwa wenzake na hivyo kushindwa kumvumilia kutokana na vituko vyake.
MAUAJI YA VIKONGWE YASHIKA KASI MLELE- KATAVI
Madiwani wakifuatilia kwa umakini wakati mwenzao akichangia hoja katika kikao hicho
(Picha zote na Kibada Kibada –Mlele Katavi)
Na Kibada Kibada –Mlele Katavi.
Wimbi la mauaji kwa watu wenye
umri kuanzia miaka 60 na kuendelea Wilayani Mlele Mkoani Katavi
linaonekana kushika kasi na kutishia hali ya ulinzi na usalama kama
hatua za makusudi hazitachukuliwa.
Hii ni kwa Mujibu wa Taarifa ya
Hali ya ulinzi na Usalama Wilayani humo iliyotolewa na Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa wilaya hiyo , Zabron Ibeganisa kwenye
Mkutano Mkuu wa Baraza la Madiwani uliokuwa ukipokea taarifa ya
utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha
mwaka wa 2013/2014.
Mkuu huyo wa upelelezi wa makosa
ya jinai alieleza kuwa changamoto zitokanazo na matukio ya mauaji ni
kubwa katika wilaya hiyo na watu wanaolengwa na mauaji hayo ni wale
wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ambapo kwa sehemu kubwa mauaji
hufanyika nyakati za usiku kwa kuwavamia walengwa kwenye makazi yao.
Alisema katika matukio 24
yaliyotokea, watu 24 kwa kipindi cha januari hadi juni mwaka
2014 wameuwawa na waliolengwa hasa ni watu wa umri huo.
Alisema kuwa wauaji hao hutumia
silaha zenye makali kama panga,shoka, na sime kuwakata waliowalenga na
kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote.
Mauaji haya yanafanana sana na jinsi yanavyotokea katika mikoa ya Shinyanga kwa kuwaua vikongwe kwa imani kwamba ni wachawi.
Aidha akifafanua zaidi alieleza
kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita kuanzia mwezi januari hadi
juni 2014 , yametokea mauaji 24 na watu 24 wameuwawa ambapo kati ya
mauaji hayo watuhumiwa sita walikamatwa.
Akibainisha hali ya uhalifu katika
wilaya hiyo alieleza kuwa matukio mbalimbali ya makosa madogo ya
kuwania mali yalikuwa 107 makosa makubwa dhidi ya binadamu kwa mauaji
yalikuwa 24, kubaka 23,kulawiti mawili ,makosa madogo dhidi ya Binadamu
yalikuwa 194, makosa madogo dhidi ya uvunjwaji wa maadili yalikuwa 108,
ajali zilizosababisha vifo ni mbili,ajali zilizosababisha majeruhi
zilikuwa 39, ajali za kawada 17, makosa mengine 844.
Makosa makubwa dhidi ya maadili ya
jamii kama kupatikana na bangi yalikuwa manane, kupatikana na pombe ya
moshi 8, makosa ya kupatikana na nyara za serikali yalikuwa matatu na
kupatikana na silaha moja
Ipo changamoto kutokana na ugumu
uliopo wa kuwatambua wauaji ,hata hivyo jeshi la polisi linatoa wito kwa
jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kuwaasa wana
jamii kuendeleza ule utaratibu wa daftari la wakazi kwa kuwaorodhesha
wakazi kwenye maeneo kwa kuwa ni muhimu na litasaidia kuwatambau wageni
wanaoingia kwenye maeneo na iwapo watakuwa na nia mbaya watabainika.
"MWANDISHI WA HABARI WA REDIO YA MHESHIMIWA RAGE MBARONI KWA KUJIFANYA USALAMA WA TAIFA,UONGOZI WA V.O.T WAMKANA
Kitambulisho alichokuwa akikitumia Mussa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu |
Uongozi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Tabora ulimfikisha Mwandishi huyo mbele ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni Afisa Usalama wa Taifa. |
"AJIRA YA VIJANA KWA USAFIRI WA BAISKELI TABORA NI MOJA KATI YA AJIRA TULIZOZITEGEMEA"
SERIKALI YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI WA BARABARA ZA JUU KWA JUU
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa
Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano
ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano
ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya
zaidi ya bilioni 128.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akionyesha michoro ya itakavyonekana barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam leo wakati wa kusaini hati ya makubaliano ya miradi miwili zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128 na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia).

"KILA MTU ANA HAKI YA KUGOMBEA UBUNGE,KAMA ULIWAJIBIKA VIZURI KWA WANANCHI WATAKUCHAGUA TENA"-MH.MUNDE
Na Mwandishi wetu.
