NA LUCAS RAPHAEL,NZEGA
Diwani wa Kata ya Mwamala wilaya ya
nzega mkoani Tabora Hamis Lubunga Shomali anashikiliwa na jeshi la Polis
kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya gunia 39 za mahindi ya msada
yaliyotowa kwa ajili ya watu waliopata tatiza la njaa.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bituni
Msangi kuwa viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma hizo za wizi wa mahindi kwa
gunia 39 za kata ya mwamala ambapo mahindi hayo yalipotea.
Msangi akizungumza na gazeti hili jana alisema
kuwa tukio hilo
lilitokea 29 January mwaka huu na taarifa hizo kufika ofiosni kwake
ziliwasilishwa na wananchi wasamalia wema juzi.
Alisema kuwa wananchi hao ambao majina yao yamehifadhiwa walitoa
taarifa hiyo na hatua kali za ufuatiliaji ulianza katika kata hiyo ya mwamala
ambapo uchunguzi wa awari ulibani kuwa viongozi hao akiwepo na diwani wa kata
hiyo aliyetambulika kwa jina la Hamis Lubunga Shomali wanatuhumiwa kuhusika na
ubadhilifu huo.
Akitaja majina nya watuhumiwa hao kuwani Diwani wa
Kata hiyo Hamis lubunga Shomali,Mtendaji wa kijiji Saidi Madua Saidi,mwenyekiti
wa kijiji Amosi Wambura pamoja na mlinzi aliyefahamika kwa jina moja la
Mashaka.
Alisema kuwa watuhumiwa wengine wanao tafutwa
kuhusika na tukio hilo kuwa ni kaim mtendaji wa
kijiji Nseka Munete,mlinzi mwingine Wambura mwita pamoja na Dereva wa roli hilo jina lake
halikufahamika.
Mkuu huyo alili ambia gazeti hili kuwa kata hiyo
ilipaswa kupokea magunia 193 sawa na tani 18 hata hivyo magunia ya awari yaliyo
pelekwa yalikuwa magunia 130 ambapo magunia hayo yalipo hesabiwi hayo na
kamati ya ulinzi na u8salama ya wilaya walikuta magunia 91.
Msangi alisema kuwa mahindi hayo hayakupokelewa na
kamati ya maafa haikupata taarifa kuwa mahindi yamefika na kuongeza kuwa
viongozi hao hawapaswi kupokea mahin di badala yake wao nikuwa waangalizi.
Aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea ilikubaini
mahindi yaliyo potea na kuwapata washiriki wengine ambao watakao bainika
kuhusika na ub adhilifu huo wa mahindi ya m saada.
Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa
vion gozi wa wilaya pal,e wanapo kuwa na mashakla ya utekelezaji wa maihindi
hayo pamoja na kuwahim iza viongozi wa ngazi za kata na vijiji kutambua wajibu
wao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
hiyo Rozalia Magoti alisema kuwa kamati za maafa zigawe mahin di hayo huku
viongozi wa kata na vijiji wasimamie zoezi hilo.
Alisema kuwa viongozi hao wanapaswa kutopa taarifa
za kila siku za ugawaji wa mahindi hao wa klila siku ikiwa na kugawa mahindi
hayo kwa uangalifu zaidi ili zoezi hilo
lifanikiwe.
Magoti amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa
kutosha katika kutoa taarifa hizo na kutoa ushirikiano kwa vion gozi wa kata na
vijiji,aliongeza kuwa uchunguzi wa jeshi la polis unaendelea ili kupata ukweli
zaidi katika suala hilo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment