Saturday, February 23, 2013

MAJANGILI MATATU YAUAWA MKOANI DODOMA LEO

 

Wameuawa kisha kuchinjwa na kuchomwa moto ndivyo miili ya marehemu wanaodhaniwa kuwa ni majangiri wa wanyama poli inavyoonekana ilipofikishwa kuhifadhiwa katika hospital ya Mvumi Dodoma.
Mwili wa Mtu anayedhani wa kuwa ni Jangili ukiwa umehalibika baada ya kuuawa kuchinjwa na kuchomwa moto katika chumba cha kuhifadhia maiti mvumi Dodoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akiwaonyesha waandishi wa Habari meno 73 ya tembo yenye thamani ya zaidi 225 mil ambayo ni sawa na tembo 36 pamoja na Gari aina ya Noah NO T 983 BZJ waliokamata juzi katika kijiji cha Miganga mvimi wilayani Chamwino Dodoma.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habri kuhusu tukio la vifo vya watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majangili waliouawa na wananchi katika kiji cha miganga Mvumi Dodoma pembeni ni Gari aina ya Noah No T 983 BZJ walilokuwa wakilitumia na kuku meno 73 ya Tembo.
Na John Banda, Dodoma

MAJANGILI watatu wa nyara za serekali wameuawa kwa mishale yenye sumu na kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi katika purukushani na polisi walipokuwa wakijaribu kukimbia ili kutorosha meno  ya tembo.

Tukio hilo lilitokea jioni ya alhamis wiki hii katika kijiji cha Miganga kata ya mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo miili yao ilikutwa ikiwa imehalibika kutokana na kuchomwa moto.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alisema majangili hayo yaliuawa na wanachi wenye hasira kali kwa zana mbalimbali za kijadi walipokuwa wanakimbilia polini ili kujiokoa na mkono wa polisi.

Misime alisema jeshi hilo lipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kuwa kulikuwa na Gali likitokea Manda likiwa na Meno ya Tembo  na kisha kuweka mtego katika kijiji cha mwitikila ambapo waliona gali aina ya NOAH T 983 BZJ na kulisimamisha na Dereva wa Gali hilo alifanya kama anapunguza mwendo na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.

‘’Polisi wakishirikiana na wananchi walianza kulifukuza  walipofika kijiji cha Miganga Mvumi polisi walifanikiwa kupiga Risasi tairi moja ya kushoto na hivyo watu watatu waliokuwemo ndani gari hilo waliruka na kutawanyika, wananchi waliojichukulia sheria mkononi waliwashambulia kuasi cha kupoteza maisha yao’’, alisema
 
Aidha kamanda Misime alisema baada ya kulipekua Gari hilo walikutaMeno 73 ya Tembo yenye uzito wa kilo 255.9 yakiwa na thamani ya zaidi ya TSH 225 mil pamoja na hati ya mashitaka [CHARGE SHEET] ambayo ni kesi ya kuhujumu uchumi namba 4/2012 iliyokuwa imefunguliwa katika mahama yam panda mkoa wa katavi na Leseni ya Udereva na 4000692535 Aboubakar Peter huku wakihisi ni mmoja ya waliouawa.

Alisema walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la kupatikana na Meno 3 ya Tembo Tarehe 17.06.2012 na maafisa wanyama poli  katika eneo la Msaginya Wilaya ya Mlele mkoa wa katavi majina ya walikuwa wameshatakiwa ni Joseph Marius [NGONDO] 59 mkazi wa maili mbili Dodoma, Aboubakar Mhina 25 mkazi wa Mkuhungu Dodoma, Msafiri Milawa 36 mkazi wa Nkuhungu Dodoma na Petro Mtipula 55 mkazi wa mpanda.

Kamanda alitoa wito kwa wananchi wasijichukulie Sheria mikononi kwani kwa kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi na inawawia vigumu polisi kupata mtandao inayohusika na matukio kama hayo.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJAPURE BLOG

No comments:

Post a Comment