December 16, 2014: Watanzania waendelea kufaidika
kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini India. Hii ni kufuatia hosiptali
hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni
kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014
nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama
Thoraco Omphalopahus na upasuaji
uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana
na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya
kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini
yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji
wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha
damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari
waliokuwepo wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50
waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya
upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11. Watalaamu
walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa vimeungana lakini mapacha hawa
walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada
ya upasuaji.
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika
upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya
kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt.
K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya
upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia
mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo
mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo
katika mahala pake.”
Upasuaji huu wa mafanikio wa mapacha
waliounganika kutoka ncini Tanzania sio wa kwanza kufanywa na hospitali ya
Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha wengine wakiume waliokuwa wameungana na
kujulikana na wataalamu kama Pygopagus,
Ericana & Eluidi kutoka Tanzania
walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment