Wednesday, December 3, 2014

NHIF WAZINDUA KAMPENI YA MFUKO WA AFYA YA JAMII VIJIJI VYA NZEGA


Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akipokea msaada wa shuka kwa ajili ya wagonjwa wa Zahanati ya kijiji cha Ubinga zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ambapo Afisa Matekelezo wa mfuko huo Sunday Matoi alikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Nzega kabla ya kufanya ufunguzi wa majengo mapya ya zahanati ya Ubinga..

Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akifungua Zahanati ya Ubinga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii katika kata ya Muhugi wilayani Nzega
Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akizungumza na wananchi mara baada ya kufanya ufunguzi wa zahanati ya Ubinga na kukagua majengo ya zahanati hiyo na baadae kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii hatua ambayo itawasaidia kupata huduma bora za matibabu katika familia zao pindi wanapopata matatizo ya kuugua.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ubinga wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi wakati akihamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF.
Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi akikagua moja kati ya timu zilizoshiriki mashindano yaliyolenga kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii katika kata ya Muhugi wilayani Nzega.


No comments:

Post a Comment