"Hakuna mtu mwenye haki miliki ya Ubunge,kwani hiyo ni dhamana tu tuliyopewa na wananchi,lakini kwanini ifikie hatua ya watu kuhitilafiana na kugombana pasipo sababu za msingi"hii ni kauli ya Mbunge wa vitimaalumu mkoa wa Tabora Mheshimiwa Munde Tambwe wakati akizungumza na mtandao huu.
Wakati huu kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa kura za maoni kwa Chama cha Mapinduzi kumekuwa na hali ya kupigana vikumbo kwa baadhi ya makada wa Chama hicho hatua ambayo imebadili kabisa ukurasa wa maisha ya kawaida ya kibinadamu na kujenga sura mpya ya siasa za chuki kwa mtu mmoja kumchafua mwingine au kikundi cha watu fulani kumchafua mtu mmoja jambo ambalo linadhihirisha watu wamesahau kabisa majukumu yao na kugeuza kuwa ni ajenda muhimu ya katika maisha.
Jambo hili limemsukuma Mbunge wa vitimaalum Mheshimiwa Munde Tambwe na kuona kuwa watu wanakoelekea siko ambako CCM inataka kutekeleza malengo yake katika kuwahudumia wananchi ambao kimsingi ndio wamekiweka madarakani chama hicho.
"Ninavyofikiri mimi kwa muda huu sisi kama wanaccm ni vema tushirikiane,tujenge mshikamano katika kutekeleza Ilani ya Chama chetu badala ya kukaa tunajengeana chuki zisizo na msingi,yaani huyu kamsema yule na yule kamsema huyu,hii haitusaidii kabisa itatufanya tushindwe kujibu maswali ya msingi ya wananchi watakapo tuuliza nini tumefanya tangu tuwe madarakani"alisema Mheshimiwa Munde
"Ubunge si haki miliki ya mtu,kwani yeyote anahaki ya kugombea muda ukifika lakini kwasasa tunatakiwa kuwasaidia wananchi,wewe kama umewajibika ipasavyo kwa wananchi, wenyewe watakuchagua hata kama ni vipindi vitatu,lakini kama umepewa dhamana ya kuwa mbunge halafu unashindwa kutekeleza majukumu yako huna sababu ya kugombana na watu,wananchi wenyewe wataamua na wewe utavuna ulichopanda"msisitizo wa ziada wenye lengo la kujenga.
Kwa kauli hii ni vema pia watu waliopewa dhamana au ridhaa na wananchi ya kushika wadhifa walionao wapate fursa ya kujipima,je,wanayo nafasi tena ya kujitosa wakati wa kura za maoni utakapowadia?au ndio kuanzisha chuki na vurugu kwa kila mtu mwenye uwezo wa kifedha unayemuona amevaa sare ya Chama na kutoa misaada kwa watu unamhisi anataka kuchukua nafasi yako?
"Hakuna mtu anakatazwa kushirikiana na wengine katika kufanya kazi za chama ni vema tukafuata taratibu na kanuni za chama chetu na muda ukifika refarii atapuliza kipenga kila mmoja wetu ataona kama anauwezo wa kuomba nafasi anayoitaka kuliko kuanza kujipitisha huku na kule na kujinadi,binafsi sitofanya hivyo isipokuwa nawaombeni makada wenzangu tushirikiane kutekeleza Ilani ya chama chetu ili wenzetu wa vyama vya upinzani wakose la kuhoji"alisema Mheshimiwa Munde
"Chama cha Mapinduzi kina utaratibu mzuri sana katika kuwapata viongozi wa kada mbalimbali wakiwemo wabunge ni dhahiri kwamba mtu akifuata taratibu na kanuni za chama chetu atakuwa na haki ya kuwania nafasi anayoitaka na si kweli kwamba kutumia fedha kwa maana ya kuwahonga wapigakura inaweza ikawa sababu ya kuchaguliwa hilo si kweli"alisema huku akitahadharisha wanachama hasa makada ni vema wakashirikiana katika kutekeleza majukumu ya chama katika kutimiza ahadi zilizotolewa na viongozi wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi uchaguzi wa mwaka 2010.
"KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUUJENGA MKOA WETU,VIONGOZI TUWASAIDIE WATU WAONDOKANE NA UMASIKINI WA KIPATO,CCM DAIMA"
POLISI APONGEZWA BAADA YA KUKATAA RUSHWA YA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA-TABORA
Baadhi ya dawa za kulevya na vifaa vya matumizi ya dawa hizo zilizokamatwa zikiwa zinatumiwa na watu hao kumi na wawili waliokamatwa KENIOS GUEST HOUSE huko eneo la kata ya Isevya manispaa ya Tabora. |
Kamanda Suzy amesema watu hao baada ya kukamatwa walitaka kutoa rushwa ya shilingi elfu tisini kwa kiongozi wa timu ya makachero wanaofuatilia dawa za kulevya mkoani Tabora ambaye ni mkaguzi wa Polisi Harun Kasubi ambapo alikataa na kuwafikisha kituo kikubwa cha Polisi Tabora.
