Rais
Jakaya Kikwete jana amefanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma na
kukagua maendeleo ya Ujenzi wa daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi
wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Picha Zote na IKULU.
Rais Kikwete alitembelea daraja
hilo na kuzungumza na wananchi wa eneo jirani na daraja hilo na kuwataka
walitumie vyema katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia
ardhi yao kwa kilimo na si kuiuza kwa watu wengine.
Kikwete amewaambia wakazi hao kuwa
wasikubali kulubuniwa na wageni wanaokuja kama wawekezaji na kununua
maelfu ya hekta za ardhi yao.
No comments:
Post a Comment