WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewataka waislam na wakristo wote Nchini kuungana kwa pamoja kuitetea na kuilinda amani tuliyonayo kwa vitendo.
Akizungumza katika Harambee ya kanisa la Moraviani kanda
ya magharibi iliyofanyika katika wilaya ya nzega mkoani Tabora,kuwa
waumini hao kwa pamoja wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika
kuitetea amani iliyopo kwa vitendo.
Lowassa
aliendelea kusisitiza kwamba kwa sasa kuna baadhi ya watanzania
wanaichezea amani iliyopo kwa sasa hapa nchini na kufanya mauaji ya
watumishi wa mungu lakini isiyo Tanzania tunayoihitaji .
Hata
hivyo alikuwa na kimwabingizo cha hii ni Tanzania tunayoihitaji ili
kuwa na upendo na utulivu amani tunayoisema tutailinda amani kwa nguvu
zote hapa Tanzania.
“hii ni Tanzania tunayoitaka kwa waislamu na wakristu kushirikiana katika ibada kama hii leo hapa kanisani “alisema Lowassa.
Alisema
kwamba katika maisha yetu ya kila siku ni watu wakutengemeana kwa kila
jambo kwani hakuna muda saa ambao uwezi kuacha kumuona muislam akipita
njiani na hata mkristo pia katika mitaa nayo ni hivyo hivyo .
Lowassa
aliendelea kusisitiza watanzania tunapaswa kuhakikisha kila siku
tunamuomba mungu ili kuendeleza amani yetu hapa Tanzania inadumishwa kwa
hali na mali.
Hata
hivyo katika changizo hilo la harambee ya kanisa la morviani kanda ya
magharibi alisema kwamba yeye ni tajiri wa watu nasio tajiri kama watu
wanavyosema huko mitaani .
Alisema
kwamba watu wanaomsema vibaya kila kukicha waendelea kufanya hivyo
kwani kwafanya hivyo wanaendela kumuimarisha kiimani na nguvu kubwa ya
ushawishi kwa watu wa mungu amboa ndio wamekuwa wakimuunga mkono kila
siku katika kazi ya mungu.
“mimi nitajiri wa watu nasio tajiri wa fedha kama wanavyo sema huko mitaani na watu wasiokuwa na mapenzi mema na mungu”alisema lowassa
Aidha
katika harambee walikuwapo waislamu kutoka mikoa ya mwanza ,shinyanga
na Tabora pamoja na viongozi mbalimbali wa siasa kutoka sehemu mbalimbli
hapa nchini.
Askofu Mkuu wa kanisa la moraviani kanda ya magharibi Issack Nicodemo alisema kuwa waislam na wakristo hapa nchi ni ndugu kutokana na mahusiano yaliyopo toka hapo awali.
Alisema
kuwa vitendo vinavyoendelea kufanyika hapa nchini vya mauaji kwa
viongozi wa dini ni vyakulaniwa na kongeza kuwa upendo na amani
inahitajika kupoteza suala hilo.
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la kaliua Profesa Juma kapuya alisema kuwa
kunabaadhi ya watu wamelewa na amani iliyopo nchini hivyo amani inapaswa
iheshimiwe.
Naye
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa shinyanga Hamis Mgeja
aliwataka waislamu na wakristo kuliombea taifa hili ilikuweza kuwa na
amani na upendo.
Awali
Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa idara ya
wanawake wa kanisa la Morania Agness Nsanto katika harambee hiyo
ikiongozwa na waziri mstaafu Edward Lowassa ilifanikiwa kukusanya fedha
million 110,168,250,fedha tathilimu zilikuwa Million 36,706,250 wakati
ahadi zikiwa Million 71.
Hitaji harisi ilikuwa Millioni 80 ambapo wanawake hao walikuwa na Million 20 kama kianzio cha kukusanya fedha hizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment