Monday, February 4, 2013

CCM NZEGA WAOMBA WILAYA KICHAMA KUTOKA JIMBO LA BUKENE

MWENYEKITI WA CCM WA WILAYA YA NZEGA AKITETA JAMBO KA KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA WA MKOA WA TABORA EMENUELI GEMBE KABLA YA KUANZA KWA MAANDAMANO YA KUTIMIZA MIAKA 36 YA CCM KIMKOA YALIFANYIKA NZEGA

KATIBU WA UMOJA WA VIJANA WA CCM MKOA WA TABORA KAPETO AKIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA MKOA WA TABORA

KATIBU WA CCM WA MKOA IDD AME AKIWA NA KATIBU WA UVCCM MKOA KAPETO NA VIONGOZI WENGENE WA CCM WA WILAYA YA UYUI

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA TABORA HASSANI WAKASUVI WAKIWA KATIKA MAANDANO YA KUTIMIZA MIAKA 36 WA CCM KWENYE OFISI YA CCM WILAYA YA NZEGA

MWENYEKITI WA CCM NA MKUU WA WILAYA YA NZEGA BITUNI MSANGI AKLIYEVAA USHUNGI WAKIANZ MAANDAMANO KUTOKA OFISI ZA CCM WILAYA YA NZEGA

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA NZEGA AMOS KANUDA AKIWA NA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA IGUNGA COSTA OLOMI KWENYE VIWANJA VYA CCM WILAYA YA NZEGA KABLA YA KUANZA KWA MAANDAMANO HAYO









"WAZEE WABARIKI NDOA KANISA LA MORAVIAN TABORA,WENGI WAFURAHIA TUKIO LA KIHISTORIA"

 Mchungaji akiwaaga wanandoa baada ya Ibada takatifu ya kubariki ndoa hiyo katika kanisa la Moravian Tabora ambapo Mzee Laurent Mchele alibariki ndoa yake na mkwewe Bi.Devota Laurent Mrisho.
Mchungaji akitoa mawaidha kwa ajili ya kuwaasa wanandoa Mzee Laurent Mchele na mkewe Bibi.Devota Laurent Mrisho wakati wa kubariki ndoa hiyo iliyokuwa kivutio kikubwa kwa waumini waliohudhuria katika ibada kanisa la Moravian Tabora mjini.

 Wakati wa kubariki ndoa hiyo huku mamia ya waumini wakishuhudia tukio hilo la heri kwa wanandoa hawa wawili.
 Wanandoa baada ya ibada ya kubariki ndoa hiyo wakiwa wametulia kama ilivyozoeleka kwa maharusi.


Mara baada ya kubariki ndoa hiyo baadhi ya ndugu na jamaa wa karibu pamoja na watoto, wajukuu wa Mzee Laurent Mchele na mkewe Bibi.Devota Laurent Mrisho walipiga picha ya pamoja ikiwa ni kumbukumbu ya tukio hilo la kihistoria.

SEMINA YA PSPF CHUO CHA UALIMU TABORA



 Wanachuo wa chuo cha ualimu mkoani Tabora,wakisikiliza mada kwenye simina iliyoendeshwa na PSPF hivi karibuni.
 Afisa Mfawidhi wa mfuko wa PSPF,Lupakisyo Mwaipungu,akitoa mada kwenye semina iliyofanyika chuo cha ualimu Tabora.

 Victor Luvena,akitoa mada kwenye semina iliyoendeshwa na mfuko wa PSPF ambayo ilifanyika chuo cha ualimu Tabora.

 Mmoja wa wanachuo cha ualimu mkoani Tabora,akiuliza swali kwenye semina hiyo.



JK AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO KIGOMA


22
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wana CCM katika makao makuu ya CCM Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza Matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho yanayofikia kilele leo kwa  sherehe kubwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Chama cha Mapinduzi CCM kinahitimisha sherehe hizo baada ya Sekretarieti yake ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kufanya shughuli mbalimbali za kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali mkoani Humo.
23
Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maandamano hayo wakimshangilia Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiongea nao.
9
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akijiandaa pamoja na viongozi wengine wa chama wakijiandaa tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano mjini Kigoma leo asubuhi.
10
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akiongoza  viongozi wengine wa chama katika  matembezi ya mshikamano yaliyofanyika leo mjini Kigoma  asubuhi.
12
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kulia akiwa na Edward katika matembezi hayo.
13
Matembezi ya Mshikamano yakielekea ofisi ya CCM mkoani Kigoma.
15
Brass Band ya Jeshi la Polisi ikongoza matembezi hayo leo asubuhi.
16
Wananchi mbalimbali wakiwa wamejipanga kando ya barabara wakati matembezi hayo yakipita.
17
Wananchi mbalimbali wakiwa wamejipanga kando ya barabara wakati matembezi hayo yakipita.
1
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kulia ni Katibu wa Halmashauri kuu Oganizesheni Mohamed Seif Khatib.
2
Kutoka kulia ni Juma Kengele, Ahmed,  Michuzi, Adam na Othman wakishoo Love kwa picha.
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akimsiliza Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM.
4
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Dk. Rajab Rutengwe Mkuu wa mkoa wa Katavi.
6
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza  Mkuu wa Wilaya ya Kobondo Ndugu Venance Mwamoto, Katikati ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganizesheni.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mwigulu Nchemba.
8
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kabla ya kuanza kwa maandamano hayo leo asubuhi.
19
Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza barabarani wakati maandamano hayo yakipita kuelekea Ofisi za  CCM Mkoa wa Kigoma.
24
Kutoka Kulia ni Dk. Rajab Rutengwe Kanali Fabian Masawe Mkuu wa mkoa wa Kagera na mdau Alice wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maandamano hayo.

Friday, February 1, 2013

BALOZI ATAKA HOSPITAL YA NDALA KUTOA HUDUMA ZA AFYA KWA WATANZANIA


 Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla Askofu wa jimbo kuu la Tabora Paul Ruzuka akiwa na mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi wakikata utepe wa jengo la kutolea huduma ya mama na mtoto katika hospital ya Ndala baada ya kutimiza miaka 50
 Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla pamoja viongozi wengine wa serikali ya wilaya ya Nzega  na mtendaji mkuu wa hospital hiyo SR Geogretha Paul aliyeshika sahani ya mkasi na meneja wa kanda wa CSSC SIMIONI KASONGA
Askofu wa jimbo kuu wa tabora Paul Ruzoka akiteta jambo na mwakilishi wa papa hapa nchini

Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla akipokea zawadi kutoka kwa waumini wa kanisa la parish ya Ndala pembeni yake ni Sr George Paul

Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla akisoma maji kabla ya kubariki na kuyabariki majengo ambayo haliyafungua







NA LUCAS  RAPHAEL,NZEGA 

Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla amesema kuwa nchi ya Vatcan  itafanya kila linalowezekana kuhakikisha hospitali ya ndala wanaisaidiwa ili iweze kutoa huduma za afya kwa  watanzania kwa miaka mingine 50 na kukabiliana na  changamoto zilipo kwa sasa katika hospital zingine.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kufungua majengo ya kutolewa huduma kwa mama na watoto pamoja na chumba cha upasuaji chenye  vya  vifaa vya kisasa ambavyo vyote vimegharimu jumla ya shilingi milioni 465

Balozi huyo wa papa hapa nchini alisema kwamba huduma nzuri za afya kwa watanzania ndio kitu muhimu sana kwani bila afya hakuna amani, hakuna upendo na hakuna chochote ambacho wananchi wananweze kupata kumbukumba ya kuwepo kwake hospital hiyo hata baada ya miaka 50 ijayo.

“umati uliofika hapa unataka kujua je huduma zinazotelewa katika hospitali hiyo zitaendelea kuwepo vile vile ama zitakuwa nzuri kwa watu wanaipata huduma hizo “alisema balozi  Padilla

Aidha aliwataka watoa huduma wote wa hospital hiyo kufanya kazi kwa moyo wa kujitolewa kwa watanzania wote wanaofika katika hospital hiyo kupata huduma ya matibabu ili kutumiza malengo ya mungu kwa kutoa na kutoa na kupokea .

Hata hivyo alisema kwamba hospital ya ndala kutimia miaka 50 ikiwa inaendela kutoa tiba kwa wananchi wa Tanzania ni jambo nzuri la kujivunia na lamafanikio makubwa sana kwa kanisa na waumini wake

Awali Sista mkuu wa Hospitali hiyo Bernadette Kessy wakati akisoma risala kwa barozi wa papa nchini Askofu mkuu Fracinsco Padilla kwenye sherehe ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya utoaji huduma za afya tangu kuanza kwake mnamo mwaka 1963.

Aidha hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo kuu la Tabora licha ya kutikiza miaka 50 tangu ianze kutoa huduma ya  afya kwa jamii mwaka 1963 bado inakabiliwa uhaba mkubwa wa fedha zakununulia madawa ya kutosha, vifaa tiba, vitendanishi na upungufu wa watumishi wa kada zote.


Kessy alisema kuwa mbali ya ukosefu huo wa fedha pia wanakabiliwa na ukosefu wa chumba cha chenye ukubwa wa kutosha kwa ajili ya kutolea huduma za maabara ya magonjwa ya binadamu.

Pia alisema kwamba hospitali hiyo inaukosefu wa gari la huduma kwa wagonjwa waliombali na hospitali gari ambalo hutumika kusarisha wagonjwa mahututi katika hospitali za rufaa.

Hata hivyo Sista Kessy alimweleza balozi huyo wa Vatcan nchini kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo lakini wameweza kuboresha miuondombinu ya majengo ya zamani na kuyafanya kuwa ya kisasa .

Aidha amebainisha kwamba mbali na kuboresha majengo hayo, wameeza kujenga majengo mengine manne mpya ambayo ni jengo la huduma ya upasuaji, jingo la huduma ya tiba kwa watu wanaishi na VVU, jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto pamoja na jengo la wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu.


Mwisho

RAIS JOSEPH KABILA ATEMBELEA NCHINI TANZANIA

kabila1 e0967
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

kabila2 5daa4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
kabila3 3b705

kabila aa938
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt  Kilimanjaro jijini mchana wa leo Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU

MWANASHERIA AWATAHARISHA KIDATO CHA SITA NA NDOA ZA UTOTONI


 Mwanasheria wa kujitegemea Bw.Emmanuel Mwasaka akitoa cheti kwa mhitimu wa kidato cha Sita katika mahafali ya Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana ambapo Bw.Mwakasaka alikuwa mgeni rasmi.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana Bi.Helen Makala akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika shule hiyo. 
 Baadhi ya watumishi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana wakiwa katika mahafali hayo.
 Wahitimu wa kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana wakiimba nyimbo ikiwa ni sehemu ya mahafali.


Na Lucas Raphael-Tabora

Mwanasheria wa kujitegemea nchini Bw.Emmanuel Mwakasaka amewatahadharisha  wahitimu wa kidato cha Sita  na suala la ndoa za utotoni kwakuwa zimekuwa zikikwamisha maendeleo ya kutaka kujiendeleza zaidi  kielimu.

Akizungumza katika mahafali ya kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Tabora wasichana Bw.Mwakasaka ambaye pia ni mdau wa maendeleo mkoani Tabora,alisema ipo haja kwa wahitimu hao kuwa na mtazamo wa kuendelea zaidi na masomo kuliko kufikiria kuolewa wakati huu wakiwa na umri mdogo jambo ambalo huenda likawatia kwenye matatizo katika maisha yao.

Alisema maisha ya sasa yamekumbwa na changamoto nyingi ambapo kwa sehemu kubwa ya maisha yanahitaji kujitosheleza zaidi kielimu ili kuweza kuyamudu.

''Hivi sasa jamani mtakuwa katika kipindi kigumu sana wakati huu mnapokwenda majumbani kwenu,changamoto ni nyingi hasa mbaya zaidi kwa ninyi mnaokwenda vijijini,maana huko si ajabu mnaweza kuwa wazazi au walezi wenu wamekwisha chukua fedha kwa ajili ya kuwaozesheni"alisema Mwakasaka.

Hata hivyo Bw.Mwakasaka pamoja na kuahidi kusaidia komyuta tatu,Projekta moja na Jenereta moja katika Shule hiyo alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wanaobaki Shuleni hapo kuona umuhimu wa masomo ya Sayansi ambayo kimsingi alidai kuwa yamekuwa yakitoa ajira kwa wingi kuliko masomo mengine ulimwenguni.

Kwaupande wake mkuu wa Shule hiyo ya Tabora Wasichana Bi.Helen Makala katika risala yake kwenye mahafali hayo alisema kukosekana kwa uzio katika Shule hiyo ni moja ya changamoto kubwa na ni tishio kwa maisha ya wanafunzi hao wakike.

Alisema licha ya Shule hiyo kufanya vizuri lakini wanafunzi wamekuwa wakiishi katika mazingira ya wasiwasi kutokana na vibaka kuvamia mara kwa mara na kuiba nyakati za usiku.

"Shule hii ina eneo la hekta 97.4 hakuna uzio wowote hata wa kuzunguuka eneo dogo linalozunguuka majengo,mazingira haya ni hatarishi zaidi kwa wanafunzi wa kike wakiwemo albino na wasioona"alisema mkuu huyo.

Aidha Shule ya Tabora wasichana ambayo ni ya bweni ilianzishwa mnamo mwaka 1928 ikitajwa kuwa baadhi ya viongozi wakubwa wanawake  wa serikali ya Tanzania wamesoma katika shule hiyo ambayo kwasasa inajumla ya wanafunzi wapatao 610.