MSHINDI
wa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa mwaka 2014 Afrika imekwenda kwa
mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi.
Hapajawahi
kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora
kutoka Algeria kuishinda tuzo hiyo, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa
tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe nyingi.
Brahimi
amewabwaga wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang
wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na
hatimaye Yaya Toure aliyechukua tuzo hilo mwaka jana.
TAKRIBANI
watu 36 wanahofiwa kufariki katika shambulio lililotokea kwenye
machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Shirika
la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limethibitisha.
Wakazi
wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio
Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo
Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio
hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28
waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab limekiri kuhusika na mauaji hayo.
Sasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House
Mfanyakazi
katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya
kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha
na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi
Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake
wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi
kwenye hafla ya jioni.
Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
Rais
Jakaya Mrisho kikwete akimuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam
Disemba 02, 2014
Rais
Jakaya Mrisho kikwete akitia sahihi yake kwenye nyaraka baada ya
kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa
Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Disemba 12, 2014
Rais
Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku na
kumpendekeza waziri mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi hio.
Wakati
huohuo mkuu wa polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo
amejiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yake afanye hivyo kwa kushindwa
kukabiliana na utovu wa usalama nchini.
Rais
Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali
'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Rais
alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo
jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera
Kaskazini ya Kenya.
Aliyekuwa mkuu wa polisi David Kimaiyo
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.
Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.
Hatua
ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa
jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu
wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.
Uteuzi
wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani
atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.
Alipokuwa
anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza mda wa vikao
vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua
nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili
wamuidhinishe.crdt BBC Swahili
Mkuu
wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akipokea msaada wa shuka kwa ajili ya
wagonjwa wa Zahanati ya kijiji cha Ubinga zilizotolewa na Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ambapo Afisa Matekelezo wa mfuko
huo Sunday Matoi alikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Nzega kabla
ya kufanya ufunguzi wa majengo mapya ya zahanati ya Ubinga..
Mkuu
wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akifungua Zahanati ya Ubinga wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii katika
kata ya Muhugi wilayani Nzega
Mkuu
wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akizungumza na wananchi mara baada ya
kufanya ufunguzi wa zahanati ya Ubinga na kukagua majengo ya zahanati
hiyo na baadae kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
hatua ambayo itawasaidia kupata huduma bora za matibabu katika familia
zao pindi wanapopata matatizo ya kuugua.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Ubinga wakimsikiliza kwa makini mkuu wa
wilaya ya Nzega Bituni Msangi wakati akihamasisha wananchi kujiunga na
Mfuko wa Afya ya Jamii CHF.
Mkuu
wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akikagua moja kati ya timu
zilizoshiriki mashindano yaliyolenga kuwahamasisha wananchi kujiunga na
Mfuko wa Afya ya Jamii katika kata ya Muhugi wilayani Nzega.
Safari ya mwisho wa mwandishi wa habari wa siku nyingi Hamis
Bakari kikoroma maarufu kama Ben kiko (70) ilitimishwa jana katika kijiji cha
ndaukilo kitogoji cha usupilo wilayani sikonge mkoani Tabora katika mazishi
yaliohudhuriwa na watu mbalimbali mkoani
hapa.
Mazishi hayo yakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani
Kumchaya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa tabora Fatuma mwassa naambapo aliwataka waahdishi wa habari
hapa nchini kuinga yale yote yaliomema
aliyofanya mwandishi huyo mkongwe hapa nchini
Alisema kwamba kwamba waandishi wa habari na vijana kwa ujuma
wake wanatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi
yao kama alivufanya marehemu katika uhai wake kwa kutumikia nchi yake katika
vita ya kagera na sehemu mbalimbali ambazo alifanya kazi kwa kujituma .
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kila mtu anatakiwa kujitoa
kwa ajili ya nchi yake na sio kuweka maslahi ubinafsi mbele kwani huo sio uzalendo bali kutoa
kwa nchi kama alivufanya ben kiko wakati wa utendaji wake wakazi.
Alisema kwamba licha ya kufanya kazi tbc kwa vipindi tofauti tofauti
bali alikuwa ni mfanyakazi katika Redio ya Tabora VOT na kuwa mwalimu wa waandishi
wa habari katika mchuo cha musoma Utalii Tawi la Tabora .
Marehemu amepata elimu shule ya msingi misheni sikonge kabla
ya kwenda chabutwa kusoma elimu ya kati mwaka 1959-1962 shule ya wavulana
tabora kidato nne kabla ya kuhudhuri mafunzo ya ualimu ya miaka miwili katika
chuo cha ulimu mpwapwa mkoani Dodoma na kufanikiwa kupata cheti cha ualimu daraja A.
Aidha mwaka 1984-1985 alikwenda nchini India kupata mafunzo ya
uandishi wa habari ya ngazi ya Diploma .
Ben kiko hadi mauti yanamfika alikuwa mwenyekiti wa mtaa wa
uhazili uliopo katika kata ya kanyenye manispaa ya Tabora ameacha wajane watatu na watoto kumi.
MWILI WA MWANDISHI WA HABARI ZA SIKU NYINGI BEN KIKO UKIINGIZWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE .
SHEKHE SALUM
MAHARUKI AKIONGOZA SALA YA KUUONBEA MWIILI WA MWANDISHI WA SIKU NYINGI
NCHI HABARI BEN KIKO NJE YA NYUMBANI YAKE KATIKA KIJIJI CHA USUPILO
WILAYA YA SIKONGE MKOANI HAPA
WANANCHI KUTOKA TABORA MJINI NA WALE WA WILAYA YA SIKONGE WAKIWA KATIKA MKUSANYIKO WA KUKAMILISHA SAFARI WA BEN KIKO