Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla pamoja viongozi wengine wa serikali ya wilaya ya Nzega na mtendaji mkuu wa hospital hiyo SR Geogretha Paul aliyeshika sahani ya mkasi na meneja wa kanda wa CSSC SIMIONI KASONGA
Askofu wa jimbo kuu wa tabora Paul Ruzoka akiteta jambo na mwakilishi wa papa hapa nchini |
Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla akipokea zawadi kutoka kwa waumini wa kanisa la parish ya Ndala pembeni yake ni Sr George Paul |
Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla akisoma maji kabla ya kubariki na kuyabariki majengo ambayo haliyafungua |
NA LUCAS RAPHAEL,NZEGA
Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco
Padilla amesema kuwa nchi ya Vatcan itafanya kila
linalowezekana kuhakikisha hospitali ya ndala wanaisaidiwa ili iweze
kutoa huduma za afya kwa watanzania kwa miaka mingine 50 na kukabiliana na changamoto zilipo kwa sasa katika hospital zingine.
Kauli hiyo aliitoa baada ya kufungua majengo ya kutolewa
huduma kwa mama na watoto pamoja na chumba cha upasuaji chenye vya vifaa vya kisasa ambavyo vyote vimegharimu
jumla ya shilingi milioni 465
Balozi huyo wa papa hapa nchini alisema kwamba huduma nzuri
za afya kwa watanzania ndio kitu muhimu sana kwani bila afya hakuna amani, hakuna upendo
na hakuna chochote ambacho wananchi wananweze kupata kumbukumba ya kuwepo kwake
hospital hiyo hata baada ya miaka 50 ijayo.
“umati uliofika hapa unataka kujua je huduma zinazotelewa
katika hospitali hiyo zitaendelea kuwepo vile vile ama zitakuwa nzuri kwa watu
wanaipata huduma hizo “alisema balozi Padilla
Aidha aliwataka watoa huduma wote wa hospital hiyo kufanya
kazi kwa moyo wa kujitolewa kwa watanzania wote wanaofika katika hospital hiyo
kupata huduma ya matibabu ili kutumiza malengo ya mungu kwa kutoa na kutoa na
kupokea .
Hata hivyo alisema kwamba hospital ya ndala kutimia miaka 50
ikiwa inaendela kutoa tiba kwa wananchi wa Tanzania ni jambo nzuri la kujivunia
na lamafanikio makubwa sana kwa kanisa na waumini wake
Awali Sista mkuu wa Hospitali hiyo Bernadette Kessy wakati
akisoma risala kwa barozi wa papa nchini Askofu mkuu Fracinsco Padilla kwenye
sherehe ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya utoaji huduma za afya tangu
kuanza kwake mnamo mwaka 1963.
Aidha hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo
kuu la Tabora licha ya kutikiza miaka 50 tangu ianze kutoa huduma ya
afya kwa jamii mwaka 1963 bado inakabiliwa uhaba mkubwa wa fedha zakununulia
madawa ya kutosha, vifaa tiba, vitendanishi na upungufu wa watumishi wa kada
zote.
Kessy alisema kuwa mbali ya ukosefu huo wa fedha pia
wanakabiliwa na ukosefu wa chumba cha chenye ukubwa wa kutosha kwa ajili ya
kutolea huduma za maabara ya magonjwa ya binadamu.
Pia alisema kwamba hospitali hiyo inaukosefu wa gari la huduma
kwa wagonjwa waliombali na hospitali gari ambalo hutumika kusarisha wagonjwa
mahututi katika hospitali za rufaa.
Hata hivyo Sista Kessy alimweleza balozi huyo wa Vatcan nchini
kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo lakini wameweza kuboresha
miuondombinu ya majengo ya zamani na kuyafanya kuwa ya kisasa .
Aidha amebainisha kwamba mbali na kuboresha majengo hayo,
wameeza kujenga majengo mengine manne mpya ambayo ni jengo la huduma ya
upasuaji, jingo la huduma ya tiba kwa watu wanaishi na VVU, jengo la huduma ya
afya ya mama na mtoto pamoja na jengo la wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment