Na Lucas Raphael,Tabora
Siku
chache baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa nchini mkoani tabora
mwananfunzi aliyemaliza kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya
Kanyenye mjini Tabora, amejinyonga kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha nne
mwaka huu.
akizungumza
na waandishi wahabari ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP
Anthony Rutta amemtaja mwanafuzi huyo kuwa ni Michael Fidelis (19) ambaye ni
mkazi wa skanda mtaa Mwinyi kata ya chemchem Manispaa ya Tabora.
Alisema
mwanafuzi huyo alienda kuangalia matiokeo ya kidato cha nne majira ya saaa 11
jioni Februari 18 mwaka huu na badaye kukutwa amejinyonga hadi kufa chumbani
kwake kwa kutumia kamba ya manila.
Kamanda
Rutta alieleza kuwa marehemu alipata darajala mwisho kwa maana ya sifuri
aliacha ujumbe uliosomeka “Nisamehe sana mama usitafute mchawi, nakupenda sana,
uwamuzi niliochukua nisababu ya matokeo mabaya, nakutakia maisha mema” ulisema
sehemu ya ujumbe huo.
Mkuu
wa shule ya sekondari ya kenyenye alipokuwa akisoma mwanafunzi Fidelis, Kapufi
Patson alisema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ni mpole na mtaratibu na
wameshangazwa na uwamuzi aliochukua wa kujinyonga.
Matokeo
ya shule ya sekondari ya mwinyi yanaonyesha hakuna mwanafuzi aliyepata alama ya
ya kwanza na yapili huku waliopata darajala tatu wakiwa wanafuzi wawili,
daraja la nne 14 na waliopata sifuri ni wakiwa wanafunzi 85, wakati wanafuzi 36
matokeo yao hayaktoka kwasababu walikuwa wanadaiwa ada ya mtihani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment