Na Lucas
Raphael,Nzega
WANACHAMA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Wilayani Nzega Mkoani Tabora wameutaka mfuko huo uboresha huduma
zake katika Hospital ya wilaya ya Nzega ili wachama wa mfuko waweze
kunufaika na huduma hizo
Wakizungumza katika kikao cha Bima ya Afya
kilichoandaliwa na Bima ya AFya kanda ya Magharibi,walisema kuwa katika
hospitali ya Nzega kuna uhaba mkub wa wa Dawa hali ambayo wananchama
huwapelekea kununua katika maduka ya Dawa nje ya hospital hiyo .
Licha ya kutokuwa na Dawa katika Hospitali
ya wilaya,wanachama hao wameiomba Bima ya Afya kanda ya magharibi kupitisha
moja ya Duka la Dawa muhimu ambalo litakalo weza kuwasaidia wanachama hao,
wakosapo Dawa katika Hospitali ya wilaya .
Walisema kuwa Duka la Dawa litakapo patikana
wilayani hapa pamoja na maduka mengine vijijini yataweza kuondoa kero na madukuduku
ya wanachama hao hasa wakosapo huduma katika hospitali ya wilaya.
Wakitoa malalamiko yao walisema kuwa baadhi ya watoa
huduma hospitalini hapo hutumia lugha chafu kwa wanachama hao pamoja na kutozwa
pesa kwa gharama ya matibabu watakayo patiwa.
Wakitoa ushauri wameutaka mfuko huo wa Taifa wa
Bima ya Afya kuboresha huduma bora za Afya pamoja na kufuata sera za
mfuko huo ili wanachama wanufaike maradufu.
Kaimu Meneja kanda ya Magharibi, Hipolit Lello
alikiri kuwepo kwa uhaba wa Dawa katika Hospital ya wilaya ya Nzega pamoja na
zahanati zake.
Lello akitoa ushauri kwa Halmashauri ya wilaya kuwa
itume maombi ya kupata fedha za tele kwa tele zitakazo weza kununua Dawa pamoja
na kuboresha mazingira ya huduma bora kwa wananchama hao tofauti na sasa
wanavyo lalamika.
Aliwataka wanachama hao kuwa hamasisha wadau
wengine wajiunge katika mfuko huo lengo likiwa ni kuwa saidia katika huduma za
Afya zenye bei nafuu pamoja na kuwa himiza wananchi kujiunga na (CHF),
ambapo kaya zilizo andikishwa 8,245 sawa na 7% ya kaya
zote.
Alisema kuwa kwa Idadi hiyo ni kidogo tofauti na
matarajio ya zoezi hilo ambalo ni mmoja ya huduma zenye gharama nafuu kwa
watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment