Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEELEZWA
kuwa,wananchi wasiokuwa na vitambulisho vya mfumo wa Biomertic Voter Registration
hawatahusika katika mchakato wa kupiga
kura wa maoni na uchaguzi mkuu 2015.
Akifafanua
hilo Kamishana wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Hamid Mahmoud alisema
wanananchi hawana budi kupokea mfumo huo,ambao ni tiba ya kuondoa
changamoto ya uchakachuaji wa mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara mbili.
“huu mfumo
wa BVR inachukua taarifa za kibailojia ya muhusika hivyo si rahisi kuibika
inatambua tabia,alama za vidole,sura,mpangilio wa mikono,mboni ya
jicho,sauti na harufu ya mtu na
kuhifadhiwa katika kanzi data na jamii
ishiriki kujiandikisha.” A libainisha Mahmoud.
Alisema
mchakato upo kwa watu wote, walio na kadi ya kupigia kura za awali zenye mfumo
wa `optical mark recognition’ kutoa
picha papo kwa papo na wale ambao wanatarajia kutimiza miaka 18 ifikapo 2015
wanawajibika kushiriki kupata kadi ya `BVR’
ili kuboresha daftari la kudumu la kupiga kura.
Kwa upande makam
Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Taifa Mohamed Kiboko alibainisha changamoto za awali ni
pamoja na kushindwa kubadilisha taarifa za mtu kwa wakati husika,majina
kujirudia zaidi ya mara moja,kuwepo na majina ya marehemu na kutoonekana kwa
majina ya wapigakura.
Alisema wananchi walio na kadi za awali wanahitajika
waende na vitambulisho hivyo ili wapewe vitambulisho vya kisasa na endapo
atakuwa amehama au kubadilisha taarifa zake inabidi atoe taarifa husika kwa
mwandishi mapema ili kurekebisha na kumwezesha kupiga kura eneo husika.
Aliongeza
kwa kusema wananchi wasio raia wa hapa watabainika kupitia wadau wao
kama tasisi ya Rita na Nida katika kuthibitisha data za muhusika na
kuomba wananchi wawe wazi kuwafichua wahamiaji wasio rasmi ili wasitumie
fursa hiyo.
Aidha
itambulike
kuwa,taifa hili si ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo kutokana na
nchi kadhaa wanatumia mfumo wa BVR ikiwemo
Zanzibar(2009),mali(2005),Nigeri(2007)Ghana(2009),Uganda(2008),Kenya(2013),Liberia(2005),Zambia(2008),Afrika
kusini
(2009),guinea(2005.
Alisema changamoto
zilizojitokea katika mataifa hayo hayahusiani na mfumo huo wa Biometric na
kudai mfumo huo ni tiba sahihi ya changamoto za awali ambazo ziliikwaza tume
hiyo na serikali husika.
No comments:
Post a Comment