Na Lucas Raphael,Nzega
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) Mkoani Tabora kimesema
madiwani ambao hawakuhudhuria katika sherehe za maadhimisho ya chama hicho
kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kutokana na kutoheshemu sherehe hizo .
Hayo yalisemwa na katibu wa chama hicho mkoa
wa Tabora Iddi Ame katika sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama hicho
kimkoa zilifanyika wilayani Nzega ambapo kwa sasa kina sherehekea miaka 36 toka
kizaliwe.
Alisema kuwa kuwa baadhi ya madiwani kupitia
tiketi ya chama hicho hawakuhudhuria katika sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa
kwa chama mapinduzi CCM wahesabu wameumia kwa kitendo chao hicho.
Alisema kuwa kitendo hicho chakuto kuhudhuria
sherehe hizo kubwa za kitaifa ni kukiuka maadili ya chama hicho na chadharau
kwa chama hicho.
Aliwataka madiwani hao pamoja na viongozi wengine
wa kichama kuheshemu sherehe hizo muhimu za kitaifa pamoja na maagizo
mbalimbali ya chama.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho mkoani
hapa ,Hassani Wakasuvi aliwata viongozi hao kuweka utamaduni wa kuzungumza na
wananchi mara kwa mara ilikujua kero zao na kuzifanyia utatuzi mapema.
Alisema kuwa viongozi hao endapo wakizungumza na
wananchi kwa nyakati mbalimbali wataweza kujiwekea imani kwa wananchi hao kwa
kutatua matatizo yatokeapo kwenye maeneo yao .
Mwenyekitu huyo aliwataka wabunge wa mkoa wa
Tabora kushirikiana kwa kikamilifu katika katika kutetea hoja zenye maslahi ya
wananchi ili kutimiza ahadi zao walizokuwa wamewaahidi wananchi hao wakati
walipokuwa na wanaomba uwakilishi bungeni.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment