Sunday, June 2, 2013

VITUKO MBELE YA WABUNGE KATIKA SHINDANO LA MISS TABORA

 
Mmoja wa washabiki wa muziki wa kizazi kipya ambaye alivaa vazi lililochangia kudondosha hata heshima yake ambaye alipanda jukwaani kumkumbatia  msanii  maarufu nchini Ommy Dimpoz  wakati alipokuwa akitoa burudani katika mashindano ya Redds Miss Tabora.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema  Bw.William Ngereja akiwa na Diwani wa kata ya Kitete manispaa ya Tabora Bw.Daniel Mhina ambaye alikuwa MC katika onesho hilo lililofanyika katika ukumbi wa Frankman Hotel mjini Tabora.
Ommy Dimpoz akitokwa na machozi wakati akitumbuiza jukwaani alipofikia hatua ya kumkumbuka marehemu msanii  maarufu Mangwea.
Ommy Dimpoz alionesha kukubalika zaidi katika onesho hilo
Mbunge Ngereja akiwa na mbunge wa vitimaalum mkoani Tabora wakijaribu kucheza kwa pamoja muziki uliokuwa ukiimbwa na Ommy Dimpoz.

ANNASTAZIA DONALD NDIYE MISS TABORA 2013


Redds Miss Tabora 2013 Annastazia Donald(19)ambaye ni mwanafunzi wa Theofil Kisanji University,kushoto ni mshindi wa pili katika kinyang'anyiro hicho  Sabrina Juma(18) kutoka chuo cha African Utalii na mshindi wa tatu ni Cornecia Cossei(21)kutoka chuo cha Utumishi wa Umma Tabora. 
Warembo baada ya kutangazwa na kupatiwa zawadi zao katika shindano lililofanyika ukumbi wa Frankman Hotel mjini Tabora
Redds Miss Tabora 2013 Annastazia  Donald akiwa  katika vazi la ufukweni ambalo lilionesha kuwa kivutio kikubwa mbali na umahili wake wa kujiamini wakati wa kujibu maswali jambo ambalo lilichangia kumletea ushindi.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo Sabrina Juma akiwa katika vazi la jioni
Mbunge wa Jimbo la Sengerma Bw.William Ngereja akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya uermbo yaliyofanyika
Warembo wakipita jukwaani kila mmoja akionesha uwezo wake mbele umati mkubwa wa wakazi wa Tabora waliofurika kushuhudia shindano hilo.

Saturday, June 1, 2013

MWAKASAKA AKUSUDIA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA KATIKA MICHEZO TABORA

Mjumbe wa kamati ya uchumi na Fedha jumuiya ya Wazazi mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mwanasheria ya kujitegemea Bw.Emmanuel Mwakasaka akikabidhi vifaa vya michezo Jezi na mipira kwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora kwa ajili ya kusaidia kuibua vipaji vya vijana katika Soka,Vifaa hivyo vilipokelewa na Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij.
Bw.Emmanuel Mwakasaka Kada wa CCM


Monday, May 13, 2013

WAANDISHI WA HABARI WAPO HATARINI - TUNDU LISSU


lisu1 fda6e
Mh Tundulisu akitoa Vyeti kwa wana chaso katika Haflahio,

WAANDISHI wa habari wapo katika hatari kubwa ya kutoweka nchini kutokana na kuandika maovu yanayofanywa na viongozi wa serikali.
Haya yamezungumzwa na Mbunge wa Singida Mashariki na mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu katika mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa (CHASO) katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kilichopo katika Manispaa ya Iringa.
Lissu alisema waandishi wa habari wapo katika hatari ya kutoweka hasa kwa kuuawa kutokana na ukweli wao wanaouandika hasa kuyaweka madudu ya baadhi ya viongozi wa serikali.
Alisema hasa katika ripoti ya uchunguzi ya mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ya tume iliyoundwa na vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) inaonesha wazi juu ya hatari walionayo waandishi wa habari.

Alitaja chanzo cha kuwamaliza waandishi hao kuwa ni polisi wanaotumiwa na viongozi hao kama njia ya kuzuia kuendelea kuandika madudu yao.
Hata hivyo alisema waajiri wa waandishi ni chanzo moja wapo cha kinachochangia waandishi kuwa katika hatari hiyo kwa kuwatengenezea mazingira mabovu ya utendaji wao hasa wawapo kazini.
Lissu alisema waandishi wa habari ambao wapo katika hatari kubwa ni wa Iringa ambao tayari wapo katika listi ya kupotezwa kwa namna yoyote kwa kile kilichoelezwa kuwa hawaandiki habari zao kwa unafiki.
"Tuwalinde sana waandishi wa habari kwa kweli wapo katika hatali kubwa sana. Kila mmoja awe mlinzi wa waandishi hawa na ifike mahali tukasema hatutaki Mwangosi mwingine. Hasa waandishi hawa wa Iringa wapo katika wakati mgumu sana" alisema.
Pia aliwaasa wanafunzi waliomaliza kwenda kuungana na wananchi kuendeleza harakati za Mageuzi kuanzia katika Mashina,kata, na Majimbo ili kufanikisha mpango wa kuelekea ikulu vinginevyo ni ndoto hapondipo utatokea ukombozi wa Waalimu, Madaktari, na Wanasheria
Wasio na kazi kwasababu ya Mipango mibovu ya utawala uliopo kupata furusa ya kuitumikia nchihii kukiandaliwa mipango mizuri ya ajira,
Historia inaonyesha hakuna Mzee aliefanikisha mapinduzi ya kisiasa katika nchiyake kama hakuanza wakati akiwa kijana na kuelekea katika Mafanikio ndipo uzee unamkuta akiwemo ndani ya Harakati,

