Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Baada
ya kuchapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa soka Simba SC katika mchezo wa
‘ Hisani Nani Mtani Jembe’ siku ya Jumamosi iliyopita, klabu ya Yanga
SC imeamua kufikia maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha Marcio Maximo na
ni wazi Mholanzi, Hans Van De Pluijm atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara
ya pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao mara baada ya kufungwa na
Simba. Ikumbukwe mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie Brandts aliondoshwa
baada ya kufungwa mabao 3-1 katika Mtani Jembe.
Tofauti
na ilivyokuwa kwa Brandts ambaye aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na
kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13,
Maximo yeye amefukuzwa baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo tisa
ndani ya miezi mitatu. Yanga imepoteza michezo miwili kati ya saba ya
ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza vizuri klabuni hapo kwa
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii,
alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar katika
uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Yanga
imeshinda michezo minne msimu huu, lakini hadi l,igi inasimama katika
raundi ya saba hakuna mtu alikuwa na shaka kuhusu uwezo wa Maximo. Kocha
huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amechokwa
haraka sana na mashabiki, wapenzi, wanachama na viongozi wa klabu yake
kutokana na kiwango kidogo cha uchezaji. Mifumo yake ya ufundishaji
imekosa mvuto, lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba kimeshindwa
kuvumilika.
COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo
sababu kubwa, ukitoa mbinu zake, Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi
wachezaji raia wa Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos ( ambaye
aliomba mwenyewe kuachwa baada ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira
siwezi kuzungumzia kwa sababu mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo alicheza
katika kiwango cha kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya
kwanza.
Jaja
alifunga mara mbili dhidi ya Azam, ila alikosa makali katika ligi kuu
kiasi cha kufunga bao moja tu katika michezo saba ya ligi kuu.
Alishindwa kumudu presha ya mashabiki wa Yanga ambao hawakuwa
wakipendezwa na kiwango chake huku uchezaji wake wa taratibu ukiwaboa
wengi. Maximo aliwanyima nafasi washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry
Tegete, Saimon Msuva, Hussein Javu na Hamis Kizza hata pale wachezaji
hao wa Kibrazil waliposhindwa kufanya vizuri.
Kuwang’ang’ania
wachezaji hao na kuwanyima nafasi wale wenye uwezo kumewakera . Brandts
aliondolewa baada ya kufungwa 3-1 licha ya kusaini mkataba mpya wa
miaka miwili zaidi, yeye aliondolewa kwa kuwa alipingana na uamuzi wa
viongozi kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.
Brandts
ndiye mwalimu aliyeifanya Yanga kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na
ndiye aliyeimarisha kiwango cha wachezaji kama, Saimon Msuva, Frank
Domayo ( yuko Azam FC kwa sasa), Juma Abdul, Oscar Joshua na wengineo
lakini kwa Maximo imekuwa ni tofauti, wachezaji wengi wameshuka viwango
na ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao ‘ wanasua-sua’. Yanga
wamefanya uamuzi sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.
No comments:
Post a Comment