TRA YAFUTURISHA BAADHI YA WANANCHI TABORA
Baadhi ya viongozi wa Serikali na vyama vya siasa akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake UWT mkoa wa Tabora Bi.Mwanne Mchemba walishiriki katika hafla hiyo ya Futari |
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Abraham maarufu Nkokota naye alikuwa ni mmoja kati ya wageni waalikwa |
Baadhi ya walipa kodi wafanyabishara wa Tabora |
Baadhi ya watumishi wa TRA Tabora nao walishiriki hafla hiyo ya Futari |
Katibu wa ccm mkoa wa Tabora Bw.Idd Ali Ame akizungumza katika hafla hiyo ya Futari |
Mmoja kati ya viongozi wa dini ya kiislam Tabora mjini Sheikh Issa Bilali akisoma dua maalum wakati wa hafla hiyo. |
Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele akipeana mkono na Mkurugenzi wa fedha wa TRA nchini Bw.Mshoro,pembeni ni Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij |
|
Friday, July 18, 2014
WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUIELIMISHA JAMII KUHUSU DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA LINALOTUMIA TEKNOLOJIA YA BVR
BENKI YA EXIM YAFUNGUA MILANGO KUSAIDIA MICHEZO KWA VIJANA TABORA
Reactions: |
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya walimu wa soka mafunzo yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi |
Mkufunzi wa mafunzo hayo ya walimu wa soka Meja mstaafu Omari Mingange akitoa maelezo mafupi wakati wa hafla ya ufungaji mafunzo hayo |
21 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA WA SOKA TABORA
Na Allan Ntana, Tabora
WAALIMU 21 wanaofundisha timu za mpira wa miguu kutoka mikoa ya
Simiyu, Shinyanga, Mbeya na Tabora wamehudhuria na kuhitimu mafunzo ya
ukocha (intermediate course) yaliyofanyika katika uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora.
Mafunzo hayo yaliyochukua muda wa wiki 2 yaliendeshwa na Mkufunzi
mahiri hapa nchini Meja mstaafu Abdul Omar Mingange toka jijini DSM,
ambapo washiriki 22 walitoka mkoani hapa huku 2 wakitokea Shinyanga, 1
Simiyu na 1 jijini Mbeya.
Akikabidhi vyeti kwa waalimu hao, Meneja Masoko wa benki ya EXIM tawi
la Tabora Jeremia Bajebere aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Meneja
wa tawi hilo Edwin Poul aliwataka wahitimu hao kujiendeleza zaidi ili
wawe na kiwango kikubwa kwani ukocha ni ajira nzuri sana siku hizi na
inalipa.
Mwenyekiti wa Chama cha Makocha (TAFCA) mkoani Tabora Mwl Mohamed Ali
Mozi alisema lengo la mafunzo hayo ni kuinua viwango vya makocha toka
ngazi ya awali kwenda ngazi ya juu ili waweze kutoa elimu bora
itakayosaidia kuinua kiwango cha soka kwa vijana katika mikoa yao.
‘Hawa waalimu wamepata taaluma nzuri sana ya mpira wa miguu, naamini
watasaidia sana kuinua soka la vijana mashuleni na katika vilabu
mbalimbali ikiwemo kutambua vipaji vya wachezaji na kuviinua’,
aliongeza.
Aidha alisema changamoto kubwa inayowakabili waalimu wa soka hapa
nchini ni uhaba wa vifaa vya michezo vya kufundishia sambamba na vyama
vya soka kutowatambua na kuwatumia ipasavyo makocha wazawa kama mtaji
wa kuinua vipaji katika mchezo huo.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Meja mstaafu Abdul Omar Mingange amesifu
mwitikio mkubwa na kiwango kilichoonyeshwa na waalimu hao wakati wa
mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa nadharia na vitendo jambo ambalo
limewawezesha kufaulu kwa alama za juu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Tabora Yusuph Kitumbo
amepongeza hatua ya waalimu hao kujitokeza kwa wingi katika mafunzo
hayo kwani itaongeza idadi ya makocha wa soka mkoani humo huku
akiahidi kulipa gharama zote za vyeti vya wakufunzi hao.