WAFANYAKAZI WA MRADI WA MILENIA MBOLA WAFANYA SHEREHE


 Kiongozi wa mradi wa vijiji vya Milenia Mbola Dr.Gerson Nyadzi akizungumza katika hafla fupi ya jioni ya wafanyakazi wa Mbola Mvp ilyofanyika katika ukumbi wa Polisi mjini Tabora.
 Hapa ni wakati ulipowadia kwa wafanyakazi hao kulisakata Rumba kwa kila mmoja kwa Staili yake na akionesha ufundi juu ya hilo.
 Ilikuwa vigumu kuvumilia kwa Kiongozi wa Mradi Dr.Gerson Nyadzi kuwaachia Staff peke yao kunyoosha viungo vyao akaamua kuwasindikiza kwa kucheza Kiduku kama inavyoonekana hapa ambapo ukumbi ukachangamka.
 Ikafikia hatua hata ya viatu kuwa vizito na uchangamfu ukakolea bila kujali muda wa kukamilisha hafla hiyo ya jioni.
 Wakati wa maakuli ulipewa kipaumbele cha kwanza kabla ya mambo mengine ili kusawazisha mambo.


"DR.KAFUMU NI MBUNGE HALALI WA JIMBO LA IGUNGA"-MAHAKAMA YA RUFAA


Dr.Dalali Peter Kafumu mbunge halali wa jimbo la Igunga - Mahakama ya Rufaa kanda ya Tabora.
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya Chadema  Mwalimu Joseph Kashindye mstari wa pili kutoka kulia ni mtu wa pili aliyevaa sare ya Chadema akizungumza jambo na mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Tabora muda mfupi kabla ya kutolewa kwa maamuzi ya Mahakama ya Rufaa dhidi ya kesi ya kutenguliwa Ubunge Dr.Dalali Kafumu.


Baadhi ya viongozi wa Chadema na CCM ngazi za wilaya wakiwa mahakamani kushuhudia kesi ya rufaa ya kutenguliwa kwa matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Igunga Dr.Kafumu

Thursday, May 9, 2013

MAHAKAMA YA RUFAA YATENGUA MAAMUZI YAMREJESHEA DKT KAFUMU CCM UBUMGE‏


 

Na Lucas Raphael,Tabora

 
Mahakama ya rufaa nchini imetengua maamuzi ya mahakama kuu na kumrudishia ubunge wake Dkt Peter Dalali Kafumu – CCM wa jimbo la Igunga baada ya kuridhika ha hoja za upande wa mrufani kuwa jaji aliyesikiliza shauri hilo hakuzingatia matakwa ya kisheria.

Akisoma  uamunzi huo mwenyekiti wa jopo la majaji wa mahakama hiyo jaji Nathalia Kimaro akisaidiana na jaji William Mandia na jaji Semistrocles Kaijage amesema kuwa mlalamikiwa hakulipa ada ya mahakama kama sheria ya uchaguzi inavyoelekeza.

Aliongeza kuwa awali wakati shauri hilo namba  10/2011 linafunguliwa mahakama kuu jaji aliyelisikiliza hakusikiliza pingamizi la mrufani kwamba hakukuwa na ada iliyolipwa hivyo hakupaswa kuendelea na usikilzwaji wake.

“ kutolipwa ada ama kutokuwepo kwa kumbukumbu yoyote katika jalada la mahakama inayoonyesha kitu kiwekwa kama kinga ilikuwa ni sababu tosha ya kutosikiliza shauri hilo” walisema majaji hao katika maamuzi yao.

Katika hoja zake wakili  wa serikali Gabriel Malata  za kutaka yatenguliwe maamuzi ya mahakama kuu aliwaambia  majaji wa mahakama ya rufaa kuwa jaji aliyesikiliza kesi hiyo alikosea kuanza kuisikiliza kwani mlalamikaji hakutimiza matakwa ya kisheria.

Malata alidai kuwa mlalamikaji hakulipa ada ya mahakama kiasi cha shilingi milioni moja alizotakiwa kutoa au hati ya nyumba kabla kesi hiyo haijaanza kusikilizwa kama sheria ya uchaguzi kifungu na 111 inavyoelekeza.

Wakili Malata aliongeza kuwa kwa vile mjibu Rufaa Joseph Kashindye  na wenzake hakutekeleza sharti hilo  usikilizwaji wa shauri hilo pamoja na mwenendo mzima yakiwemo maamuzi vyote vilikuwa ni batili.

Aliongeza kuwa malalamiko yaliyopelekwa mahakama  ni ya kutengeneza kwani hayajawahi kuwasilishwa katika kamati ya maadili ya uchaguzi kama walivyofanya juu ya suala la mbunge wa Tabora mjini Ismali Aden Rage  ambaye alitozwa faini ya shilingi laki moja kwa kutembea na
silaha kwenye mkutano.

Hoja hizo na nyingine zilipingwa na wakili wa mjibu rufaa profesa Abdalah Safari ambaye aliitaka mahakama ya rufaa kuzitupilia mbali na kwamba Mahakama iliyosikiliza kesi hiyo iliridhika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa jimbo la Igunga ndipo katengua matokea.

Kukatwa rufaa hiyo kunafuatia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani hapa baada ya kubainika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura.

Jaji Mary Nsimbo Shangali wa mahakama kuu Agasti 21 mwaka jana alitangaza kutengua matokeo hayo baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba  zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji  kati ya hoja  19 zilizowasilishwa katika mahakama hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Joseph kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili Maarufu nchini Profesa Abdallah Safari  ambapo alipinga matokeo ya uchaguzi huo akilalamikia kukiukwa kwa sheria ya uchaguzi mkuu.

Upande wa Utetezi  uliwakilishwa na  mawakili Mohamed Salum Malik na Gabriel Malata kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali,Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga,  na mawakili Antony Kanyama na Kamaliza Kayaga waliokuwa wakimtetea mbunge wa Igunga Dkt Peter Dalali Kafumu.

Akisoma hukumu jaji Shangali alizitaja baadhi ya kasoro zilizopelekea kutengeliwa kwa uchaguzi huo ni pamoja na  Ahadi  iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi  Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu  ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo alidai kwamba  kama wananchi hawataichagua CCM daraja hilo halitajengwa, wakati ambapo katika kipindi hicho kulikuwa na shida kubwa ya usafiri katika eneo hilo.

Alisema Kitendo pia kilichofanywa na mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage, hakikuwa cha uungwana kwani alitumia lugha ya uongo kwa lengo la kupotosha wapiga kura ambapo alidai mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo  ( Chadema) amejitoa katika uchaguzi huo.

akizungumza na gazeti hili mara baada ya maamuzi hayo nje ya mahakama aliyekuwa mjibu rufaa  Joseph Kashndye  amekubali na kuridhika na maamuzi hayo  huku akiwalalamikia mawakili wake kwamba hawakumwelekeza kufanya hivyo.

“ Sikujua, sikuelezwa  hili ni tatizo la kiufundi  hivyo silaumu” alisema  Kashindye.

Umati wa wananchama wa chadema ambao ulijaa ndani ya chumba cha mahakama kwakweli uliondoka kwa uzuni eneo hilo la mahakama wakikibali matokeo huku wengine wakisema tukajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao

Hata hivyo Dkt kafumu akuwepo mahakamani alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kwamba hukumu iliyotewa na mahakama ya Rufaa ndio haki kamili kwani mwanzo alikuwa na wasiswasi na jaji yule lakini alionekana anaongopa kuangushwa .
Alisema kwamba amerejeshwa ubunge wake kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Igunga bila kujali Itikadi ya chama chochiote cha siasa kwani waliompa kura na kumyima kura wote ni wananchi wa Igunga.

Dkt Kafumu alisema kwamba yale ambayo alikuwa hameyaanzisha ndio anataka kuendeleza kwa nguvu zake zote kwa ajili ya maendeleo ya Igunga na wananchi wake  kwa ujumla.

“mimi nijembe kama nilivyokuwa nasema wakati wa kampeni zangu kwamba mimi ni kwa ajili ya wananchi wa Igunga hasa vijana na wale wa vyama Rafiki na ccm “alisema Dkt Kafumu.

Aidha mwenyekiti wa ccm wilaya ya Igunga Costa Olomi alisema kwa ushindi wa kafumu ni wananchi wote wa Igunga sio wa chama bali ni kwajii ya maendeleo ya Igunga na mkoa wa Tabora .

Alisema kwamba baaada ya kurejeshwa umbunge wake chama cha mapinduzi kimepanga mapokezi makubwa ya kupokea mbunge huyo hapa mei 12 mwaka huu kwa ajili ya sherehe ya kupongeza .

MWISHO.