Alisema kuwa kuanzia sasa timu zote hapa Tabora kuanzia daraja la nne
na kuendelea ni lazima zifundishwe na makocha waliopitia mafunzo
maalumu yaliyoandaliwa na chama cha Makocha TAFCA ili waweze kutumia
elimu yao vyema.

WASIO NA KADI YA BVR KUTOPIGAKURA 2015-KIGOMA,TUME
Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEELEZWA
kuwa,wananchi wasiokuwa na vitambulisho vya mfumo wa Biomertic Voter Registration
hawatahusika katika mchakato wa kupiga
kura wa maoni na uchaguzi mkuu 2015.
Akifafanua
hilo Kamishana wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Hamid Mahmoud alisema
wanananchi hawana budi kupokea mfumo huo,ambao ni tiba ya kuondoa
changamoto ya uchakachuaji wa mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara mbili.
“huu mfumo
wa BVR inachukua taarifa za kibailojia ya muhusika hivyo si rahisi kuibika
inatambua tabia,alama za vidole,sura,mpangilio wa mikono,mboni ya
jicho,sauti na harufu ya mtu na
kuhifadhiwa katika kanzi data na jamii
ishiriki kujiandikisha.” A libainisha Mahmoud.
Alisema
mchakato upo kwa watu wote, walio na kadi ya kupigia kura za awali zenye mfumo
wa `optical mark recognition’ kutoa
picha papo kwa papo na wale ambao wanatarajia kutimiza miaka 18 ifikapo 2015
wanawajibika kushiriki kupata kadi ya `BVR’
ili kuboresha daftari la kudumu la kupiga kura.
Kwa upande makam
Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Taifa Mohamed Kiboko alibainisha changamoto za awali ni
pamoja na kushindwa kubadilisha taarifa za mtu kwa wakati husika,majina
kujirudia zaidi ya mara moja,kuwepo na majina ya marehemu na kutoonekana kwa
majina ya wapigakura.
Alisema wananchi walio na kadi za awali wanahitajika
waende na vitambulisho hivyo ili wapewe vitambulisho vya kisasa na endapo
atakuwa amehama au kubadilisha taarifa zake inabidi atoe taarifa husika kwa
mwandishi mapema ili kurekebisha na kumwezesha kupiga kura eneo husika.
Aliongeza
kwa kusema wananchi wasio raia wa hapa watabainika kupitia wadau wao
kama tasisi ya Rita na Nida katika kuthibitisha data za muhusika na
kuomba wananchi wawe wazi kuwafichua wahamiaji wasio rasmi ili wasitumie
fursa hiyo.
Aidha
itambulike
kuwa,taifa hili si ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo kutokana na
nchi kadhaa wanatumia mfumo wa BVR ikiwemo
Zanzibar(2009),mali(2005),Nigeri(2007)Ghana(2009),Uganda(2008),Kenya(2013),Liberia(2005),Zambia(2008),Afrika
kusini
(2009),guinea(2005.
Alisema changamoto
zilizojitokea katika mataifa hayo hayahusiani na mfumo huo wa Biometric na
kudai mfumo huo ni tiba sahihi ya changamoto za awali ambazo ziliikwaza tume
hiyo na serikali husika.
JENGO LA MAABARA YA KISASA LA NIMR LAFUNGULIWA TABORA
Mkurugenzi wa NIMR Tabora Dr.Joseph Swila akionesha baadhi ya vifaa vya kisasa katika chumba cha maabara hiyo ambayo inatajwa kuwa huenda ikasaidia mikoa yote ya kanda ya magharibi. |
Jengo la maabara ya utafiti katika kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu lililogharimu zaidi ya shilingi milioni.297.8 |
Dr.Hassan Mshinda akiangalia moja ya mashine ya kupimia magonjwa ya binadamu wakati akikagua jengo hilo na kuangalia vifaa tiba vilivyomo katika jengo hilo. |
Mkurugenzi wa NIMR Tabora Dr.Joseph Swila akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la maabara ya Tabora |
Mkurugenzi mkuu wa NIMR Dr.Mwele Malecela wakati akisoma taarifa fupi tangu kuanzishwa kwa maradi wa Jengo hilo la maabara ya kisasa. |
Mwenyekiti wa Bodi ya NIMR ,Prof.Samwel Masele Akizungumza wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa jengo la maabara ya kisasa. |
Mwandishi wa habari mkongwe wa Redio Tanzania Bw.Benkiko ambaye alipata fursa ya kusalimiana na mgeni rasmi wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo hilo |
Wadau mbalimbali wa afya walihudhuria katika sherehe za ufunguzi wa Jengo hilo.Picha zote na TABORALEOhabari.COM |
Subscribe to:
Posts (Atom)